Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la Makatibu Muhtasi nchini Tanzania (2th National Secretarial Confrerence) linaloendelea hivi sasa kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika Beach Resort,Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa Mwanza,Eng.Evarist Ndikilo akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la Makatibu Muhtasi nchini Tanzania (2th National Secretarial Confrerence) linaloendelea hivi sasa kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika Beach Resort,Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Pili Penda akitoa maelezo mafupi ya Kongamano hilo kwa Mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu wakati wa ufunguzi uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika Beach Resort,Jijini Mwanza.
Baadhi ya Makatibu Muhtasi waliohudhuria kongamano hili
au
Kuna pengo kubwa baina ya wanawake na wanaume katika kazi hii ya ukatibu muhtasi!!
ReplyDeletehongereni lakini jiendelezeni, maana nyie ndio mnajua ofisi kuliko mabosi wenu na kazi yenu ni makini. Kero yangu ni kwamba hii kazi inaonekana ni ya wanawake anagalia walivyojazana hapo
ReplyDeleteNadhani muda si mrefu hata makatibu muhtasi wanaume wataongezeka. Unajua huki cheo kimekuwepo toka kipindi cha mfumo dume wa kiutawala. Wakati huo mabosi wengi walikuwa wanaume. Hao wasichana (makatibu muhtasi)pamoja na kazi nyingine, kazi mojawapo ilikuwa ni ku-take care bosi wa kiume. Kwa ufupi huyu huitwa mke wa pili wa bosi. Baada ya muda kadhaa, anaenda kumuuliza bosi nikuletee nini? Mara anamtengeneza vizuri kola ya shati au tai. Ikibidi hata anampatia kidogo kitumbua chake.
ReplyDeleteHawa wana kazi kubwa, kwa kawaida wanatunza kumbukumbu za kampuni. Wanajua kila kinachoendelea na wanajua taratibu za kampuni kuliko baadhi ya mabosi. Waongezwe mshahara na malupulupu, kwa kweli kazi yao ni nzito kuliko watu wengi wa ngazi yao au wengine wenye kazi za kikarani.
ReplyDeleteWengi wamejiendeleza ili kuwa sambamba na technolojia ya electronic. wanaweza kutunza mahesabu na kukusanya takwimu ( database). Wanajua mabo ya human resources na administration kwa ujumla. Mungu awaongezee ushupavu.