Washiriki wa kitongoji  Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City Center 2012, wakiwa katika picha ya pamoja,tayari kuchuana vikali Mei  5 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.katika shindano hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni kwa viti maalum ni sh.25,000/= na kwa viti vya kawaida ni sh 15,000/=
Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi,Modern Driving School,ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano hilo.
Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa darasani kwenye mafunzo ya nadharia yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi,Modern Driving School,ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano hilo.
========   ========   ========
Mashindano ya Ulimbwende ngazi ya kitongoji  Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City Center 2012,yanatarajiwa kufanyika Mei  5 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.

Akizungumza leo jijini Arusha,Mratibu wa shindano hilo Bi Upendo Simwita kutoka  kampuni ya Tour Visual Entertainment ambao ndio waandaji wa shindano hilo,amebainisha kuwa mpaka sasa maandalizi yao yanakwenda vizuri na kila kitu kimekwisha kamililka ikiwemo sambamba na kuwapata warembo ambao mpaka sasa wametimia 20.

Bi Upendo Simwita amesema kuwa wameishakamilisha mchakato wa kuwapata Warembo wenye mvuto na wenye vigezo stahiki,anaongeza kuwa warembo hao wenye ari kubwa ya ushindani,kama waandaji watahakikisha muwakilishi wa Miss Tanzania 2012 anatokea kwenye kitongoji hicho.

“Shindano hilo litakalokuwa la tofauti kubwa na miaka ya nyuma litawakutanisha walimbwende wapatao 20,ambao watachuana vikali jukwaani, na hatimaye kumpata Mshindi wa Miss Arusha City Center”,alisema Upendo.Amesema kuwa kiingilia katika shindano hilo kimepangwa kuwa ni kwa viti Maalum sh 25,000/= na kwa viti vya kawaida sh.15,000/=. Fanya booking yako ya tiketi mapema kupitia namba – 0755975454 au 0713681059.

Kwa upande wa Burudani,Upendo  amesema kuwa kutakuwepo na Msanii mahiri wa Muziki wa kizazi kipya aitwaye Sam wa Ukweli,Muziki wa Asili,Live Band ya Watoto wa Simba pamoja na burudani nyingine  mbalimbali zitakazotolewa na walimbwende wenyewe siku hiyo.

Upendo amewataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni REDD’S  ORIGINAL,NAURA SPRINGS HOTEL,CLAUDS FM / CLAUDS TV AND MAWINGU CLUB – ARUSHA,BG HORIZON, MODERN DRIVING SCHOOL,MAKO ADVENTURE,SEBE&BEKI FOR LIFE, MWANDAGO INVESTMENT,S.G. RESORT,MEJA LINK LTD,GEO SECURITY,GOLDEN ROSE HOTEL,RIVERSIDE SHUTTLE SERVICES,ARUSHA TRAVEL LODGE,LITTLE ROSES, LA BELLA VISTA,WAKIPAMBWA NA JANETH BEAUTY PAURLOR NA BI. HADIJA HASSAN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. jamani, dada zetu wazuri!

    Viongozi mmeona yanayomkuta J Edward aliyekuwa mgombea uraisi wa USA?
    "John Edwards was accused of using illegal campaign contributions during the 2008 presidential race to cover up his pregnant mistress"By BEN FORER -ABC News

    ReplyDelete
  2. Kaka,

    Mbona unatubania? Mambo haya ndio yalikuwa yanafaa yawe na ile sentensi "KWA MAPICHA ZAIDI BOFYA HAPA".

    Sasa mbona hujatupa pa kubofya zaidi?

    ReplyDelete
  3. Warembo Arusha City Centre:

    Jamaa huko Arusha wanalima hadi juu ya mawe, kuanzia Makanisani, Migodini, Mashuleni ,Vyuoni na hadi Stendi za Mabasi kwa wapiga Debe na Masokoni!

    Fanyeni Urembo lakini mjihadhari saaana kutumiwa na SIASA ZA KI-ARUSHA ARSUHA ZA CHADEMA !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...