Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh Fatuma Mwassa akiwa meza kuu na viongozi wa NHIF na wa mkoa
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh Fatuma Mwasssa akihutubia mkutano huo
 Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw Emmanuel Humba akitoa maelezo ya mfuko huo
 Wadau wa NHIF waakifuatilia kwa makini mkutano huo wa uhamasishaji na elimu kwa umma


Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa amezitaka halmashauri za wilaya mkoani humo kuongeza juhudi katika kuihamasisha jamii kujiunga na mfuko wa Afya ya jamii ikiwa ni  hatua muhimu ya kuwawezesha kupata huduma ya matibabu kupitia mfuko huo.

Akizungumza katika mkutano wa wadau wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya uliofanyika mjini Tabora,mkuu huyo alisema halmashauri na wadau wengine wa mfuko huo  wanaowajibu katika kuuelimisha umma kuhusu mfuko huo ikiwa ni hatua muhimu  ya kufanikisha dhamira ya Serikali kwa kila mtanzania kuwa kwenye utaratibu wa Bima ya Afya.

Alisema ni ukweli usiopingika kuwa gharama za matibabu zimekuwa zikipanda mara kwa mara huku akibainisha kuwa njia pekee ya kumkomboa mtanzania ni kumpa uhakika wa kutibiwa yeye pamoja na familia yake kupitia mfumo wa Mfuko wa Afya ya jamii ambao unaratibiwa na NHIF.
Pamoja na kuainisha masuala kadhaa ya faida za mFuko huo Mkuu huyo wa mkoa alitoa mfano kwa nchi nyingi duniani zimekuwa zikifanikiwa katika masuala ya Afya kupitia Mifuko ya aina hiyo.

“Kwa wenzetu suala la Bima ya Afya ni la lazima kwa kila mtu,hata kwa wengine wanaopata fursa ya kwenda nje ya nchi kusoma ni lazima uwe umejiunga vinginevyo hutaweza kupokelewa”alisema Bi.Fatma Mwassa

Hata hivyo kwa upande mwingine mkuu huyo alionesha masikitiko yake juu ya uchangiaji mdogo wa huduma ya  Mfuko wa Afya ya Jamii  CHF huku akianisha takwimu zinazoanzia Januari 2012,ambapo kati ya kaya 410,148 zilizopo mkoani Tabora ni kaya 14,860 tu ndizo zilizojiunga na mfuko huo ambayo ni sawa na asilimia 3.6.

Aidha pamoja na kuwa mkoa wa Tabora ndio chimbuko la la Mfuko huo wa Afya ya Jamii CHF ambao ulianzia wilayani Igunga kwa halmashauri zote hapa nchini lakini jambo la kushangaza bado halmashauri nyingine zilizopo mkoani Tabora zinashindwa kufanya vizuri katika kufikia lengo lililowekwa na Serikali.

Kwaupande mwingine mkuu huyo wa mkoa Bi.Fatma alilazimika kuwataka wadau na halmashauri kwa ujumla kutumia vikundi vya ushirika pamoja na vyama vya msingi kama njia muhimu itakayosaidia kuandikisha wananchi waliowengi kujiunga na CHF.

Mkutano huo wa wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ulihudhuria na baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu kitaifa wa NHIF,Katibu tawala mkoa wa Tabora,Wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Tabora,waheshimiwa wabunge,Viongozi wa halmashauri za wilaya na manispaa wakiwemo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...