Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,akiweka Shada la mauwa katika kaburi la Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume leo viwanja vya CCM Kisiwandui mjini Unguja.
Viongozi wa Kitaifa wakimuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,katika kaburi alipozikwa kiongozi huyo huko Viwanja vya CCM KIsiwandui Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati) Rais wa mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,(wa pili kushoto) akimuakilisha, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji,na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Qaabi,pamoja na viongozi wengine wakisoma hitma ya kumuombea dua Muasisi wa Mapinduzi,na Rais wa Kwanza wa Zanzibar Abeid Amani Karume,Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Mabalozi na Wananchi waliohudhuria katika kisomo cha dua ya kumuombea marehemu Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,huko Ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo.
Mke wa Muasisi wa Mapinduzi na Rais wa kwanza wa Zanzibar,Mama Fatma Karume,(wa nne kushoto) pamoja na wake wa Viongozi mbali mbali wakiwa katika hitma ya kumuombea dua Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,huko Ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo.
Baadhi ya Akina mama wa Mitaa mbali mbali ya Unguja,wakimuombea Dua marehemu Mzee Abeid Amani Karume,huko Ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo.
Mke wa Muasisi wa Mapinduzi na Rais wa kwanza wa Zanzibar,Mama Fatma Karume,(kushoto) pamoja na wake wa Viongozi mbali mbali, wakiomba dua katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,huko viwanja vya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Duh!! Maalim Seif kayatambua Mapinduzi?!! Nasubiri Ismail Jussa naye ayatambue. Mapinduzi Daima!! Muungano Udumuuuuu!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...