Zoezi la uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kiwila mkoani Mbeya limekamilika usiku hu kwa wananchi kushiriki kwa amani uchaguzi huo ambao umemwezesha mgombea wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Laurent Mwakaribule kuibuka na ushindi wa kura 2621 kati ya kura 1649 alizopata mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM).

Mwandishi wa mtandao  wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka mkoani Mbeya Moses Ng'wat anaripoti kuwa wananchi wa kata hiyo ya Kiwila wameshiriki uchaguzi huo katika hali ya amani na utulivu mkubwa na kuwa mbali ya mvua kunyesha katika eneo hilo ila bado wananchi walionekana kuwa na shauku kubwa ya kujua matokeo hayo.

Akitangaza matokeo hayo ya uchaguzi mdogo wa kata ya Kiwila msimamizi wa uchaguzi huo Lauden Nnala alisema kuwa Chadema ndio washindi wa uchaguzi huo huku CCM ikishika nafasi ya pili na NCCR MAGEUZI wakishika nafasi ya tatu kwa mgombea wake kupata kura 33 huku chama cha wananchi (CUF) wakiambulia kura 13 pekee.

Angalizo: Globu ya Jamii na washirika wake wanaendelea kufuatilia kwa karibu matokeo ya uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Arumeru Mashariki ambako habari zinasema kura zinaendelea kuhesabiwa hivyo matokeo bado hayajatangazwa. Tuvute subira tafadhali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. ChakubangaApril 01, 2012

    Stop these non sense ! We want to know Arumeru outcome and nothing else

    ReplyDelete
  2. Hivi kazi za madiwani ni nini? watanzania tuamke hizi nyadhifa nyingine ni za kutumbua kodi za wananchi.Badala ya kuwa na chaguzi za madiwani na sijui wabunge wa kuteuliwa ambao wanatoka ktk majimbo yaliyofanya uchaguzi pesa zinazotumiwa kuwalipa hawa watu zingetumika katika mambo mengine ya jamii... kwa muonekano wangu Wakuu wa mikoa wangekuwa wanachaguliwa badala ya kuteuliwa na rais maana wangeleta upinzani au maono tofauti na chama kilicho madarakani.

    ReplyDelete
  3. CHADEMA JUU JUU JUUUU ZAIDI ARUMERU
    CCM CHALI MIGUU JUU KIFO CHA MENDE.

    ReplyDelete
  4. Michuzi hata update basi ya Arumeru ndugu mbona umetubania hivyo. At least tumjue mambo yanaendeleaje. Au mzee chama chako kiko hoi bin taabani maana ulikuwa unajitahidi kutoa habari zao kweli hasa kwenye ufungaji wa kampeni ukagoma kabisa kutupa habari za upinzani. Naona itakua imekula kwako ndio maana uko kimya namna hii. Pole ndugu lakini kumbuka asiyekubali kushindwa si mshindani.

    ReplyDelete
  5. Can we know about Arumeru pls? Ankal mbona hutupi update za Chadema Arumeru? Chadema Ooyeeeeeeeeeeee,

    ReplyDelete
  6. ankal angalau tupe tathmini ya vituo vya kula usiuchune ndio mambo tunajua mulala chaleee

    ReplyDelete
  7. CHADEMA IMESHINDAAAAAAAAAAAAAAAA!!! ARUMERUUUUUUUUUU

    ReplyDelete
  8. chadema noma

    ReplyDelete
  9. arumeru chadema wameshinda. hii ni mara ya pili kwa upinzani kuibwaga serikali uchaguzi mdogo. mara ya kwanza ilikuwa temeke pale mrema alivyochezesha kwata serikali yote. hadi raisi alienda kupiga kampeni lakini mrema akaibuka kidedea.Hongera Chadema.

    ReplyDelete
  10. CHADEMA kidedea Arumeru, Kirumba na Kiwila. Kweli sasa mafisadi wanaanza kuondonewa mmojammoja hadi 2015 wataisha

    ReplyDelete
  11. CCM kazi mnayo,,,cha muhimu ni KUACHA KUUBEBA UFISADI ili muendelee ama sivyo mtachemsha mawe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...