mkurugenzi mkuu wa SSRA Bi. Irene Isaka akiwasilisha mada kwa wastaafu wa mkoa wa Dodoma
 Katibu mkuu chama cha wastaafu mkoani dodoma bw. John Kanyetto  akieleza kero zinazowakabili wastaafu
 Picha ya Pamoja wastaafu wa mkoa wa Dodoma,Mkurugenzi mkuu SSRA, na mkuu wa Hazina ndogo mkoani dodoma Bw. Evance Assenga.

Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti  wa sekta ya Hifadhi ya jamii (SSRA) imekutana na Wastaafu wa mkoa wa Dodoma.Wastaafu hao walikutana na uongozi wa Mamlaka ili kuelezea mafanikio na kero wanazokabiliana nazo katika malipo yao ya Pensheni.

Wastaafu hao walimueleza mkurugenzi mkuu wa SSRA Bi.Irene Isaka kuwa Pensheni wanazolipwa ni ndogo sana ikilinganisha na hali halisi ya uchumi nchini.Wastaafu hao waliomba pensheni zipandishwe kulingana na thamani ya shilingi na pia sambamba na upandaji wa  kima cha chini cha mshahara.

Wastaafu waliipongeza Hazina kwa kutatua baadhi ya kero zao, kwani kero nyingi walizosiwasilisha katika kikao chao cha mwisho zimetatuliwa.

Pia waliipongeza Serikali kupitia Wizara ya kazi na Ajira  na waheshimiwa wabunge kwa kupitisha muswada wa mabadiliko ya sheria za mifuko ya hifadhi ya Jamii, kwani kwa kupitisha muswada huo wana imani kubwa kuwa Mamlaka imepewa meno nayo itafanya kazi  kikamilifu  na kuboresha pensheni,huduma  na mafao yatolewayo na mifuko ya Hifadhi ya jamii.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...