![]() |
Mbunge mteule wa Arumeru Mashariki Mh. Joshua Nasari akiongea baada ya kutangazwa kuwa mshindi asubuhi hii huko Arumeru |
Matokeo ya kura za Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki yametangazwa sasa hivi na Msimamizi wa Uchaguzi na Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru Bw Gracias Kagenzi amemtangaza mgombea wa CHADEMA Bw Joshua Nassari kuwa mshindi baada ya kupata kura 32,972 dhidi ya mpinzani wake wa karibu kutoka CCM Bw Sioi Sumari aliyepata kura 26,757
Matokeo kwa Vyama vingine sita vilivyoshiriki ni kama ifuatavyo
DP -77
NRA - 35
AFP - 139
UPDB - 18
TLP - 18
SAU - 22
Kwa mujibu wa Bw Kagenzi zaidi ya watu 120,000 walijiandikisha na aliojitokeza na kupiga kura walikuwa 60,696 ambapo kura halali zilikuwa 60,038 na zilizoharibika ni kura 661.
HUKO MWANZA NAKO...
Wakati huo huo, habari kutoka Mwanza zinasema CHADEMA kimeshinda katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kirumba mkoani Mwanza.
Msimamizi wa uchaguzi huo, Bw. Aloyce Mkono, amemtangaza kuwa mshindi mgombea wa Chadema Mh Dany Kahungu kwa kura 2,938 dhidi ya mgombea wa CCM Mh Jackson Masamaki aaliyepata kura 2,131.
Wagombea wengine walioshindwa vibaya katika uchaguzi ni pamoja na Mh Haji Issa wa CUF aliyepata kura 184, Mh Kasala Muhana wa UDP amepata kura 7 na Mh Athuman Jumanne wa NCCR Mageuzi aliyeambulia 0 katika uchaguzi huo .
Msimamizi huyo alisema kuwa uchaguzi huo umefanyika katika hali ya amani na utulivu,na kuwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo na kuonyesha utulivu mkubwa wakati wa uchaguzi na zoezi la kutangazwa kwa matokeo.
Sasa huyo wa NCCR aliyepata zero Ina maana hata yeye hakujipigia?
ReplyDeleteTanzania is changing. Africa is changing!
ReplyDeleteWhat makes me wonder is where were the 60,000 voters who although registered did not turn up to vote?. I suspect majority of these absconders are students & youth in general. What a shame really. Now only 26% out of 100% have decided who would represent Arumeru East. Efforts should be made to educate young people on the importance of voting and driving changes in our society. alex bura, dar
ReplyDeleteSAFIIIIIII SANA JAMANI NIMEFURAHI MTOTO MBICHI MIAKA 26 TU ANAJIAMINI.CCM WAJIPANGE VIZURI 2015 WASIPANDE JUKWAANI NA KUTUKANA WAOMBE KURA TU KISTAARABU LUSINDE KAWAPONZA. WATAJIBEBA. LOWASA PRESHA INAPANDA PRESHA INASHUKA. POLENI SANA WANA CCM
ReplyDeletePipoooooooooooooz! Pawaaaaaaaaaaaaaa!
ReplyDeleteHongereni wananchi wa Arumeru. Mmeniwakilisha vyema kwa kweli! Duh!
Na nyie wa upinzani nao it is high time mfanye kitu chenye akili. Kuna haja gani ya kushiriki uchaguzi hafu hata wewe mwenyewe hujipigii kura? Si nyote mngekubaliana mkawapoa Chadema? Ubinafsi tuuuuu! Aggrrrh!
huyo wa NCCR-Mageuzi , inaonyesha ALIKUWA MZUGAJI.
ReplyDeleteANATAKIWA AKAJIELEZE MAKAO MAKUU. HUYU NDIO WALE MAMLUKI WA CHAMA.
NCCR-MAGEUZI OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
Tumeshinda na Udiwani Mbeya na Songea!!Na bado...Tanzania childhood inakuja 2015!!
ReplyDeleteDavid V
Ukisikia gharama chafu ya kuubeba Ufisadi matokeo yake ndio haya Arumeru Mashariki haya C.C.M,,,,,,,KAZI KWENU !
ReplyDeleteAwali zuri
ReplyDeleteMATOKEO YA UCHAGUZI ARUMERU MASHARIKI:
ReplyDeleteImethibitika kuwa,
Zile zama za 'TAWALA ZA KIUKOO, na 'SIASA ZA KIUKOO' sasa zimekwisha !
ccm bye bye bye!!!!
ReplyDeleteWapi CCM? Chezea Peoples Power ww. Big Congrats to Chedema. Very SOrry to CCM.
ReplyDeleteKUANGUKA KWA CHAMA TAWALA ARUMERU MASHARIKI:
ReplyDeleteKitu kibaya zaidi Mgombea wa Chama Tawala alikuwa 'Mgongoni mwa Fisadi' huku kada huyo wa Chama akiwa ni Baba Mkwe wake !
HONGERA SANA JOSHUA NA CHADEMA KWA UJUMLA, MNASTAHILI!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteC.C.M ijifunze kuwa Siasa za Upendeleo hazifai kabisa tena mbaya zaidi kumkataa Sarakikya aliyekuwa safi akapewa mtu aliyekuwa na nasaba na Ukoo uliochafuka nchini !
ReplyDeleteHata sioi na mshindi pia hawakujipigia kura, kwani walijiandikishia sehemu nyingine. Sioi hata huko Arumeru alikuwaga hajawahi kupafika, yeye alizowea mbezi beach. Karibu tena mbezi beach kaka, nimefungua mzigo mpya pale pale dukani kwangu, kuna suruali, mashati, pafyumu na hereni kibao, chaguo lako. Mama D.
ReplyDeletehongereni wana ARUMERU kwa kupata uhuru.
ReplyDeleteMatokeo ya Uchaguzi wa Arumeru Mashariki,
ReplyDeleteMbona unaweka picha moja tu?
Tunafahamu kuwa Michuzi wewe ni Kada wa Chama tawala na pia wewe ni Yanga Damu na Pia wewe ni Liverpool !
Fundisho na Aibu kubwa,
ReplyDeleteCCM mnakubalika sana isipokuwa mnajishusha wenyewe kwa Siasa zenu za Upendeleo zitakazo wagharimu sana kwa kipindi hiki cha Dunia ya Mageuzi ya Kisiasa.
Watu sasa sio ng'ombe wa kuelekezwa kila upande na wakaunga msafara.
SIOI ni muda wake sasa AOE kwa vile ameshapigwa mweleka !
ReplyDeleteWala asiwe na wasiwasi wa kazi baada ya kushindwa Uchaguzi!
ReplyDeleteKazi ni kazi bora mkono wende kinywani, mwanaume hasa Mmasai hachagui kazi !
Mgombea wa Chama Tawala aende akachunge ng'ombe wa baba mkwe wake Monduli.
Mkoa ule sio wenu ssm, mtu hadanganyiki pale sasa ivi. Poleni sana, hongera chadema!!!
ReplyDeleteSiyoi
ReplyDeleteLusinde
Lowasa
Mkapa
Wassira
Nape
Mwigulu
Wamekighalimu chama Arumeru hawa jamaa hawana mvuto kwa wapiga kura.
Mwana CCM damu damu
Wala asiwe na wasiwasi wa kazi baada ya kushindwa Uchaguzi!
ReplyDeleteKazi ni kazi bora mkono wende kinywani, mwanaume hasa Mmasai hachagui kazi !
Mgombea wa Chama Tawala aende akachunge ng'ombe wa baba mkwe wake Monduli.
Siasa ni biashara ngumu sana kwa sasa,,,ni sawa na kukalia kuti kavu!
ReplyDeleteHaya kumekucha TZ, wale waliosema kutumia helkopter ni hasara na kufilisika kwa CHADEMA mupo.
ReplyDeleteBwana LIVINGSTONE LUSINDE aibuuuuu sijui utaificha wapi sura tako na mitusi yote ile uliyotukana! WELL DONE WANA ARUMERU.
ReplyDeleteAhhh wapi Sioi aende SACCOS akachukue Mkopo aanze kuuza Vocha za simu Sokoni Tengeru !
ReplyDeleteArumeru Oyeeeeeee!!!!
ReplyDeleteSiasa za Manyau nyau sasa basi !
Hii ndo Demokrasia ya kweli, mapambano ndo yanaanza, Watanzania wa sasa hawaangalii sifa za chama wala ahadi hewa, amechoka na ufisadi, efedhuli na dhuluma. Binafsi sikuona mantiki ya Sioi kulazimishwa kugombea ilihali alikuwa hakubaliki. Na huo ndo ukweli. Si kila mtoto wa kigogo anaweza sisa jamani!
ReplyDeleteKidumu Chama Cha CHADEMAAAAAAA!!!
ReplyDeleteCHADEMA OYEEEEEEE!!!!, nabado tunakuja taratibu, 2015, asiye na mwana abebe jiwe,asie na jicho aweke la mbuzi, Dr Slaa au Zitto Kabwe lazima wachukue nchia habari ndio hiyo. Mdau mbeba box Uk.
ReplyDeleteCHADEMA JUUUUUUUUUUUUUU!!! nlisema! nilisema! Vidume 5 vya CHADEMA vimewashinda viongozi wooooote wa CCM walioenda ARUMERU? hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!
ReplyDeleteCCM muache Siasa za Ki uongo uongo na kuubeba Ufisadi !
ReplyDeleteAma sivyo baadae mtafikia kuambulia Kura '0' kama huyo Mgombea wa NCCR Mageuzi !
Mtambo umezama barabara !
ReplyDeletetena bila ganzi wala kutemea mate,
CHADEMA OYEEEEEEE !!!!!!!
Hongera Chadema! Michuzi na CCM yake Ziiiiiiiiiiii!
ReplyDeleteBig up wananchi wa Arumeru mashariki hamkuchagua chama mlichagua mtu atakayewawakilisha.
ReplyDeleteHaiwezekani mtu anaishi mbezi beach dar es salaam aje tuu kutaka uongozi kisa kaoa kwa lowasa eti apewe uongozi, huo ni utovu wa nidhamu.
Na hii serikali yetu ijifunze bila aibu viongozi mbalimbali wa chama walifunga safari eti kupiga kampeni, ZA NINI NA KWA LIPI MNAFIKIRI WATANZANIA HATUKO MACHO HUO UFISADI MNAOUFANYA JIONEENI AIBU TENA ABU KUMWA SANA KWA CHAMA TAWALA.
michizi usinibanie hii comment yangu najua wewe ni c c m damu
Pepoles power mpo juuuuuuuuu!!! hii inaonyesha jinsi gani wananchi wameichoka CCM.nina uhakika 2015 CDM inaingia white house. Hongera sana CHADEMA tupo nyuma yako.
ReplyDeleteMWISHO WA MAFISADI TANZANIA UMEKARIBIA!
ReplyDeleteAJABU NA KWELI. Yaani hata yeye mwenyewe japo ukisema na mkewe anaweza kuwa amemsaliti mumewe ila ya kwake itakuwaje. Pongezi kwa aliyeshinda then sasa tufanye kazi tuache malumbano ya hapa na pale kwa kuwa mtu akishinda sio wa chama tena bali ni wa watu wote
ReplyDeleteUNCLE HABARI YA SAA HIZI?NAKUSALIMIA TUU.
ReplyDeleteMabadiliko yanachukua mkondo wake taratibu.
ReplyDeletehana mke? hata mke au sijui katibu au mwenyekiti wake wa eneo hilo? au ofisini yupo mwenyewe?
ReplyDeletefunny
CCM tukusanye nguvu na ile mbinu yetu ya kuiba kura wataalam wako wapi? Mnajua tukikosa uongozi wa nchi chama kitakufa na ndo kinatuweka mjini?Cho nde chonde kama mbinu uwizi wa kura inagomba naomba tutafute mbinu mbadala. Degelavita.
ReplyDeleteNiliwaambia kwamba karibu tunafika pelekeni tu watoto shuleni hata kama hawapati kazi katika nchi yao wenyewe, faida yake ndo hii kwamba waelewa wazidi nasi tutafika salama katika mageuzi ya kisiasa na kiuchumi.amen.
ReplyDeletePolisi wanapopiga watu mabomu bila kosa itazidisha kuigharimu CCM. Kile walichokifanya Mbeya ni kitendo cha kusikitisha sana
ReplyDeletehuyo wa Chadema Mbwembwe tu hana lolote
ReplyDeleteLabda hakuwa na sifa za kupiga kura. Usishangae ni kitu cha kawaida Bongo, hata mgombea wa CCM hajapiga.
ReplyDeletewamegawanya ccm ilichukua jimbo la Igunga na wachadema wamechukua jimbo la Arumeru bado tena kivmbi cha 2015
ReplyDeleteHongera sana sana kaka
ReplyDeleteMakomredi vipi hamkupeleka mgombea?
ReplyDeletekwani huji wizi hata cheyo mwanza alisha wahi kuto kupata
ReplyDeletePeople's Power Bana! we acha bana!
ReplyDeleteSauti ya watu ni sauti ya Mungu nimeamini!
Kwa kweli leo hii nimejisikia ni Mtanzania halisi, na ukweli ushindi wa Nassari unaipatia CCM heshima kubwa sana katika kukuza demokrasia.
ReplyDeleteNina hakika kuwa kama chaguzi zetu zote zitaendeshwa hivi na matokeo kutangazwa bila mizengwe ni dhahiri kuwa Tanzania itaendelea kuwa nchi ya amani na utulivu na mshikamano. Tuienzi hii hali kwa kutenda haki.
Hongera Nassari chapa kazi sasa.
Ama kweli teja Chama Tawala habebeki!
ReplyDeletePamoja na Libeneke kuwa upande wa wakubwa lakini haikusaidia kitu, chaliii wamepiga mwereka !
Hakika CCM sasa wamekwisha!
ReplyDeleteThis is good - it's indictive that our people are finally waking up.
Siku zote nasema humu, waTanzania wa sasa siyo kama wa zamani zile za enzi za Nyerere na enzi za uhuru. Mtanzania wa sasa yuko 'aware'. Tumeamka na tumeshachoka 'kuburuzwa'!!
Thank Goodness!!
Buckinghamshire
Kampeni zingine na vigezo wala haviingii akilini.
ReplyDeleteOhhh Joshua Nassari hajaoa, hivi ni nani aliwaambia ya kuwa ktk Ndoa ndio kigezo cha uwezo wa Uongozi na Uadilifu?
1.Ni wanagapi walio ktk Ndoa lakini bado ni wazinzi?
2.Ni wangapi ktk Ndoa ambao ni wezi na si waadilifu?
3.Je ni wangapi walio ktk ndoa na ndio kwanza wanazisaliti Ndoa zao?
Michuzi wewe ni Noma, umegoma kuweka comments kisa CCM imepigwa chini. Kweli globu ya jamii ina itikadi kali
ReplyDeleteHongera sana Chadema. Ushauri kwa CCM: Muache utawala wa mabavu, kutetea ufisadi na ubinafsi. Mfuate maadili kama jina la chama chenu linavyoiitwa, Chama Cha mapinduzi kwa wananchi. Kauli mbiu ya maisha bora kwa kila Mtanzania iwe ya kweli kwa kila mtu na sio kwa wachache.
ReplyDeletePamoja na utu uzima wangu, leo hii nimetokwa na machozi, na wala sikumbuki mara ya mwisho nililia lini.
ReplyDeleteChadema, mbarikiwe sana. Tuna imani na ninyi.
Ahsante Mjomba Michuzi kweli Siasa unaiweza na umekomaa kama Kada wa CCM !
ReplyDeleteNimefurahi sana kuona maoni yangu yote ya 'Mabunduki' dhidi ya chama chako umeyaanika hewani !
KUANGUKA KTK UCHAGUZI, NDIO ITASAIDIA MJIPANGE NA MJIREKEBISHE.
HAIWEZEKANI ANKAL KILA UCHAGUZI UNASHINDA WEWE TU, KAMA VILE SISI WENGINE NA VYAMA VYETU NI MAITI !
LAZIMA UKUBALI MATOKEO NA PIA UHUDHURIE MBUNGE AKIAPISHWA NA RAISI !
HUO NDIO UKUBWA ANKAL NA UKOMAVU WA KISIASA !
Zama za SIASA za MABAVU na UJAMBAZI ZIMEKWISHAAAAA !
ReplyDeleteUENEZI WA SIASA ZA KIUSANII UMEZIKWA KABURINI ARUMERU MASHARIKI JANA !
CHADEMA nyinyi ni watu wa mungu sna mana wte viongozi wenu ni wazuri sna kwa kuongea tu munajua
ReplyDeleteCHADEMA amka sasa;mbinu mpya ya PEOPLES'POWER imejibu.Ni kuanzia leo mrekebishe vitatizo ndani ya chama kabla havijaota mapembe. hapo sie waTZ wengi tutajiunga na Chama hiki chenye kutuonesha matumaini.
ReplyDeleteCCM mjipange upya,muache kuukumbatia ufisadi, muache siasa za kujuana za kupendelea watoto wa vigogo, siasa za uongo wa kujenga barabara wakati si kweli. Sioy hakuwa mmwanasiasa bali aliwekwa kwa kuwa ni mkwe wa fisadi na waliogopa kumuengua kwa vile fisadi angekuja juu. Wale walioachwa katika kura za maoni ndio wangefaa kuitete CCM.
ReplyDelete