Home
Unlabelled
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
kaka michu na wana libeneke wote, shikamooni.HOJA yangu ni hii,niko huku America,sina hamu naomba msaada wa kuonyeshwa njia ya kurudi kwetu shinyanga,nilikuja huku miaka ya zamani kidogo,nikajidanganya kuoa mzungu,tumezaa mtoto mmoja na sasa hivi mimi na mzungu tulikwisha achana,ila tu sheria za huku lazima niendelee kulipa pesa za mtoto hadi atakapotimiza miaka 18.hili siliioni kuwa jambo baya,ninazilipa hizo pesa kwa roho moja ila ndo sina madaraka na mtoto wangu,hata kumwa-dabisha siwezi,ana ishi na mama yake, nguo anazovaa ni zile za aibu tupu,vigolori kwenye ulimi,nywere zake anapaka rangi mbali mbali,nyumbani kurudi ni usiku wa manane,kushika kitabu kusoma hiyo ni ndoto,shuleni pia hafanyi vizuri. Mke wa kizungu kanitia adabu,maana niliolewa na siyo kwamba nilioa,nyumba nisafishe,vyombo nioshe,nguo nifue,nimevumilia mpaka kifua kikajaa,achilia mbali mke kunifokea,kitendo cha ndoa nilikuwa sipewi mpaka hapo yeye anapojisikia.well lenye mwanzo linamwisho,tumeachana na sasa naomba tu ushauri wa anayejua namna ya kuirudisha hii passpoti yao mimi nirudi kwetu shinyanga,huku si pahala pa kuzeekea hata kidogo, miaka kadha iliyopita nilirudi bongo na nikashuhudia vijana niliosoma nao wana maisha mazuri kunishinda mie,wana familia zao na zenye heshima kubwa,watoto wao wanasafisha meza baada ya chakula na kuondoa vyombo mezani na wana watuma sokoni!! mtoto wangu ,kila baada ya neno lazima atumie F.Angelikuwa Shinyanga ,asinge behave namna hii.Jamani hili lipasipoti lao silitaki,naomba nirudi bongo.Nina ki akiba kidogo cha dola elfu 50, hata biashara ya ngombe nitafanya. asanteni wale wote wenye nia njema ya kunishauri ,pia na wale wenye upeo mfinyu wa kuponda kila jambo nao nitawashukuru,maana kwenye msafara wa mamba, kenge nao hawakosekani.ni mimi ,Mna Ntuzu o,Bariadi.
ReplyDelete