Mkurugenzi wa Uhusiano na Kitengo cha Sheria wa TBL, Steve Kilindo, akitoa maelezo kwa Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi cha Anga kuhusu historia ya kampuni hiyo.
Meneja wa Masuala ya Usalama mahali pa kazi wa TBL, Renatus Nyanda, akielezea kuhusu hatua mbalimbali za uzalishaji wa bia kiwandani hapo.
Meneja Ubora wa Bidhaa za TBL, Lydia Soi akitoa maelezo jinsi wanavyodhibiti ubora wa bidhaa kiwandani hapo.
Ofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kikosi cha Anga, akielekezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni yaYour Solution Tanzania Limited, Damian George, jinsi ya kukitumia kifaa cha kisasa cha kuzimia moto kiitwacho DSPA, walipotembelea kiwanda cha bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, kujifunza masuala ya usalama kazini, afya za wafanyakazi na utunzaji wa mazingira.
Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kikosi cha Anga, wakitembelea kiwanda cha bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, sehemu ya matanki yanayotumika kuchachulia bia. Askari hao walifanya ziara ya kujifunza masuala ya usalama kazini, afya kwa wafanyakazi na mazingira.
Askari wakiangalia unga wa mahindi unaotumika kutengenezea bia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. DU! KUMBEEE NAJUA KUNYWA TU JAMANI, MAHINDI NDIYO YANAYOTENGENEZEA BIA? MARA OOOO KIMEA, SHAIRI, NGANO, AMA KWELI TEMBEA UJIONEE NILIKUWA SIJUI

    ReplyDelete
  2. jamani watu wanakufa na njaa tanzania hii hii na afrika kwa ujumla nyie mwatumia mahindi kutengenezea kilevi?

    ReplyDelete
  3. Sasa hawa wanajeshi na bia wapi na wapi ndo maana wengi wao ni kina-chapombe!

    ReplyDelete
  4. Mdau wa tatu hapo juu,

    Dalili ya Wanaulinzi JWTZ kutembelea Kiwanda cha Pombe ni kutoa salamu kwa Mamlaka kuwatuma ktk Mission za Amani ili wakavute $$$ (DOLA) zao huku wakitumikia taaluma yao.

    ReplyDelete
  5. CHADEMA fanyeni Sherehe zenu za Ushindi wa Uchaguzi kwa amani na ustaarabu,

    -Arumeru Mashariki (Ubunge)
    -Mbeya (Kata)
    -Kirumba Mwanza (Kata)

    Mkileta fyokooo wenyewe mtayavua magwanda yenu ya Mgambo na kukimbia,,,tutawatumia hawa jamaa (Majeshi) ili wawatoe kamasi!

    ReplyDelete
  6. Msifikiri wapo likizo:

    Wazee wa Kazi, Wazee wa Mtarimbo wanatembelea Kiwanda cha pombe kuwavutia pumzi Chadema na vurugu zenu.

    Mkileta nyokooo sisi Watawala wa Nchi na Chama chetu tutawatumia Madege ya Majeshi mkione cha mtema kuni!

    Mtatafutana ndani ya mashamba ya mikahawa na midizi Arumeru Mashariki!

    ReplyDelete
  7. JWTZ yahusika nini na kiwanda cha bia.Mambo mengine yanahitaji common sense.

    ReplyDelete
  8. Kwanza kabisa; fuatilieni kilichowapeleka hapo, kimeandikwa hapahapa na kama huelewi rudia tena na tena kabla hujamuuliza mwenzio. Pili; wanajeshi na siasa kinadharia ni vitu viwili tofauti kabisaaa, kwa hiyo msiingize siasa wanapokuwepo hawa, na mwisho kabisa wewe unayejiita 'sisi watawala' unayetishia kuingiza mkono wa jeshi unaelekea kufilisika kisiasa kabisaaa! Umeshatengeneza mazingira ya dalili za kushindwa kwa 'watawala wenzako'....jeshi kupigana na wapinzani wa chama tawala?.......aibu hiyo!

    ReplyDelete
  9. Cha Muhimu hapa ni Chadema pamoja na Ushindi wao ujumbe ni kuwa waendelee kuiheshimu Mamlaka na Serikali.

    Ushindi wa uchaguzi katika Jimbo moja (Arumeru Mashariki) na Kata 2 (Mbeya na Kurumba Mwanza) hauhalalishi wao kwa fujo, vurugu na majigambo kuitawala nchi nzima!

    Ama sivyo kwa ujinga wao huo ndio Majeshi yatatumika katika Siasa na ndipo kamasi zitawatoka!

    ReplyDelete
  10. Hakuna jukumu gumu kama kuwatawala genge la ''Wachagga wachache wanaohesabika na Chama chao'' wakorofi wasiyejua Siasa na ustaraabu wasiozidi milioni 5 tu katika nchi ya watu milioni 45, isipokuwa kwa kutumia Jeshi na Mabavu !

    ReplyDelete
  11. Hivi wengine mnakurupuka?mbona kilichowapeleka hao wanajesh kimeandikwa au ndio sifa ilimrad na ww umecoment?kama haujaelewa jarib kurudia kusoma kabla ya ku coment achen ulimbuken

    ReplyDelete
  12. Hiyo Mdau unaetoa Maoni na kuishia ....?kama haujaelewa jarib kurudia kusoma kabla ya ku coment achen ulimbuken....

    Blogu ya Jamii kusudio lake ni kuwaeleza wasioelewa kuwa SIASA haishirikiani na MAJESHI isipokuwa waoendesha hiyo Siasa WAKIYAALIKA MAJESHI KWA KUONYESHA DALILI ZA UCHOCHEZI NA UVUNJAJI AMANI,,,,AH AH AH AHA YATAWASHUKIA KAMA MWEWE!!!,,,MAJESHI HAYATAPATA MUDA WA KUTEMBELEA KIWANDA CHA POMBE NA BADALA YAKE YATAWAANGUKIA KWA KIPONDO WANASIASA WAKOROFI KAMA CHADEMA!

    ReplyDelete
  13. Majeshi yapo matembezini Kiwanda cha Pombe,,,Hukumu ya Kesi Jimbo la Arusha Mjini imetoka asubuhi leo,,,Majeshi yamekaa tayari na yanaweza simamisha ziara za matembezi yao ili kuwaangukia Chadema Arusha kama wataelata Ujinga !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...