Balozi wa Indonesia Nchini Tanzania , Mh Yudhistiranto Sungadi (kushoto) akimkabidhi Diwani wa Wadi ya Kikwajuni , Mahboub Juma Issa miche ya Minazi iliyotolewa na ubalozi wake kwa jumuia ya Imarisha Mazingira Zanzibar (JIMZ) ambapo inategemewa kupandwa katika eneo la Kizingi mjini Zanzibar
Balozi wa Indonesia Nchini Tanzania , Mh Yudhistiranto Sungadi (kushoto) akipanda mti kuashiria uzinduzi wa kampeni ya upandaji wa miti katika eneo la Kizingo mjini Zanzibar, ambapo miti ipatayo 3,000 inategemewa kupandwa , zoezi hilo linafanywa na Jumuia ya imarisha mazingira Zanzibar (JIMZ) ya Kikwajuni kulia katibu wa Jumuia hiyo Rajab Ali na Diwani wa wadi ya Kikwajuni Mahboub Juma Issa.(Picha na Haroub Hussein).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. sasa hiyo ni miti au maua?

    ReplyDelete
  2. Ndio, kuna tofauti kati ya miti (tree) na mimea (plants). Mnazi naona uko kwenye kundi la (monocotyledon), miti ni dicontiledons). Miti hudumu kwa miaka mingi wakati minazi (plants) inenda kwa misimu michache. Minazi(palmae), nyanya au mawese haina tofauti na mahindi au cabbage. Ile ya muda mfupi ilopandwa DSM, Mkuranga na Kisarawe ilishafikia ukomo wake siku nyingi. Kinachofanyika hapa ni uboreshaji wa mazingira na sio upandaji miti. Nisaidieni Botanists. Mazingira

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza hii ni miti aina ya minazi.

    Mradi ni mzuri ila tunaomba uwe endelevu kwa kuhakikisha miti iliyogharimu fedha inatunzwa hadi kukuwa kwake. Isijetokea miti hii inapandwa leo na kesho ikaibiwa na wezi wa mimea, kufanyiwa hujuma za makusudi au kutelekezwa.

    Kwa uzowefu kumekuwapo na mpango wa upandaji miti kila mwaka lakini utuzaji unakosekana na hivyo kutofikia malengo yaliyokusudiwa. Wanajumuiya watueleze wanampango gani kuhakikisha miti hii inatuzwa.

    Ndugu Hifadhi Mazingira ya nchi yako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...