Hawa ni vijana wa Jamii ya Kimasai ambapo kamera man wa Globu ya Jamii alibahatika kukutana nao huko maeneo ya Makuyuni,Mkoni Arusha.hivyo alilazimika kupata taswira zao na kutuletea hapa.Je,kuna kwenye data zozote juu ya  vijana hawa kuwa katika hali hii???kama yupo tunaomba atumwagia hapa libenekeni.maana tushazoea kuwaona watu wa jamii hii wakiwa katika mavazi yao ya aina tofauti na haya.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. Safi hiyo, kwa ufahamu wangu mdogo hawa ni morani ndo wametoka jandoni.. au bado wako jandoni. Watavaa hivi na kulala nje ya nyumba zao kwa miezi kadhaa.

    Mdau

    ReplyDelete
  2. MIE PIA NAOMBA KUULIZA? JE HAWA MAVAZI YAO NA RANGI ZAO ZA USO CBE WANAKUBALI? Najuwa mtu nikipiga hivyo mtasema oh kadata JE HAYO PIA YA HESHIMA? NA JE VIONGOZI WAACHE TAI NA SUTI KAMA ILIVYO HAWAVAI KANZU WAANZE KUVAA MAVAZI HAYO? JE RAISI KUVAA SUTI NA TAI SHERIA YA AFRIKA(TANZANIA) AU BRITISH LAW?

    ReplyDelete
  3. mhh hao watakuwa wamasai pori

    ReplyDelete
  4. Mwanalibeneke mtoa taswira, swali lako haliko wazi. Kama unahitaji kufamu data za hao vijana uliowapiga picha, nafikiri ulikuwa na wakati mzuri wa kuwauliza ulipokutana nao na pengine uka-share na sisi nini umejifunza. Kama unahitaji data za vijana wa kimasai ambao siyo lazima wawe hao ila wenye outfit ya aina hiyo basi kuuliza hadharani ni sahihi.Lakini mkuu data zinakuwa kwa mfumo wa numeric au statistics. Ni namba zipi hasa unazohitaji?

    ReplyDelete
  5. hawa wanaitwa ``skolio`` wametoka jando siku za karibuni hivyo wapo katika transition ya kuingia katika rika la morani. Wale wanaovaa nguo nyekundu ndio morani. Vile vile hiki ni kipindi chao cha mafunzo kuhakikisha kua wameiva kikamilifu katika kuitumikia jamii na pia utayari wa kuchukua majukumu km familia n.k, mwisho wa stage hii huwa wanafanyiwa sherehe na baada ya gapo hawavai tena hizi kaniki, wanavaa zile nguo nyekundu. kwa kawaida tohara hufanyika kwa miaka 7, then inaahirishwa kwa miaka 7, sasa huu ndio mwaka wa kwanza tangu rika jipya limeanza kutahiriwa so mtarajie kuendelea kuwaona vijana kama hawa mpk miaka 7 itakapoisha.
    tchao,

    ReplyDelete
  6. Hahaha,
    Hawa ni Masokolio Bro Misupu.Ni makabila ya Kimeru,Kiarusha na labda wamasai ila sidhani kama wamasai watakaa barabarani wakiwa masokolio.Masokolio ni Vijana walio toka kutairiwa soon wanapo pona ndio wanatembea tembea vichakani na mavichoni kama hivi.Ni mila na desturi zao.Ni wadau wengi tu watakuwa wamepitia level hii.Duh bado wana mila hizi?.Kweli we need #ChangeTZ

    ReplyDelete
  7. Hao wako kwenye mafunzo ya kuingia utu uzima, kuna ngazi mbalimbali ya mfunzo, likiwemo lile la kumuua simba peke yake kwa kutumia mishale na ngao, hiyo ni ngazi ya juu kabisa, sasa hawa wako kwenye intermidiate category yaani ngazi ya kati, mara nyingi ukiwaona katika hali hii, na kunamichoro usoni yenye kumaanisha kitu fulani katika ngazi husika, kwa hawa hapo wako kwenye jando na theory zake.

    ReplyDelete
  8. I am curious to know as well,...Inaonekana sio waarusha.
    (http://hadithiutamaduni.blogspot.ca/)share your story

    ReplyDelete
  9. Hawa SIO wamasai wanaitwa Wabaragaig

    ReplyDelete
  10. hii ni style yao mpya ya kutafuta hela huko ngorongoro, maana watalii huwa wakipita wanasimama wanapiga nao picha halafu wanawapa hela, ni ubunifu tu!

    ReplyDelete
  11. ndiyo wametoka jando,baada ya muda mfupi watabadili jezi na kuvaa nyekundu ambapo ndio umorani wenyewe

    ReplyDelete
  12. Wametoka kutahiriwa hao, home tunawaita layoni. Baada ya hapo ndio unakuwa Morani na mwishowe ukibahatika unakuwa Laigwanani.

    ReplyDelete
  13. hao ndo wametoka kwenye jando

    ReplyDelete
  14. wametoka jando

    ReplyDelete
  15. Wamasai Wadau kazi kwenu tupeni kwa Uchache hapa Jamvini kuhusu hao jamaa !

    ReplyDelete
  16. Makomandoo wa Kimasai ndio hawa,

    Yaani Askari wa Kikosi Maalum cha Vita au Mashujaa wa Vita wa kukabiliana na hali ngumu ktk Vita au kwa suala la Kumsaka mnyama Mkali kama Simba.

    ReplyDelete
  17. Hao ni Wamadeege, Mashujaa wa Kimasai wa Vita.

    ReplyDelete
  18. majibu yote yaliyotolewa sio ya uhakika. Jee wamasai wenyewe mpo, tupeni data za uhakika sio porojo. Hii glob ni ya kuelimishana. Na wewe mdau unaesema tunahitaji kubadilika, mbona wascottish wanavaa sketi ndio vazi lao la kitaifa. Waafrika mavazi mnayoyavaa sio hata utamaduni wa kizungu. Kila kitu ulaya ni udictator wa kibiashara.

    ReplyDelete
  19. Hivi ni kwa nini kila mtu anajibu, wakati wengine hawajui hata hilo jibu. Wabongo mtu akiuliza ajibiwe, ukiwa hujui usiandike kitu.Soma na uondoke. Mfano, ukiandika nadhani, nafikiria maana yake huna uhakika kwahiyo unabahatisha.Mda ni mali, kama huna uhakika usiandike.mawazo yangu hayo.Tuko hapa kuelimishina, na kupeana habari muhimu. Ndio maana ni mpenzi wa blog kwa muda.Hongera kaka Michuzi.Mdau nje ya nchi.

    ReplyDelete
  20. Majibu yote moja tu ndio sahihi, kwamba hawa ni wasanii tu, wanabangaiza vijisenti toka kwa watalii, hawana lolote, njaa tupu. Spolion tunawajua hawazururi barabarani, wanakaa porini kujifunza maisha.

    ReplyDelete
  21. MDAU WA KWANZA KABISA, YOU ARE RIGHT. HAWA NI MORANI AMBAO WAKO JANDONI. HAWATAONDOA HAYO MAJIVU MPAKA WAMALIZE KIPINDI CHA JANDO. KATIKA KIPINDI HICHO, MORANI HAWA WANATARAJIWA KUJITEGEMEA KWA KILA KITU: MAJI, CHAKULA, N.K. KIKUBWA ZAIDI, WAKATI MORANI HAWA "WAKIPIGWA KISU" HAWATAKIWI KUONYESHA WOGA NA HAWATAKIWI KUONYESHA KUWA WANASIKIA MAUMIVU. KATIKA TEMBEA YANGU TANZANIA BARA NA VISIWANI, NIMETOKEA KUWAHESHIMU SANA WAMASAI NA WASHIRAZI KWA KUTHAMINI MILA NA DESTURI ZAO. WAHENGA WETU WAMESEMA "MDHARAU ASILI NI MTUMWA". VERY TRUE. MDAU WENU J. MOSHA WA NJIRO ARUSHA.

    ReplyDelete
  22. Mimi ni mmasai. Naomna nitoe ufafanuzi juu ya hili. Hawa ni vijana wa kikamai wakioko jandoni, wametoka kutahiriwa hivi karibubi na bado wako jandoni kimafunzo. Wanavaa mavazi hayo ili kutofautiana na wengine ili unapokutana nao ujue kabisa wako jandoni. Siku wakimaliza muda wao jandoni wanatolewa kwa sherehe kubwa sana na sometime wanapewa zawadi kuwapongeza kwakuwa wamekuwa watu wazima wanaoweza kutegemewa na jamii. Pia wakitoka hapo wanaweza sasa kuoa kwani b4 hawatakiwi kuwa na mwanamke kama hujatahiriwa. Hayo mavazi ni special kwaajili ya vijana walioko jandoni, huwezi kuta mmasai kavaa hizo nguo nyeusi kama hayuko jandoni. au kupaka hizo rangi uzoni. NAWASILISHA

    ReplyDelete
  23. Niliwahi kukutana na vijana hao na niliuliza wenyeji niliokuwa nao. Jibu ni kwamba vijana hao wametoka Jando na wanatakiwa kukaa porini kujifunza maisha ya kujitegemea. chakula chao wanatakiwa kuwinda wenyewe na pia wanatakiwa kujifunza ukakamavu. lakini hawa wa sasa wamegundua njia mbadala. kwa kukaa barabarani watalii wapita njia wanawapiga picha kwa malipo. Zamani hatukuwahi kuwaona kwa kuwa walifanya vile ilivyotarajiwa.

    ReplyDelete
  24. HAO SIO WAMASAI KWA TAARIFA ZENU HAO WANAITWA WAMANGATI HAO JAMAA NI NOMA SANA YANI WAKOROFI KUSHINDA WAMASAI NA VITA YAO NI MBAYA SANA MARA NYINGI WANAGOMBANA NA WAMASAI KWA KESI ZA MIFUGO

    HAO WAMANGATI MARA NYINGI SANA WANAKUWA WANAANZISHA VITA NA WAMASAI WAO HUANZA KWA KUWAIBIA WAMASAI NGOMBE AU KUGOMBANIA MAENEO YA KUISHI
    WAMANGATI WAPO WENGI MAENEO YA WAME DAKAWA NJIA YA KUTOKA MOROGORO KUELEKEA DODOMA WAPO PALE KATI PANAITWA DAKAWA

    WAMANGATI WANA SIFA YA KURUSHA VIZURI SANA MISHALE YAO NA ANAWEZA KURUSHA JUU UKIJA KUANGUKA CHINI KATIKATI YA KUNDI LA WAMASAI NA KUJERUHI AU KUUWA WAMASAI.

    ReplyDelete
  25. Hawa ni vijana wa kimaasai, waliotoka kutahiriwa hivi karibuni(ndio wamepona kiasi flani -sio full kupona).Kwa jina wanaitwa ISIKOLIO.Kumbuka kuwa sisi wamaasai tuna stages mbalimbali za kimaisha.Vijana hutahiriwa wakiwa na umri mkubwa(tofauti na makabila mengine wanaotahiri hospitalini).Soon baada ya tohara wanaitwa ISIKOLIO.Hawa huvaa kaniki(kama wanavyoonekana pichani),huchora uso kwa chokaa(Lime stones), huwa na mishale isiyo ncha kali.Hawa mara nyingi hawalazimishwi kufanya kazi yeyote(labda mtu aamie kwa utashi wake), huzurura sana.Hii ni stage ya mafunzo(shule) ya kuelewa jamii, na kujiandaa kuingia stage ya MORAN.

    Moran huvaa nguo nyekundu.Wana majukumu makubwa ya ulinzi wa jamii, mifugo, na kutafuta malisho ya mifugo has nyakati za ukame.Wakati wa ukame moran huhamisha ng'ombe kufuata sehemu zenye malisho na maji ya kutosha, na hukaa huko mpaka mvua inkinyesha ndi hurudisha nyumbani.Sehemu wanazohamishia ng'ombe nyakati za ukame huitwa RONJO.Kumbuka ISIKOLIO hawaendi RONJO, ni MORAN pekee ndio huenda ronjo.

    Tohara hufungwa kwa miaka saba.Kwa miaka saba hii hakuna atakayetahiriwa, na ikitokea mtu kamtahiri kijana(LAYONI) wake ktk kipindi hichi, basi atapewa adjabu kali sana.(sitazungumzia adhabu za kimaasai leo).

    Baada ya miaka saba tohara hufunguliwa kwa miaka saba, kabla ya kufungwa tena kwa miaka saba.Mzunguko huu wa miaka saba saba umedumu toka enzi na enzi. Hakuna mabadiliko.

    Watu walotahiriwa ktk miaka saba(seven yrs period) huwa ni kama generation moja na hupewa jina lao.Ndio maana utasikia kuna ILTALA,ILTERITO,ILNYAGUSI,ILMAKAA(ILTOIPO), ILANDIIS, ILKORIANGA(Ilkorianga ndio newst).

    ReplyDelete
  26. Hao wamefanyiwa tohara wanatoka kwenye ulaiyoni kuwa morani

    ReplyDelete
  27. MDAU MMOJA KAMJIBU MLETA DATA JIBU ZURI ANGEWAULIZA TU WAO KAMA ALIWAPIGA PICHA MIE NAONA KAWAOGOPA HAKUJIAMINI... MDAU MWENGINE KAJIBU UKWELI ULAYA MAGAIDI WA BISHARA TU, TIZAMA USA MA AMISH WANAVAA KIMILA NA HAWAWAINGILII SABABU WATU WAO UKIENDA UTAH WANAOWA NA KUWEKA NDANI WAKE ZAIDI YA 5 ILA WAO KWAO SAWA KWA NCHI ZA WENGINE SIO SAWA WANAWAIBA WATU AKILI KWA MATANGAZO YAO NJE X-MAss IMEWEKWA KWA MAUZO YA RETAIL IKIFIKA MWAKA MADUKA YAMEINGIZA PESA ZA MAVAZI, WAACHENI WENZENU WAENDELEE NA MILA ZAO. A

    ReplyDelete
  28. Mimi nimefanya kazi na jamii ya wamasai kwa muda mrefu, ni kweli hao ni vijana wa kimasai ambao bado wako porini/jandoni na huvaa hivyo mpaka watakapofanyiwa sherehe na kuwa morani. Na hizo nguo zao nyeusi za jandoni zinaheshimiwa sana kwenye jamii yao. Utakuta hawawezi kuleta nyama kwenye kundi hadi nguo nyeusi wanazovaa wanawake ndani ziwe zimefunikwa vizuri na mavazi ya nje haionekani hata upinde wake ama sivyo hapaliki. Na makabila mengine pia vijana wakiwa jandoni wanapaka rangi kwenye miili yao na usoni mfano wagogo, warangi ili kuonyesha kuwa vijana wako jandoni. Ila kipindi hicho wanaruhusiwa kutembea na hizo mask washapona vidonda zamani. Kimila mwanamke ukiwaona unakimbia au unajificha.

    ReplyDelete
  29. Mbona tunasikia wamasai HAWATAHIRIWI jamani acheni kutuzuga hapa? labda mseme wanatayarishwa kukamata simba na mshale na ngao nitaamini lakini jando mh ! mh ! hakuna hiyo !

    ReplyDelete
  30. Mdau Unasikitisha na wewe Ushasema ni "MAWAZO YAKO HAYO" kwahiyo kila mtu anayo mawazo yake wacha wenzako watoe mawazo yao japo wanabahatisha sawa na kumpotoza mtu ila wamejaribu kwenye fikra zao. Mie Maoni yangu Tanzania watu wa Media tungekuwa tunatafuta watu kama hawa Kuonyesha Documentary zao nchi watu wajue Wa-Tanzania wenzao wanavyoishi na Mila zao wapate Elimu kwao mazuri wabebe na mabaya waache japo mabaya mengine kwao mazuri, Wao pia Wapewe Elimu ambayo itawasaidia ambayo watapenda kuyachukua na wasiyoyapenda kwa sababu za Mila zao waziwache basi. Kiminyio

    ReplyDelete
  31. Mdau wa 01:46 inaonekana upo majuu unaosha masufuria kwa hiyo kiswahili cha bongo hukiwezi tena. Wenzako wadau wameelewa anauliza nini na ndio maana wameweza kujibu. Wewe data unadhani ni number tu!! Rudi bongo upanue mawazo! Nimezifurahia sana hizo picha na nimefurahi kuona wamasai wanaendeleza mila zao. Sikupata kuwaona kwenye vazi kama hilo, kwa hiyo hapo bado wanaugulia vidonda vya tohara!Asante mdau kwa picha nzuri sana.

    ReplyDelete
  32. Nafikiri mwanalibeneke alikuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuwauliza kwa nini wapo hivyo?.

    ReplyDelete
  33. HAWA NI SKOLIO. WAMEMALIZA JANDO NA MAFUNZO YA JANDO BAADA YA TOHARA NA WAMEPONA. BADO WAPO KWENYE MAFUNZO YA KUFUZU KUWA MORANI KAMILI. BAADA YA HIYO HATUA WATAOSHWA NA KUBADILI NGUO KUWA NYEKUNDU NA WATAJIPAKA RANGI NYEKUNDU USONI NA KICHWANI, PIA WATAANZA KUSUKA. HAPO SASA NDIO WANAKUWA MORANI KAMILI NA ASKARI WA GENERATION HII! MDAU ALIELEZA VIZURI KUWA NI MIAKA 7 YA TOHARA NA MIAKA SABA MINGINE INAFUNGWA. KWA KIPINDI CHOTE HIKI CHA MIAKA 7 WAO WANAKUWA MORANI LAKINI JUNIORS KWA MORANI WALIOTANGULIA MIAKA 14 ILIYOPITA. MIAKA 7 YA TOHARA IKIPITA WALE SENIOR WANAKUWA ILPAYANI! HAWA NDIO WACHUKUA NAFASI HIYO KWA MIAKA MINGINE 7. HAINA MWISHO HADI UKAMILIFU WA DAHARI! MASAI ASILIA!!

    ReplyDelete
  34. Hawa ni masaai halisi wametoka sunnah! watakuwa hivi kwa muda flan kabla ya kurejea katika hali yao halisi.

    Kwa mujibu wa mila zao utaratibu huu wa sunna hufanyika kwa miaka saba mfululizo na mara baada ya hapo zoezi hili hukom mpaka miaka mingine saba ijayo. Ndio maana inakuwa nadra kuwaona vijana kuwa katika hali hii! Sina hakika na wale akinadada wanaokutana na mkono wa ngariba, lakini tafiti zinaonyesha kuwa kutokana na huu utandawazi mangariba imewabidi kuwawahi watoto wadogo mapema kuepuka kanjanja la wanaharakati!

    ReplyDelete
  35. Hao wanaitwa "skolio" ni vijana walitoka jandoni muda cmrefu,wanavaa hizo kwa kipindi chote wanapukuwa kwenye hayo mafunzo baada ya hapo,ndio wanakuwa morani rasmi,nakufanyiwa sherehe kubwa,baada ya hapo ndio wanaanza kuvaa zile nguo nyekundu kuashiria morani kamili,mdau aliyepiga hizi picha endelea kuwaona hao vijana kwa kipindi cha miaka7 coz ndio wameanza kutahiriwa sasa,baada ya hyo miaka wanafunga hadi miaka 7 mingine, Jamani kama huyu mila za kimasai usichangie kwasababu utawapotosha watu wengine coz kuna watu humu wamechangia vitu vya uongo vingi tu. Mdau,kutoka Arusha!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...