Kaka naomba kuwasilisha

Katika gazeti la jana "The Guardian" toleo namba 5411 kulikuwa na habari inayomuhusu mtoto anaehusishwa na kifo cha mwigizaji sinema KANUMBA aliefariki hivi karibuni

Cha ajabu ni kuhusu Kidhungu/Kikristo/Kiingereza kilichoandikwa hapo kwenye kichwa cha habari hiyo, kilisomeka "Actor "Lulu" arraigned over Kanumba's death" by correspondent Karama Kenyuko

Nilijiuliza maswali mengi mengi bila kupata majibu:
  1. Hivi ni Kidhungu changu ndio chenye matatizo au ni Muandishi na Mhariri wake ndio wasiojua Kidhungu?
  2. Hivi huyu Lulu ni Msichana/Mwanamke au Mvulana/Mwanaume?
  3. Je Mhariri alipitia hii habari kabla ya kuandika au na yeye ndio akina sisi "Kayumba" tulisomea shule za kata
Kwa ninavyomfahamu "Lulu" ni msichana sasa kwanini muandishi aliandika "Actor" badala ya "Actress" na kwanini Mhariri hakuipitia hii habari na kurekebisha kasoro hii

Naamini "The Guardian" ni gazeti makini lakini napata wasiwasi na uwezo wa waandishi wake na wahariri pia maana makosa kama haya yamekuwa yakitokea mara kwa mara lakini sasa nimeamua kusema na ili wahusika wachukue hatua

Naomba kuwasilisha
Mdau
-------------------
JIBU KUTOKA KWA MHARIRI WA THE GUARDIAN
Kuh.: ‘LULU’ NI “ACTOR”, AU “ACTRESS”?
Naitwa Wallace Mauggo. Ni Mhariri wa The Guardian (ya kila siku isipokuwa J2).  Nina uelewa mzuri kiasi wa Kiingereza, na wala usiwe na wasiwasi na elimu yangu au weledi wangu.  Kama binadamu wengine wote (ikiwa ni pamoja na wewe), mara moja moja nasi (waandishi wa habari na wahariri) “huteleza” na inapobidi (kulingana na misingi ya taaluma yetu, n.k.) huomba radhi na kufanya masahihisho. Kwa maana hiyo, sisi ni waungwana na tunajali sana kazi yetu. 

Kuhusu matumizi ya ama “actor” au “actress” kwa upande wa ‘Lulu’, naapa kwamba hatukukosea hata kidogo kumtaja msanii huyo kama “actor”. TUKO SAHIHI KABISA, kwa mujibu wa kanuni za sarufi (grammar) ya Kiingereza. Ushauri: Hakuna lugha isiyokua – na Kiingereza kinatatanisha sana. Hauko peke yako kuwa na wasiwasi – hata kwa upande wangu ni hivyohivyo, na ndiyo sababu miongoni mwa rafiki zangu wa karibu sana ni ‘dictionaries’ (nzuri) na Thesaurus. Hebu tupate mwongozo kutoka Macmillan English Dictionary for Advanced Learners (International Student Edition) chapisho la 2005:
Actor: Someone who performs in plays and films, especially as their job
Actress: Woman who performs in plays and films, especially as her job. Many women performers prefer to be called actors rather than actresses.
Katika enzi hizi za kuzingatia umuhimu wa masuala ya “gender”, haki na usawa kwa watu wenye ulemavu (zeruzeru?/albino? Chairman?/Chairwoman?/Madam Chair?/Chair?), n.k. sharti lugha nazo ziende na wakati na matakwa ya jamii – na ni hatari kuwa “too rigid”.
Sina hakika kama ufafanuzi huu utakuwa na manufaa yoyote kwako, au utaamua kuendeleza mjadala. Vyovyote vile itakavyokuwa, nakushukuru SANA kwa kutusoma (The Guardian) na kutukosoa – nikiamini umefanya hivyo kwa nia njema.
Kila la heri! WM.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 41 mpaka sasa

  1. Wallace (kaka yake peda) hujatoa hitimisho la ufafanuzi wako. ulitakiwa umalizie kwa hiyo....kauli zao bado ziko hewani

    ReplyDelete
  2. Kwa mujibu wa "Cambridge Online Dictionary", Actor ni "someone who pretends to be someone else while performing in a film, theatrical performance, or television or radio programme", na Actress ni "a female actor". Kwa hiyo actor anaweza kuwa yeyote. Lakini Actress ni mwanamke pekee!! Msahihishaji ajaribu kuangalia "Dictionary" kwanza kabla ya kusahihisha watu.

    ReplyDelete
  3. Bila kujali nani yuko sawa au kakosea kwenye matumizi ya neno hili, napenda kumpongeza mhariri wa the Guardian kwa kuwa muungwana na kukubali kukosolewa. Mimi ni msomaji mzuri wa gazeti hili pendwa, na kwakweli wanajitahidi sana kudhibiti grammatical errors,lakini hii si lugha yetu kwahiyo makosa yaweza tokea.Kukiri kosa ni moja ya njia ya kuboresha umakini in future, so nawapongeza wote, mkosoaji na mkosolewa kwani through both of you namimi nimejifunza!

    ReplyDelete
  4. Safi sana bwana MAUGGO yani umefafanua vizuri kiasi kwamba umenifurahisha

    kwa upande wangu nakubaliana kabisa na maneno yako

    waandishi wa habari ni binadamu kama binadamu wengine kukosea ni kawaida ya binadamu

    jambo la pili kuhusu huyo bwana anaejifanya kukosoa watu kwanza kabisa achana na usemi wa KANUMBA japokuwa umeandika KAYUMBA

    kukosea jambo kingereza hakuitwi kanumba

    mimi mwenyewe kwa upande wangu niliwahi kujiona mjuaji na kuanza kubishana na mke wangu

    Neno DRIVER mke wangu alipomaliza kufanya mtihani wa kuendesha gari alipofanikiwa kupata DRIVING LICENSE yake ya kuendeshea gari

    alimuandikia mtu msg na kumwambia nimepata DRIVER yangu

    niliona kuwa kakosea na kumbe hakuwa amekosea maana nilivyojuwa mimi ile huitwa DRIVING LICENSE

    sikujuwa kama unaweza pia kuita DRIVER
    baadae nikajaribu kufatilia kupitia internet nikachambua nikapata jibu kuwa unaweza kutumia jina la DRIVER

    sasa basi wadau tusipende kukurupuka kwenye jambo bila kulifanyia kazi au utafiti wake

    hata kwa ndugu yetu ANKALI MICHUZI watu wengi wanaopenda kumkosoa akikosea kidogo
    wanasahau kuwa ankali ni binadamu kama binadamu wengine anaweza kukosea kama anavyokosea mwingine


    mdau wa mpakani kwa shamba la bibi.

    ReplyDelete
  5. Aisee..hii imenifurahisha sana inaelimisha sana.Asante mtoa mada..Asante bwana Wallace kwa hizo updates..

    Nyongeza kidogo tu bwana Wallace,na mimi kama msomaji wa 'The Guardian' kwenye hili Gazeti mnatumia kiingereza kigumu sana..kama vile mnawalenga wasomaji wanaokifahamu sana kiingereza..Legezeni lugha tumieni maneno rahisi ya Kiingereza ili na wale wenye upeo wa kawaida wa kiingereza waweze kusoma Gazeti lenu.Mfano Leo nilikuwa nasoma article moja kwenye gazeti hili kuhusu maambukizi ya virusi vyuo vikuu nikakutana na neno "intoned"lakini pale kulikuwa na uwezekano wa kutumia neno,rahisi mbadala,

    David V

    ReplyDelete
  6. Nafikiri ingekuwa vizuri kupitia google au dictionary.com kabla ya kuhukumu elimu za watu kwa vigezo vya matumizi ya neno moja. Kama muulizaji angetumia "reference" kama mwenzake alivyomjibu, sidhani kama angeuliza maana tayari angekuwa na jibu. Hivyo angeweza kutumia muda aliopoteza kufanya mambo mengine ya maendeleo. I like the polite and humble response.

    ReplyDelete
  7. Brother Michuzi,

    The debate on whether or not the Guardian Reporter and Editor did any harm by addressing Lulu as “an actor” has drawn attention to many, me included! I especially applaud the level of professionalism portrayed by the Editor, Mr. Mauggo, coming out in public, saying sorry (for mistakes) but at the same time goes beyond that to challenge the doubters!

    I took special interest on the matter and upon my perusal onto several sources it came to my notice that an actress is female while an actor is male, and these are the main differences between the two (i.e. in a traditional English grammar/(rigid position). However, various definitions/explanations goes further to suggest that an "actor" is one who is significantly talented, can portray a character on stage, in films, or on television, and is either male or female while an "actress", on the other hand, is a female who has very low acting ability, but nonetheless gets roles in those mediums. Usually her career is based on her looks and appeal, not any talent.

    The sources further suggest that a female actor is offended if called an "actress'

    I therefore agree with the Guardian reporter and the corresponding Editor, they did no harm, neither to Lulu nor to the language itself.

    References:-

    The online free dictionary (www.thefreedictionary.com/actor)
    1. (Performing Arts / Theatre) a person who acts in a play, film, broadcast, etc.
    2. Informal a person who puts on a false manner in order to deceive others (often in the phrase bad actor)
    Usage: To avoid referring to people by their gender, actor is often used as a general term for women and men who act.

    The Collins Online Dictionary (www.collinsdictionary.com/dictionary/english/actor)
    A person who acts in a play, film, broadcast, etc
    Informal a person who puts on a false manner in order to deceive others (often in the phrase bad actor), performer, player, artiste, leading man or lady

    Mdau from Puli-e-Khumri
    Afghanistan
    16 April 2012

    ReplyDelete
  8. Ingawa mie sie nilieleta lalamiko hilo,ila nimependa jinsi Ndugu mauggo ulivyoonesha KUJALI kwako suala hilo,hakika nimevutiwa sana na majibu yako mazuri yenye unyenyekevu kwa MTEJA wako,hii ndio inatakiwa haswa.Kwa niaba ya MUHUSIKA mi nasema ahsante.

    ReplyDelete
  9. Alfred LucasApril 16, 2012

    Nimefurahishwa sana na majibu wa Wallace Maugo hasa katika ufafanuzi wa matumizi ya maneno Actor na Actress. Hii hatari ya kuwa 'too rigid' isiwe katika somo hili la lugha tu, hata katika sekta nyingine na maisha yetu ya kila siku. Tukiruhusu mawazo mgando, tutabaki kubishana kila siku huku wenzetu wakisonga mbele kwa kutumia muda vema. Sidhani kwa ufafanuzi huo kama mjadala utaendelezwa.

    ReplyDelete
  10. Umombo unatupa taabu sana wabantu.
    Kwa undani hapa palikuwa hakuna gongana lugha. LULU ni msichana na hivyo aweza kuwa actor au actress. Aliyeandika kwenye Guardian bila shaka ana background ya Canada au marikani.Huko wasichana wengi actresses wapenda waitwe actors kuondoa sexism.Mbantu wananitia kizunguzungu.

    ReplyDelete
  11. Mkuu umejibu vyema nina imani hata aliyekuwa na utata kaelewa.Kama ni mtihani umejibu vyema kabisaaaaa bila jazba na kwa ufasaha.

    Keep on

    ReplyDelete
  12. wallace upo right katika definition as also a section katika Dictionery.com says 'usage The term actor is almost universally used nowadays to refer to people of either gender who act'
    BUT i totally differ that this has any relation to equality on gender. nothing at all. in fact you are referred to political correctiveness than equality. Chairmen/man vs chairperson is for correctiveness as if it is chaired by a female then the word loose meaning...nothing to do with equality. well sported

    ReplyDelete
  13. Well written and explained properly!!

    ReplyDelete
  14. Hakuna kitu! yaani ndio kwanza umeweka mafuta kajaribu kuzima moto. Watanzania lini tutakuwa wazi? Huwezi kuja hapa na kusema "usiwe na wasiwasi na elimu yangu" bila kuweka vielelezo. Tunapenda sana kupigan domo bila kuonyesha matendo. Weka kila kitu wazi sisi ndio tutakuwa waamuzi na sio kutaka kujifagilia.

    ReplyDelete
  15. Kusema ukweli nimefurahishwa na majibu ya mhariri wa gazeti la the Guardian. Ni ufafanuzi mzuri uliotolewa kwa njia bora kabisa isiyo na uchafuzi wa hali ya hewa, nadhani watanzania tunatakiwa kuwa hivi hata katika masuala yote.

    ReplyDelete
  16. Mhandishi hajakosea kabisa.
    Sababu uwe mwanamke au mwanaume u act in a film or movie. so u r actor.
    Pia, kutokana na usawa katika jamii, mara nyingi maneno mengi ya kutenganisha mwanamke na mwanaume siku hizi yanakua kama neno moja tu.
    mfano actress ni actor pia.

    ReplyDelete
  17. Mwandishi huyu ni muungwana sana,tena analugha ya uvumilivu na unyenyekevu.Kazi yake hii inanfaa sana,mimi nampongeza sana.

    Watu wasojua lugha sawasawa,na wasojua uchambuzi wake ni wepesi sana wa kulaumu laumu tu.

    Ahsante sana mwandishi ndg Maugo kwa ufafanuzi wake.Wewe kaendelee na kazi kama jamaa ataka kuendelea ubishi wachana naye.

    ReplyDelete
  18. Ukweli ni kwamba mkubwa akikohoa basi jua tu kwamba amekili kosa.natia shaka hiyo dictionary.inavuruga uhondo ona hiyo:Actor: Someone who performs...,especially as their job.Jamani kwa nini isiwe ...especially as his/her job.
    Nye kdhungu basi tuachage tu.

    ReplyDelete
  19. Hola Hola Wallace, hapa ni either inappropriate use of verb au makosa yetu kitanzania. Kwani sisi wa-tz tunamatatizo ya lugha hiyo hata kama tuna-masters degree. Lugha hiyo imetupiga chenga isipokuwa kwa wenzetu wachache waliovalia njuga na hawakukimbia umanda wa lugha hiyo.
    Pia-tuache kile kitabia chetu wa-tz, sikubali kishindwa na kuingiza mbinu na ujanja ujanja.
    Kwa maana dictionary uliyoitaja ime-define bayana bila hila na ujanja kuwa “Actress” a woman who performs on the stage etc. Suala la actress kutaka aitwe Actor ni “mengineyo” katika dictionary hiyo kwani imeandikwa kama kidokezo na mengineyo kuwa “Many women now prefer to be called Actors, although when the context is not clear, an actor is USUALLY understood to refer to a MAN.
    Sasa wewe context yako iko wapi, na pia si kweli kuwa ma-actress wa Tanzania wanaprefer to be called Actors. Je si kati ya misingi ya lugha za uandishi kutotumia jargons, context au verbs zisizoeleweka katika jamii unayoilenga? Tuache ubabaishaji. Alex bura, dar

    ReplyDelete
  20. actor can be use for man or woman

    ReplyDelete
  21. Ndugu mhariri nimependa ulivyomfafanulia huyo mdau.ningemshauri aulize kwanza kabla ya kuja huku na kuropoka mbele za watu. tena anapaswa akuombe msamaha mara moja

    ReplyDelete
  22. Lugha ya Kikristo ni mojawapo ya lugha zinazogawa binadamu katika jinsia. Hii imekuwa mojawapo ya vita inayoendeshwa na akina mama kukomesha ubaguzi wa kijinsia. Baadhi ya maneno kama actress, air hostess, mistress, and other '..resses' ni obselete - hayatumiki tena. Mhariri yuko sahihi.

    ReplyDelete
  23. Asante na mimi nimeelimika maana nilikuwa najua mwanamke ni actress.

    ReplyDelete
  24. wasalaam, NAOMBA KUCHANGIA japo kiduchu.
    Mdau umegusa pakubwa. Na hoja yako ni ya msingi sana.
    Japo mhariri analazimisha baya kuwa jema si vibaya akakubali ni kwa matakwa yake na hao baadhi ya watakao kuitwa hivyo kama kamusi au kitabu alicho tumia kunukuu.
    Kwa uelewa wangu Hata tafsiri alotunia na ilivyonukuliwa imethibitisha kuwa SI RASMI. Lulu akiwa mwanafamilia wetu na kwa kumfahamu japo kidogo Natambua kwenye Lugha ametulia nikimaanisha anakielewa kiingereza vema.
    Kwa kauli hii na kutokana na nukuu aliotumia Mhariri namhesabu kuwa amekosea kwasababu TAfsiri isio Rasmi yasema:- wanawake wengi gupendezewa kuitwa "Actors" swali langu ni Je Lulu aliafiki kuwa mmoja wa hao wapendao kuitwa hivyo?

    ReplyDelete
  25. ulieuza swali umefanya vyema ila pia ungejaribu kupitia kamusi yako ya kiingereza au hata unge-google kwanza.

    mhariri hajakosea ila kwa mazoea ya neno actor ni kweli hua linatumika zaidi kwa wanaume na actress kwa wanawake.

    ila kama alivyosema mahariri kutoka kwenye kamusi yake pia ukitazama kamusi nyingine kama cambridge advanced learners utaona kua "actor is someone who pretends to be someone else while performing in a film, theatrical performance, or television or radio programme"

    while "actress is a female actor"

    chukua mfano wa neno GAY AND LESBIAN

    Eddy

    ReplyDelete
  26. Rejea on-line popular dictionary: http://www.thefreedictionary.com/actor.

    Kuna sentensi chache nimezi-copy kutoka hapo:
    actor [ˈæktə]
    1. (Performing Arts / Theatre) a person who acts in a play, film, broadcast, etc.
    2. Informal a person who puts on a false manner in order to deceive others (often in the phrase bad actor)

    Usage: To avoid referring to people by their gender, actor is often used as a general term for women and men who act.

    Actress:
    Usage: The use of actress is now very much on the decline, and women who work in the profession invariably prefer to be referred to as actors.

    ReplyDelete
  27. eeh bwana wewe,kubali tu mliteleza,grammar haina siasa!actress ni jina zuri na mahsusi sana kwa kina dada waigizaji,and not otherwise!waliobuni majina hayo mawili tofauti walikuwa wanachokifanya,kuongeza ladha na nakshi ya lugha!wanawake wasikie fahari kuitwa Jike wewe!akiitwa Dume wewe,atajisikiaje,ni sifa au dharau kwa mwanamke kuitwa Dume!

    ReplyDelete
  28. World English Dictionary
    actor (ˈæktə)

    — n
    1. a person who acts in a play, film, broadcast, etc
    2. informal a person who puts on a false manner in order to deceive others (often in the phrase bad actor )

    usage The term actor is almost universally used nowadays to refer to people of either gender who act

    Collins English Dictionary - Complete & Unabridged 10th Edition
    2009 © William Collins Sons & Co. Ltd. 1979, 1986 © HarperCollins
    Publishers 1998, 2000, 2003, 2005, 2006, 2007, 2009

    ReplyDelete
  29. ndugu mwandishi wa habari kuhusu hio dictionary inasema many women they like to be called actor but hio ni debatable na bado haijawa official, so as far as im concern wanawake watabakiwa kuitwa ACTRESS please, nakubaliana na maneno yako kwamba na nyinyi ni binadam na english vilevile mmejifunza shule kama wasomi wengine so haina haja kuhukumiana kama kunamistake tutaendeleana kusaidiana
    thanks

    ReplyDelete
  30. Huyu mwandishi asijitete kwa namna hiyo ya kuhalalisha makosa, na hapa tena anasema katika sentensi ya kwanza "Actor: "someone who performs in plays and films,especially as their job"
    kwnini asiseme "as his job or her job" na amesema "as their job" wakati sentensi hii inaonyesha umoja toka huko mwanzo na hii "their" inaonyesha uwingi.
    Usitutinge, kama ni dictionary ndo imesema hivyo basi hiyo dictionary tutaomba tuifute ili itolewe kwenye maktaba zetu, maana inapotosha.

    mimi ni mwalimu wa kiingereza mzoefu na wanafunzi wangu wanafaulu somo hili.
    Toka; Los Angeles ni mimi naitwa komba.

    ReplyDelete
  31. Kwa hiyo ili kukidhi matakwa ya jamii katika masuala ya gender na Princess naye tuanze kumuita Prince?

    ReplyDelete
  32. too simplistic analysis.

    ReplyDelete
  33. duh! yani tunashindwa kuelewa ya kwamba badala ya "his/her" unatumia "their"? halafu unajiita mwalimu mzoefu?

    nyie ndo mnakaririsha wanafunzi halafu wakikwama huko hawana pa kukimbilia!!!

    ReplyDelete
  34. ubishi sasa wabongo hakuna kujitetea hapa actor ni sahihi bila maelezo anebisha yuko dunia nyingine.

    ReplyDelete
  35. Namheshimu sana Wallace Mauggo kama mmoja wa waandishi wa habari mahiri kabisa Tanzania na mwalimu wangu wa uandishi wa habari. Huyu jamaa ni 'kichwa', lakini natofautiana naye katika hili la kutetea kumwita mwigizaji wa kike 'actor'. Mauggo ni mmoja wa waandishi wa habari wa Tanzania wanaoielewa vizuri lugha ya Kiingereza na nina hakika si yeye aliyeandika 'headline' hiyo lakini imebidi aitetee kwa kuwa yeye ndiye mhariri wa gazeti hilo. Kama alivyosema, si kosa kumwelezea mwigizaji wa kike kama 'actor' lakini ni sahihi zaidi kubainisha jinsia na kutumia neno 'actress'. Hakuna haja ya kutumia 'general term' kama 'actor' wakati unaweza kutoa taarifa zaidi kuhusu unayemwelezea kwa kutumia 'actress'. Ni sahihi kumwelezea mtoto wa siku mmoja kama 'mtu' lakini ni vizuri kuwa 'specific' kwa kusema 'mtoto mchanga'. Kwa mfano, kichwa cha habari 'Watu 30 wazaliwa Muhimbili siku ya Idd el Fitr' ni sahihi lakini ni 'awkward' kwa kuwa kuna umuhimu wa kuwa 'specific' na kusema 'watoto'.

    ReplyDelete
  36. As far as English language is concerned, the usage of 'actor' in place of 'actress' is a strong mistake which in any way whatsoever not tolerated and forgivalble. The phrase that gender activists especially women prefer being called 'actors' can not justify the 'bending' of the original meaning.
    It is good that the editor has agrred that we human beings sometimes make mistakes. So, in this saga your defence is baseless.
    Let's be free to give more comments on the issue.
    Yours Pungwa Kuchona, Makunduchi.

    ReplyDelete
  37. "Nonsense" Chembilecho Chonya of Chilonwa.Watu wanaacha kujadili ujumbe ulioandikwa kwenye makala wanajadili viingreza. Watu ambao siyo waingreza na wengi wao hawaishi Uingreza.

    Kwa taarifa tuu, magazeti ya kiingereza ya uingereza nayo pia huandika makosa kama haya. Ninasema hivi kwa sababu nimewahi kuona makosa kama haya yakitokea hata kwenye website za BBC.

    Kwa mfano, juzi tuu hapa David Cameron waziri mkuu wa uingreza alisema kwamba "Britain invented DNA". Haya sasa, waziri mkuu wa uingreza, Muingreza aliyezaliwa uingreza na kuishi maisha yake yote uingreza amekosea kuzungumza kiingreza.

    Sisi wabantu tunashindana kandika kiingreza.

    Tuache za "viingreza" tujadili yanayotuhusu.

    ReplyDelete
  38. Kuna duanzi mmoja humu anasema "Britain invented DNA" ni Kiingereza kibovu. Hiki ni Kiingereza safi kabisa isipokuwa statement hiyo inawezekana haina haina ukweli. Yaani huyu anashindwa kutofautisha factual na grammatical errors. No wonder hataki watu wajadili Kiingereza humu.

    ReplyDelete
  39. Wewe mdau wa 09:56am tarehehe 17/04/2012,unayenisema mimi mwalimu mzoefu, hujanielewa, mimi ndo namshangaa huyu mhariri ndiye aleyetumia "their" siyo mimi.
    Hebu soma vizuri nilivyoandika usikimbilie kumsema mtu.wewe na mimi tunatakiwa tumshangae huyu mhariri wa hili gazeti kubwa na maalufu nnchini.

    ReplyDelete
  40. Duh! "Britain invented DNA" ni kiingereza safi? kumbe ndiyo maana hamuandiki majina yenu kwenye kutoa maoni yeni.

    ReplyDelete
  41. The next thing we are going to hear ni: Her = he, him = her, man = woman....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...