Kikundi cha EWB-USA kitakachowasili mwezi ujao.
ukarabati mfereji wa maji uliofanywa mwaka jana.
Wahandisi Wasio na Mipaka kutoka Marekani, [Engineers- without-borders USA] tawi la Chuo Kikuu cha Valparaiso, CHICAGO, watatembelea kijiji cha Masaera , Kata ya Kilema Kusini, wilaya ya Moshi Vijijini katika mkoa wa Kilimanjaro mwezi ujao.
Wahandisi hao ambao ni wageni wa kikundi cha MAENDELEO MASAERA watakuja kuendeleza shughuli ya kuukarabati mfereji wa kumwagilia wa kijiji cha Masaera, kazi iliyoanzwa miaka mitatu iliyopita.
Pamoja na kushirikiana na wenyeji wao kuujenga mfereji huo, wahandisi hao pia wamesaidia katika kumalizia ujenzi wa chekechea ya Shule ya Msingi ya Mandaka Mazoezi na kuwashauri wenyeji waimarishe upatikanaji wa maji safi na salama katika kijiji hicho.
Mwaka huu kwa ushirikiano na Rotary International na Boeing Corpration wanapanga waanze mchakato wa kuwapatia wanakiji maji safi na salama na kwa azma hiyo wameomba wakutane na mhandisi wa maji wa ofisi husika , pia na watawala na wanasiasa wa eneo ili waweze kushauriana kwa malengo ya kufanikisha azma hiyo.
Wako tayari pia kuangalia uwezekano wa kuchimba kisima cha maji safi katika kitongoji cha Masaera Kusini, endapo italazimu kufanya hivyo.
Wahandisi hao wamesema wako tayari kushirikiana na mashirika ya misaada kwa wananchi yaliyomo Tanzania ikiwa ni pamoja na makampuni makubwa ya uzalishaji na ya kibiashara.
Yaani wenzetu akina Erick, Josh, Frank, Amanda, wapo very simple and humble. Sasa wangekuwa ni watani zangu kutoka Bukoba, wote wangevaa suti na kushika blackbery tano kila mmoja mkononi. Ukitaka kuwaita majina lazima uanze na taito "injinia" Rutachokozibwa Esq. Huwezi kuonana nao bila kuweka appointment. Ukiuliza kwanini wanashindwa kutengeneza sindano ya kushonea nguo wajibu "htuna vifaa"
ReplyDelete