Mandhari ya kuvutia sana itaonekana leo na kesho katika anga ya magharibi saa moja jioni, baada ya machweo.  Tutaona hilali mbili – ile ya Mwezi, tuliozoea, pamoja na ile ya Zuhura ukiiangalia katika darubini.

Siku ya Jumanne tarehe 24 Aprili Mwezi hilali itaonekana kiasi cha nyuzi 30 juu ya upeo wa magharibi  chini ya sayari ya Zuhura inayon’gaa kama taa kali.  Tarehe 25, Jumatano Mwezi hiliali itaonekana juu ya sayari Zuhura.

Picha ya hali itakavyokuwa siku hizo mbili imetengenezwa kwa kutumia programu ya Stellarium abayo inapatikana bure katika mtandao.

Dr N T Jiwaji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Inavutia mno,Jana niliitwa nitoke nje ili nishuhudie Nyota ilivyokuwa ikiwaka,nilivyotoka basi ndo nikakuta Mwezi ndo unazama kidogo kidogo,lakini nyota ya Zuhura ilikuwa ikiwaka mpaka raha!

    Mwenyezi Mungu ni mkubwa sana!!!
    Yaani huwezi amini kama hivyo vitu viko mbali namna hiyo na vimetengana sana!

    Ahlam !!!London!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...