Mh.Balozi Mohamed Haji Hamza Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri, alikua ni mgeni rasmi katika sherehe maalum ya kuwatunuku wanafunzi waliofanya vizuri katika lugha ya kiswahili katika kitivu cha lugha za kigeni na tafsiri ya lugha za kiafrika katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar kilichopo mjini Cairo Misri. 

Sherehe hiyo iliyofanyika tarehe 24 April 2012 kwenye ukumbi wa Chuo hicho. Balozi Hamza amesifu ushirikiano wa siku nyingi uliokuwepo kati ya Misri na Tanzania katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na maendeleo ya jamii. 

Pia Mh. Balozi alisisitiza juu ya umuhimu wa kuimarisha uhusiano kati ya chuo kikuu cha Al-Azhar na vyuo vikuu vya Tanzania katika kubadilishana wataalamu na watafiti pamoja na kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka Tanzania kujiunga katika chuo hicho kila mwaka.
 Mh. Balozi (katikati mwenye tai nyekundu) akisisitiza uhusiano wa kijamii  na utafiti mbalimbali baina ya mataifa hayo.
 Mh.Balozi Hamza  akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliotunukiwa zawadi, ama wambele walioketi kutoka kulia ni Profesa Saeed Atiah Aly, Mkuu wa kituo cha lugha cha lugha ya kigeni na ukalimani. wapili ni Mh. Balozi Mohamed Haji Hamza Balozi wa Tanzania Misri. watatu ni Professor Ali Ahmed  Shaaban Mhadhiri Mkuu wa lugha za kigeni na wa mwisho Nd. Idriss Kh. Juma  Afisa Mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania Cairo Misri.

Mh. Balozi Hamza akiwa kwenye picha ya pamoja na wakuu wa idara na wahadhiri wa kituo  cha lugha za kigeni na tafsiri ya lugha za kiafrika katika chuo kikuu cha Al-Azhar Cairo Misri.   

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...