Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (kushoto) , Mkurugenzi Mtenadaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) Elishilia Kaaya (kulia) na Mkuu wa Hazina Ndogo Arusha Rehema Mwakajube (katikati) wakibadilishana mawazo leo mjini Arusha mara baada ya kupata taarifa na kujionea maendeleo ya ukarabati wa vyumba mbalimbali vitakavyotumika katika mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambao utafanyika Mkoani Arusha kuanzia tarehe 28 mwezi Mei hadi Juni Mosi mwaka huu. Mkutano huo utawashirikisha karibu wajumbe 3000 kutoka ndani ya nchi na nje ya Nchi.
Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo(katikati) akitoa ushauri leo mjini Arusha kwa wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) juu ya hatua ambazo zinatakiwa kuchukua ili kufanikisha maandalizi mkutano huo ambao utafanyika Mkoani Arusha kuanzia tarehe 28 mwezi Mei hadi Juni Mosi mwaka huu. Mkutano huo utawashirikisha karibu wajumbe 3000 kutoka ndani ya nchi na nje ya Nchi.
Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo(kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo (kushoto) wakibadilishana mawazo jana mjini Arusha mara baada ya kumaliza kikao cha kuweka mikakati mbalimbali leo mjini Arusha itakayosaidia kufanyika kwa mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambao utafanyika Mkoani Arusha kuanzia tarehe 28 mwezi Mei hadi Juni Mosi mwaka huu. Mkutano huo utawashirikisha karibu wajumbe 3000 kutoka ndani ya nchi na nje ya Nchi.
Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo(kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo(kulia) wakiweka mikakati mbalimbali leo mjini Arusha itakayosaidia kufanyika kwa mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambao utafanyika Mkoani Arusha kuanzia tarehe 28 mwezi Mei hadi Juni Mosi mwaka huu. Mkutano huo utawashirikisha karibu wajumbe 3000 kutoka ndani ya nchi na nje ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...