Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu akizungumza na madiwani wa manispaa ya Songea wakati wa kikao cha baraza la madiwani lililofanyika katika ukumbi wa manispaa hiyo ambapo alitoa siku 10 kwa manispaa hiyo kuhakikisha inazoa na kumaliza uchafu uliokithiri katika maeneo mbalimbali ya manispaa hiyo.kulia ni meya wa manispaa ya songea,Mstahiki Charlea Mhagama na kushoto katibu wa CCM wilayani songea mjini,Bi. Alphoce Siwale.
Meya Mstaafu wa Manispaa ya Songea,Herman Ndimbo akitoa neno la shukrani kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambung (hayupo pichani) wakati wa kikao cha baraza la Madiwani wa Manispaa ya Songea.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea,Charles Mhagama,kulia akizungumza na madiwani wa manispaa hiyo,wakati wa kikao cha baraza la madiwani lililofanyika jana mjini songea.kulia ni mkurugenzi wa manispaa hiyo,Bw. Zakaria Nachoha na kushoto naibu meya,Bi. Mariam Dizumba.
Baadhi ya madiwani wa manispaa ya songea kutoka chama cha mapinduzi,wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu (hayupo pichani) wakati wa kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika jana mjini songea.
Madiwani wa chama cha Chadema wakiwa wamekaa sehemu moja huku wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu wakati wa kikao cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo,kumekuwa namakundi ya namna ya kukaa kwa madiwani wa manispaa ya songea kutokana na itikadi za vyama vyao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. All diwani in this country are new graduates. Congraturatios

    ReplyDelete
  2. Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya nanihii ninaomba kuuliza...hivi haya majoho wanayovaa hawa madiwani yamebuniwa na nani? Na ni kwa nini ni madiwani peke yao tu wanaovaa namna hii na si wachaguliwa wengine katika mkoa/wilaya? Naomba mnisaidie...

    ReplyDelete
  3. Siku kumi kumaliza taka, but sehemu ya kutupa taka hakuna, muweke bin barabarani ili watu watupe taka huko, unless mtakuwa mnaweka maji kwenye gunia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...