Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Sehemu ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na wafadhili Walter Reed, wanatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:-
1. PROGRAMME OFFICER: NAFASI MOJA (1)
Kazi za kufanya:
Kusimamia na kuratibu shughuli za mpango wa Huduma kwa wanaoishi na Virusi vya UKIMWI kwa kushirikiana na Mratibu wa Kudhibiti maambukizi ya UKIMWI Mkoa (Tiba)
Kutekeleza kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na Msimamizi wa Huduma za Afya Mkoa
Sifa za kuingilia:
- Wenye shahada ya Udaktari (MD) au Stashahada ya Udaktari (AMO) ambaye amehitimu katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
- Asiwe mwajiriwa wa Serikali au Taasisi nyingine ya Serikali na Serikali za Mitaa ndani ya Mkoa.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012
2. AFISA UFUATILIAJI NA TATHMINI (MONITORING & EVALUATION OFFICER 1 NAFASI MOJA (1)
Kazi za kufanya:
Kufuatilia na kutathmini maendeleo ya mradi kwa kushirikiana na Meneja wa Mradi
Kuwezesha na kutoa ushauri na tafsiri ya Sera, Mipango, mikakati na miongozo kuhusu taarifa za Afya kwa mujibu wa miongozo ya Wizara ya Afya
Kutekeleza kazi nyingine kama zitakavyoelekezwa na Meneja wa Mradi
Sifa za kuingilia:
- Wenye Shahada/Shahada ya Uzamili katika fani ya Mipango, Uchumi na Takwimu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
- Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012
3. MHASIBU:
Kazi za kufanya:
Kufanya kazi kwa kushirikiana na Meneja wa Mradi
Kusimamia shughuli zote za Uhasibu katika Mradi
Kudhibiti hati za malipo
Kujibu hoja za Ukaguzi
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012
SIFA ZA KUINGILIA:
- Awe na Shahada au Stashahada ya Uhasibu kutoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na Serikali
4. WATUNZA KUMBUKUMBU NAFASI TANO (5)
Kazi za kufanya:
Kufanya kazi kwa mujibu wa maelekezo ya Meneja wa Mradi
Kuandaa na kutunza taarifa /kumbukumbu na nyaraka mbalimbali za Mradi
Kukusanya na kuhifadhi taarifa mbalimbali za wagonjwa.
Sifa za kuingilia:
- Awe na Shahada au Stashahada, au cheti cha utunzaji wa kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012
Maombi yote yatumwe kwa:
Katibu Tawala wa Mkoa,
S.L.P. 74,
SONGEA.
AU
Mganga Mkuu wa Mkoa,
S.L.P. 5,
SONGEA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...