MC Mchekeshaji Evans Bukuku akitoa neno wakati wa uzinduzi mbele ya maDJ wa Heineken |
Kilaji cha kimataifa cha Heineken kimefanya uzinduzi wa "Heineken Champions Planet" itakayo wapa wateja wake nafasi ya kuangalia mashindano kabambe ya Ligi ya UEFA msimu wa 2011/2012.
Uzinduzi wa “Heineken Champions Planet” unatokana na mafanikio makubwa ya matembezi ya kombe la Ligi ya UEFA ulio dhaminiwa na Heineken hapa nchini Tanzania na Kenya kutoka Machi 23 hadi Machi 31. Katika kipindi hiki, kombe la UEFA lilikuwa nchini Tanzania kwa siku tatu, ambapo walaji wengi wa Heineken pamoja na wadau wa soka waliungana pamoja kushabikia kombe hili la kifahari.
Ligi ya mabingwa ilianzishwa na UEFA mwaka wa 1992, na inadaiwa na wengi kama mashindano bora katika ulimwengu wa soka. Heineken imekuwa ikihusika na mashindano hayo kama mfadhili rasmi tangu msimu wa 2005/2006. Leo hii inaendelea kuwa mfadhili mkuu wa mashindano haya hadi msimu wa 2014/2015.
“Heineken Champions Planet” ni bonge moja la nyumba mtaa wa Oyster bay, usoni pa Jackies Pub yenye sebule kubwa, na runinga katika eneo kuu la kutizamia. Vilevile “Heineken Champions Planet” ina vyumba vingine vya michezo mbali mbali vilivyoezekwa PS3, meza za foosball, pool tables na chumba mahususi kwa wanahabari yaani Media centre.
Maandalizi haya yote ni kwa ajili ya kuwaburudisha washindi mbali mbali wa Heineken katika kuwapa kumbukumbu la maisha.
Maandalizi haya yote ni kwa ajili ya kuwaburudisha washindi mbali mbali wa Heineken katika kuwapa kumbukumbu la maisha.
Meneja mkuu wa masoko Afrika mashariki, Bwana Krijin Jansen alisema wakati wa juzinduzi “ Kama mshiriki wa muda mrefu wa Ligi ya Mabingwa la UEFA, Heineken inaelewa kuwa msisimko uliopo katika mashindano haya unahitaji mambo mbali mbali ya kuwachangamsha wateja wao.
Kwa ushirikiano mkubwa waliotuonyesha “Heineken Champions Planet” imetekeleza miundo mbinu hii ya kipekee ili kuwaigiza mashabiki wake kwa njia thamani.
Kwa ushirikiano mkubwa waliotuonyesha “Heineken Champions Planet” imetekeleza miundo mbinu hii ya kipekee ili kuwaigiza mashabiki wake kwa njia thamani.
Kutokana na umaarufu wa Heineken kote duniani, kilaji hiki kimeona kuwa wadau wake wanahitaji sehemu maalumu kwa ajili ya kuangalia na kushangilia ligi ya Mabingwa la UEFA msimu wa 2011/12 hadi mwishoni 19 Mei katika “Heineken Champions Planet”.
Mdau wakipigwa na kreti zima zima siku ya uzinduzi
Michezo kibao
Big Screen kila kona na hazina chenga wala mikwaluzo. Dah! Heineken bwana!! Taswira hizi zimedakwa na Steve Annu, mpiga picha mpya wa Globu ya Jamii. Kwa mapicha zaidi BOFYA HAPA
kilaji chetu hicho wadau wa udachini ndani ya uholanzi kilaji laini.
ReplyDelete