Mama akiwa amembeba mwanae mgongoni huku kichwani akiwa amebeba mzigo wa mboga za majani akienda kuuza ili aweze kupata rizki ya kujikumu na Mwanae.picha hii imepigwa leo maeneo ya Pasiansi,Jijini Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Bravo akina mama...mnatutoa mbali siyo siri.Tunawapenda sana.!

    David V

    ReplyDelete
  2. Pengine, ana kitoto kingine tumboni!

    POLE SANA!

    ReplyDelete
  3. Hakuna mithili MAMA, katika hii dunia,
    Hata na awe RIKWAMA, ni "MAMA" tajivunia,
    Kwa ugonjwa na uzima, wa mwanzo mfikiria,
    RABI AWAJAZE MEMA, KATU CHA KUWAFIDIA.

    Katu hakuna malipo, MAMA zetu wafidia,
    RABI wangu mpe "PEPO", kwako keshatangulia,
    Cha kumlipa hakipo, "ubani" sitochoka tia,
    Siombe awe hayupo, jikhisi hujatimia.

    Mungu awajaze kheri, yenye shari wepushia,
    Na "Jannatu" wavinjari, wote walotangulia,
    Wana tusiwe viburi, MOLA hilo twepushia,
    Kama MAMA siyo siri, namba 'wani' tabakia.

    Kweli hakuna na hatatokea kama "MAMA" duniani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...