Mimi ni mdada wa kitz naish hapa dar,ni mfatiliaji mzri wa habar kwa blogs mbalimbali kwakweli nakupongeza kwa jins unavyoendesha blog yako.Lengo la email hii ni kukuomba uwashaur bloggers weeengi waloibuka wasojua hata maadili jamani ni meng wanakosea hasa kwa picha za mtu ambae ashafariki ila alilofanya mwigizaji Ray kwa blog yake leo ndo kimenisukuma kukuandkia email hii ,jana tumempumzisha mpendwa wetu Kanumba leo yeye anaupload picha za mwili wa marehemu siku ya tukio akiwa ndani ya gar na maelezo kibao tu halaf mbaya zaid akafafanua kuwa hii hapa ni muda mchache baada ya kufariki nk kama walijua kafariki kwann hawakumfunika?wakawa bize kumpiga picha matokeo yake zimevuja kwa magazeti ya udaku wanaziweka front page kwakweli mimi binafs wameniudhi sana hao wasanii wenzie walompeleka mochwar maana ndo wamezivujisha hizo picha sasa nae kaja kuzianika kama alitaka kuweka picha kwanini asiweke za jana mazishi?Plz ankal sema na wadogo zako sasa wanaboa jamn ndo mana jana walikurupuka wakatuwekea picha za kabri ambalo sio la Kanumba wakasema ni la kwake.Nakutakia kazi njema
Mdau Kurasini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. nakuunga mkono kabisa mdau...mimi pia nashangaa sana hizi picha za marehemu Kanumba zimekua kama ni dili kwa watu wengine..watu wanazianika picha utafikiri ni fahari fulani..Jaman tuheshimu hizi picha..sio vizuri kabisa kuzianika kama watu wanaona ni fahari...
    Tumuenzi Kanumba kwa sanaa aliotuachia bali si kwa kuzitupatupa hizi picha humu mitandaoni..

    Kuna picha nzuri sana za Kanumba enzi za uhai wake..kwa nini msiziweke hizo jamani???

    Kwa sisi ambao tayari tumeshafiwa na watu ambao tuliwapenda sana tunajua athari ya kuweka picha za marehemu hadharani...

    Aksanten wanalibeneke.

    ReplyDelete
  2. Mimi naungana na huyu mdau manake nilishangazwa sana kuona mablogs wanatoa picha za mtu aliyetutoka manake hata hawakuwa na heshima ya familia yake mi niliandika msg kwa mmoja wao kuwa pls toa sio vizuri ila naona akanidharau.

    ndio maana huwa nasema mablogs yawe ya watu wasomi tu sio hawa wanaotaka tu kufungua kitu ilimradi tu wapate chochote.

    RIP S kanumba

    ReplyDelete
  3. Mbona sijaziona hizo picha za kanumba?

    ReplyDelete
  4. YAANI NAKUPONGEZA SANA ULIYETOA HII HABARI,KILICHONISHANGAZA NI SIKU ILE AMBAYO KANUMBA ALIKUWA ANAPELEKWA HOSPITAL YANI RAY ALIKAZANA SANA KUPIGA PICHA JAMANI RAY MUOGOPE MUNGU NA WALA USIDHANI KAMA UNAWEZA KUWA KAMA KANUMBA.KANUMBA YA KWAKE YAMEKWISHA YA KWAKO BADO.

    ReplyDelete
  5. Nami hili naomba niongezee.

    Nlisikitishwa nlipoona kwenye TBC wakati mwili wa marehem unatolewa nyumbani kwake kuwekwa kwenye gari, nakutolewa kwenye gari kuingizwa muhimbili.

    Ray alikua busy na simu yake akipiga picha. Hii si taswira nzuri. Hata kama mtu huyo hamkua na mahusiano mazuri naye ni bora kutofika kabisa kuliko kufika na kutoonesha kujali!

    Mbona JB, Rich na wengineo walionesha wazi kuguswa na msiba huo. kwani wao hawakua na simu zenye camera?

    Kama hiyo haitoshi, picha hizo unaenda kuziweka kwenye blog yako! Seriously! Naona picha hizo kaziondoa kwenye blog lake. Labda kapata washauri.

    RIP Kanumba

    ReplyDelete
  6. Well said mdau, na haya magazeti pia hayana maadili, kama hiyo blog imetoa picha why should magazetiz be a copy cat??? hawawezi kufikiria kuwa walichofanya wenzetu sio kizuri so na sisi tusikifanye/tusikiige??
    After all blog inaweza ikaondoa hiyo post, what abt gazeti?? lita-reverse vipi hiyo article??

    ReplyDelete
  7. Mimi sina hamu na uandishi wa hapa kwetu tangu nilipoona mwili wa marehemu Hija(RIP) ktk gazeti ukionyeshwa picha step by step tangu anashuka ktk gari la polisi, anarushiwa jiwe la kwanza, anarushiwa la pili, la tatu, la nne, mpaka umauti ukamkumba. Sina hamu kabisa. Dont they really think about ndi=ugu za marehemu watakaoona hizo picha za kutisha na kuhuzunisha???

    ReplyDelete
  8. Naomba na mimi nichanagie kwa hili. Kwa kweli inasikitisha sana watu wanashindwa kuheshimu mwili wa marehemu. Maadili yako wapi? Je fahari kweli kuonyesha mwili wa marehemu ukiwa haujafunikwa??? Kwanza huyo Ray ni mnafiki mkubwa na yeye ndiye aliyevujisha picha hizo kwa magazeti ya udaku. Na mbona tangu siku ya kwanza huyo Ray hakuweka taarifa yoyote kuhusiana na kifo cha Kanumba kwenye blog yake??? Picha zote alizotokea anaonekana anacheka cheka tu!!!! Pls vitu vingine havihitaji elimu kubwa kuvielewa. Badilika ww Ray. Umeboa sana.

    ReplyDelete
  9. Hawa wengine ndo marehemu aliwaimba kuwa hata maadui zangu watabeba jeneza langu nikifa, mlikuwa na mabifu kibao leo ghafla unampenda sana, shame on you

    ReplyDelete
  10. sasa kama hamtaki hizo picha mbona kwenye kuaga mnamuangalia?

    ReplyDelete
  11. Problem ni western culture! turudi kwenye jadi zetu.

    ReplyDelete
  12. Ni kweli jamani siyo vizuri kuweka picha za marehemu siyo kwa ray tu hata wanaoweka picha hizi kwenye face book kwa upande wangu nawashangaa sana kwa nini wasiweke picha ambazo alikuwa hai jamani.mbona picha zake ni nyingi sana.tumuenzi kwa mazuri yote aliyotuachia.DAIMA TUTAKUKUMBUKA MPENDWA WETU KANUMBA.

    ReplyDelete
  13. EDUCATION IS SEX

    ReplyDelete
  14. Nakuunga mkono mdau, kwanza cha kushangaza, yaani kweli mtu unayempenda kafa kifo cha ghafla ka ma cha Kanumba utaweza kweli kuwa na nguvu za hata kupiga picha? na hawajui hata maadili na heshima ya maiti, kwa kweli jifunzeni nyie na watu wazima sana, mtu akishasemekana amefariki, ni muhimu sana kumfunika

    ReplyDelete
  15. Kwa upande wangu nadhani kuna watu ambao kwa chuki zao binafsi walifurahia kifo cha Kanumba. Niliangalia TBC kwa kweli ujinga wa RAY niliouona sikufurahishwa kabisa. Wakati kina JB, RICH na wengineo wanahangaika kumtoa Kanumba ndani ya gari , RAY yeye alikuwa busy kupiga picha bila masikitiko kabisa.
    Ray naomba ukumbuke, utu wa mtu unapimwa kwa vitendo vyake. kwa ujumla hujatufurahisha kabisa kwa vitendo vyako kwenye msiba wa Kanumba.

    ReplyDelete
  16. Shida yako dada uliyetuma picha kwa kaka Ankal sio picha. Tatizo lako una chuki moyoni mwako iliyokubuhu. Ukijichunguza utaona sababu ya kutoandika ulichokiandika. Ray hana tatizo lolote. Shida ni wewe. Jifunzeni kuwa na upendo wa dhati.

    Watanzania tujifunze kupendana. Tusiwe ni watu wa chuki kila saa.

    Ninatamani kuona tunaongeleana kwa mazuri na si mabaya. This is my prayer - one day we see one another as brothers and sisters

    ReplyDelete
  17. Hili jambo lilinisikitisha sana na bado wanaendelea blogs zingine zimeweka barua aliyoandika baba mzazi, kwanini hii barua ilivujishwa jamani hakuna privacy? hii familia imeanikwa mpaka basi yani si jambo jema kabisa.

    ReplyDelete
  18. so sad kwa kweli...!

    ReplyDelete
  19. Mdau, nikupongeze kwa muda wako wa kuandika maoni yako, naona tu maneno ya kujisifu yeye na mama yake. The greatest lakini ukimbana vizuri hajui hata maana ya the greatest. Kanumba sikujua sana kama alikuwa maarufu sana na nimeona juzi--hii imetokana na kazi kubwa ya ubunifu aliyoifanya. tuache kuiga, tuwe creative. Mwenzaki anaitwa the great wewe unajiita the greatest?? niwaachie wenyewe--michuzi saidia kwa kuwaelimisha

    ReplyDelete
  20. hiyo blog ya ray inaitwaje?? tumpe ushauri

    ReplyDelete
  21. nimeangali naona Ray ameshazitoa.

    ReplyDelete
  22. Ni blog gani hiyo? naomba nipe link please.

    ReplyDelete
  23. NAONA AMESHAZITOA PICHA,YANI KUMBE KILE KITENDO ALICHOFANYA CHA KUMPIGA PICHA KANUMBA WATU WENGI WALIKINOTE.BLOG YAKE NI RAY THE GRETEST.YANI AMEONGEZA EST KWA GREAT KANUMBA.RIP KANUMBA.

    ReplyDelete
  24. kulikuwa na kuna kila baraka za kuitwa Kanumba "THE GREAT", ila sasa leo naona kuna RAY "The greatest" naona kama kichefuchefu!

    ReplyDelete
  25. kweli ankali Knumba kakuuma hadi umeacha Ray tumpe live na ni si kawaida yako huwa unabana sana mtu akipewa live na kutajwa jina...R.I.P. my home boy..

    ReplyDelete
  26. kwakweli na mimi nilipoona na barua ya baba yake imekuwa published I was shocked na kujiuliza ni sababu hatujui sheria ndio maana familia za hali ya chini zinafanyiwa haya yote ama ni kutukujuwa kwa wale bloggers wanaopost hiyo barua?

    ReplyDelete
  27. kwenye kuaga alikuwa amevalishwa vizuri kwa lengo la kuaga.

    na huyo Ray picha zote kwenye msiba ka-smile tuuu. hata akijiita the greatest hawezi kumfikia my Kanumba. He had a natural talent

    ReplyDelete
  28. UKUBWA NI JALALA:

    Ankal nimewahi kusikia kuwa mna Umoja na Chama cha Bloggers,

    Sasa kwa nini msifanye Mpango mkaandaa Kozi fupi za kuwaeleimisha Wanafani hasa wanaochipukia kuhusu taratibu na Kanuni?

    Wewe ukiwa ni miongoni mwa wakubwa wa fani hii (Wakongwe) si ndio Mzigo wako sasa?

    Kwa sababu hali hii ikiachiwa inaweza kuleta madhara makubwa kutoka ktk Mamlaka za Kitaifa dhidi ya Libeneke halafu tukakosa raha bureee.

    Au sio?

    ReplyDelete
  29. hawa wameibuka tu na blog, sidahani kama wanafahamu maswala ya utu, kwanza Kanumba hakupenda mambo yake yawe wazi kwa jamii msifikiri kwasababu kafariki ndo katoa loophole ya kuanika maisha yake hata alipo sasa hivi hapendi. Ray wewe ni muigizaji next time hata kama issue haijakugusa onyesha uso wa simanzi kama uko location vile, kuliko kuwa na sura kavu kama ulivyofanya kwa swaiba wako. Mimi namfahamu Kanumba kupitia movi lakini nimeumia kama mdogo wangu vile nimelia na bado namlilia wewe uso mkavu kabisa bwana. Leo ndo unajifanya sijui mama ako alienda airpot kumpokea mama Kanumba acha kujikweza wewe mama ako ungemwonyesha toka huko nyuma na kwa sasa usingekuwa na haja ya kuanza kumwonyesha eti aliyevaa nguo nyeupe.
    Zaidi nashukuru umetoa hizo picha maana sometimes unakichwa kigumu sana wewe.

    ReplyDelete
  30. judy canadaApril 12, 2012

    Jamani tujifunze kutokana na makosa na tujifunze kusamehe pia.Kweli ni kosa kuonyesha ule mwili bila kufunikwa lakini najiuliza kitu kwamba hata ukiwa ndani ya jeneza watu walitaka kuuona pia. Tuwe washauri na si wahukumu nani alijua kama kanumba alishapatana na baba yake?? Na sioni sababu ya kumhukumu huyo ray ni kumshauri sasa kama kuna watu walikuwa wamebeba mwili na nafasi ya kushika hamna mlitaka huyo ray ashike sehemu gani?Tusiwe wahukumu na sisi tutahukumiwa tuwe washauri na wasamehevu.

    ReplyDelete
  31. Jamani mwacheni Kanumba apumzike kwa amani tumfikirie huyu binti mdogo aliyeko huko mahabusu. Kama mzazi naumia sana. Tumuombee matatizo yampitie mbali na Mungu amtie nguvu. Hawa waigizaji wanaigiza hata mahali ambapo sio pa kuigiza (Ray) Msameheni bure hajui atendalo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...