Kwanza napenda kutoa pongezi kwa wanalibeneke wote kwa juhudi zenu za kutoa taarifa za matukio mbalimbali yanayotokea nchini kwetu.
Inaonyesha jiji letu la Dar es salaam halipo kwenye usalama kipindi cha mvua kubwa.
Hii imethibitisha mara kwa mara na inakuwa kama vile ni ishara kwamba inabidi zichukuliwe hatua za haraka kuepuka hili janga.
Dar es salaam ina mikondo yake ya maji tokea miaka mingi iliyopita ila sasa inaonyesha mikondo yake inazibwa.
Inaonyesha ujenzi mkubwa unaendelea katikati ya jiji, ila haieleweki unazingatia vipi maswala ya maji chafu ,safi pamoja na huduma nyingine kama vile umeme n.k
Uchimbaji wa mifereji hautotugharimu kama tutachukuwa hatuwa ya haraka haswa kwa utafiti wa picha zinavyoonyeshaili maji yanataka yaelekee yanakotaka.
( nadhani sote tunajuwa kuwa moja ya kazi zenye gharama kubwa ni kuzuia nguvu ya maji) Kuna gharama zinaikabili serikali ikiwa ni pamoja na kusaidia wanaoathirika na mafuriko.
Serikali itaendelea kukarabati barabara za kiwango cha lami mara kwa mara .
Sababu ,inajulikana kiuraisi tu maji yanapokuwa juu na chini ya lami basi lami ina tatizo la kuja kubomoka haraka.
Nimeweka mifano ya picha kutoka kwenye blog ya jamii na mfano wa ramani niliyochora haraka ya google.
Nimechora ramani ya haraka tu ,ila yeyote anayeweza kuchangia zaidi achangie haswa wasomi wa mambo ya ujenzi ,hii ni kwa manufaa ya jamii yetu.
Si walaumu jiji ila nawapa changamoto.Wanatakiwa waangalie kiumakini swala la ujenzi haswa barabara kubwa ,njia za maji chafu na safi ,na ujenzi wa maghorofa marefu yasiwe kwenye msongamano.
Haiusiani na siasa inausiana na haki za binadamu.
Tumshukuru Mungu ametuepusha na Tsunami.
Mdau
Pendekezo lako ni zuri. Ulichojiangusha ni kushindwa kwako kuilaumu Mamlaka ya Jiji.Usisite kuilaumu Jiji kama yaonekana bayana hawafanyi kazi zao inavyotakiwa. Lazima penye kila tatizo patokee wa kulaumiwa (The buck has to stop somewhere/ with someone) na ndiyo maendeleo hufanyika. Kushindwa kwa watanzania kumlaumu na kumwajibisha mtu yoyote kwa lolote lile ndio kumewafikisha hapo mlipo na hakika mtaozea hapo.
ReplyDeleteTunahitaji michango ya kiutaalamu kama hii sio tararira...tararira.... Wengine waboresha na kuonyesha sehemu nyingine tetete kama Bonde la Mpunga/MyFair, Boko msikitini, water ways za Jogoo/Kunduchi, na bottle necks za Tabata na Ali Maua. Asante Mtalaamu
ReplyDeleteSafi sana mdau, Tatizo hili linatokana na watendaji wengi wa serekali kuto kutubia akili au kukosa ubunifu.Wanataka hadi wazungu waje kuwekeza kwenye suala la mifereji na kuwazuia watu wasijenge kwenye mifereji.
ReplyDeleteSikujua kama Dar es salaam kuna Lake Tandale na Lake Mwananyamala. Kwani Lake ni nini?
ReplyDeleteTatizo kubwa ni kwa jiji kugawa viwanja bila ya kuzingatia uhifadhi wa mazingira. Matokeo yake ndiyo mafuriko kila kukicha.
ReplyDeleteMfano ni pale Msasani ambapo wamegawa viwanja na watu kujenga majumba ya thamani wakati ile ni njia ya maji ya asili. Munaona sasa matokeo yake?
Tathmini ya mazingira ni muhimu sana kwani hayo yote yangezingatiwa kwa umakini na kuangalia mbinu ambazo zingetumika kuwacha eneo la mkondo wa maji liwachwe kama kawaida.
Mazingira siyo Ngorongoro na Serengeti tu. Au mpaka tupate wazungu watuamrishe ndiyo tusikie?
Tusijenge kwenye njia za maji asilia waliokwishajenga ni heri kubomoa ili kuepukana na mafuriko na vifo.
ReplyDeleteNi Wazo kama ukivyoainisha. Hayo Ma-Lake uliyataja humo, ndo Utata unapoanzia. Sina uhakika kama yatakuwa Ma-lake kama unavyosema au Madampo..... Bahari ya Hindi inajitahidi sana kuficha upuuzi tunaoufanya mitaani kwetu. Mvua ikinyesha kwetu tunaona nafuu maana inatusaidia kufanya usafi..... Wasiwasi wangu hayo maziwa kama yatakuwa Sustainable au ndo misimu miwili yashajaa vifurushi vya taka ngumu na machupa ya plastiki
ReplyDelete