Mkurugenzi mpya wa Taasisi ya Vyombo Vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA) Tumaini Mwailege akiwaeleza waandishi wa habari umuhimu wa kupigania mazingira mazuri ya kazi na maslahi bora kazini. Mwailege ameanza kufanya kazi rasmi leo (1/5/2012) amechukua nafasi ya Rose Haji aliyemaliza muda wa utumishi wake katika taasisi hiyo mwaka jana. Katikati ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mohamed Tibanyendera akifuatiwa na Mjumbe wa bodi Elias Mhegera.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo Vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA) Mohamed Tibanyendera akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na jinsi taasisi hiyo inavyofanya kazi mbalimbali za kuhakikisha kuwa taaluma ya habari inaimarika hapa nchini huku Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Tumaini Mwailege akimsikiliza.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...