Waziri wa Miundo mbunu na mawasiliano Mh Hamad Masoud Hamadi akizundua Rasmi Bodi mpya ya mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar leo huko Unguja.
Mwenyekiti wa Bodi mpya ya mamlaka ya Viwanja vya Ndege Bw Abdulhalim Msoma akitoa neno la shukurani kwa Waziri wa Miundombinu na Mwasiliano pamoja na Uongozi mzima wa mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar kulia kwake ni Waziri wa Miundombinu na Mawasilino Mh Hamad Masoud Hamad na kushoto ni mjumbe wa Bodi kutoka Polis Zanzibar na Mwengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Viwanja vya Ndege Zanzibar.
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mh Hamad Masoud Hamad (shoto) akimkabidhi nyenzo za kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Abdullhalim Msoma huko katika ukumbi wa Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.
Waziri wa Mawasiliano akiwa katika Picha ya pamoja na Bodi mpya ya Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar.
PICHA NA NAFISA MADAI- MAELEZO ZANZIBAR.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...