Naibu Waziri wa Sayansi na Mawasiliano Charles Kitwanga akifungua mkutano wa mwaka wa 32 wa Umoja wa Taasisi za Mawasiliano Kusini mwa Bara la Afrika unaofanyika nchini kwa siku mbili unaojadili mambo mbalimbali katika mawasiliano ya simu ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya kidigitali, mkutano huo unahudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 14 za (SADC) Zimbabwe, Namibia, Botswana, Malawi Msumbiji, Afrika Kusini Rethoto na Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa TTCL,Said Amir Said akimkaribisha Naibu Waziri wa Sayansi na Mawasiliano Charles Kitwanga kwa ajili ya kufungua mkutano wa mwaka wa 32 wa Umoja wa Taasisi za Mawasiliano Kusini mwa Bara la Afrika unaofanyika nchini kwa siku mbili unaojadili mambo mbalimbali katika mawasiliano ya simu ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya kidigitali
wajumbe mbalimbali kutoka nchi za SADC wakiwa katika mkutano huo.
picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...