Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Konyagi Nchini,David Mgwasa (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam kwenye hafla fupi ya kukabidhi vyerehani kwa Mbunge Viti maalum Mkoa wa Mbeya,Dr Marry Mwanjelwa (kulia) kwa ajili ya vikundi vya akina mama wa Mkoa wa Mbeya.
Mbunge Viti maalum Mkoa wa Mbeya,Dr Marry Mwanjelwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam muda mfupi baada ya kupokea vyerehani kwa ajili ya vikundi vya akina mama wa Mkoa wa Mbeya ikiwa ni msaada uliotolewa na Kamkuni ya Konyagi nchini.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Konyagi Nchini,David Mgwasa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. vyereani!!, shule gani hiyo? na mwalimu gani huyo?

    ReplyDelete
  2. Yaani kiswahili kinauwawa hivihivi,

    ReplyDelete
  3. Habari Ankal!

    Hivi mi naomba kuuliza, Bw. David Mgwassa hawezi kuvaa kiuongozi kwani nadhani yeye ni mfano wa kuigwa kwa jamii anayoiongoza! Labda nitakuwa nipo nyuma sana kuhusu mavazi ya viongozi wa taasisi na makampuni ya umma! amevaa shati la linen vifungo hajafunga na cheni (nyororo) la dhahabu linaninginia shingoni, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Konyagi (Kunywa Ongeza Nguvu Yako Angalia Gongo Inaua)! Haya we Utandawazi uliotukuka! Naomba kutoa hoja!

    H. A. Mashaka
    shark_ham@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  4. Konyagi inabidi muongeze maendeleo zaidi kwa uzalishaji na ushirikishwaji wa umma.

    Inabidi akina mama kule Musoma ambako nao wanazalisha biidhaa hii ingawa wao hawana vibali na leseni itabidi wawauzie ninyi wenye leseni na wao kujikomboa kiuchumi au siyo BOSS David Mgwasa?

    ReplyDelete
  5. Mdau H.A Mashaka wa tatu Anonymous wa Tue Apr 03, 10:28:00 AM 2012

    Sasa Mdau ukiambiwa Ndugu David Mgwasa ni Bosi wa 'KONYAGI' sio Bosi wa BENKI elewa uzalishaji wa bidhaa unaofanyika ktk shirika lake ni bidhaa 'nzito' vilevile ina Timu mbili, TIMU YA URAIANI na TIMU YA MSITUNI, hivyo yeye binafsi inabidi awe Kisela zaidi kuliko ki u bosi au siyo?

    ReplyDelete
  6. Hahahaha Mdau Bosi wa Konyagi na kuvaa suti wapi na wapi?

    Kama unavyoona kwa maoni ya Wadau wa mwanzo hapo juu timu zipo mbili ya Hadharani na ya Mafichoni na zote ni TIMU KALI SANA!

    ReplyDelete
  7. He he he he,

    Makali ya Konyagi mchezo?

    Bosi wa Konyagi akivaa suti wateja wa kinywaji wataandamana hadi Kiwandani Keko!

    ReplyDelete
  8. Hahaha Konyagi inamweka mtu chali na muda mwingine ukasahau kufunga zipu ya suruali, je ungekuwa wewe utaweza kukumbuka kuvaa suti?

    ReplyDelete
  9. Unaambiwa Bosi wa 'Kampuni ya Konyagi' ,,,,,sasa angekuwa Bosi wa Kampuni ya Soda ndio angevaa suti!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...