Na Mwandishi Maalum

New York

Wakati Jumuia ya Kimataifa, ikijaribu kubuni mbinu na mikakati madhubuti ya kukabiliana na biashara ya binadamu, imelezwa kwamba biashara hiyo huwaingizia wahusika zaidi ya dola Bilioni 32 kwa mwaka.

Kwa siku nzima ya jumanne, maafisa wa ngazi ya juu katika wa Umoja wa Mataifa (UM), nchi wanachama , na wadau kutoka makampuni binafsi na wanaharakati, walikutana hapa Umoja wa Mataifa kwa kazi moja tu ya kujaribu kubuni njia mbadala za kupambana na biashara hiyo, pamoja na kuhimiza ushirikiano baina ya wadau wa mbalimbali.

Mkutano huo ambao uliandaliwa na Rais wa Baraza Kuu la 66 la UM Bw. Nassir Abdulaziz Al-Nasser, kwa kushirikiana na Muungano wa Kundi la Marafiki dhidi ya Biashara ya Binadamu na ulifunguliwa na Katibu Mkuu wa UM, Ban Ki Moon.

Ni kupitia majadiliano yaliyofanyika katika mkutano huo, ilipoelezwa wazi na wadau mbalimbali akiwamo Katibu Mkuu wa UM, kwamba hakuna nchi hata moja iwe kubwa na tajiri au ndogo na maskini inayoweza kukabiliana na biashara ya binadamu kivyake vyake.

Akizungumzia ukubwa na upana wa biashara hiyo na adhari zake kwa haki, uhuru na utu wa mwanadamu na hususani wanawake na watoto wa kike.

Ban Ki Moo anasema,mataifa yanatakiwa siyo tu kuongeza juhudi za kukabiliana na tatizo hilo bali yapashwa kushirikiana kwa karibu kutokana na ukweli kwamba hakuna nchi inayoweza kufanikiwa ikiwa peke yake.

“ Lazima tuongeze juhudi lakini ni muhimu sana kushirikiana kuzuia biashara hii na kuwalinda waathirika. Pale ambapo wafanyabiashara wanatumia vitisho na silaha. Sisi lazima tuwajibu kwa kutunga sheria na kuwafikisha mbele ya sheria wafanyabiashara hao” anasisitiza Ban Ki Moon.

Katika hatua nyingine Ban Ki Moon amezitaka nchi kukabiliana na mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine yanachangia au yanakuwa kichocho cha biashara ya binadamu.

Anayataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni umaskini uliokithiri unaopelekea baadhi ya wazazi kuuza watoto wao

Akasisitiza pia umuhimu wa nchi kusimamia na kutekeleza kwa vitendo mikataba na Itifaki zinazohusu haki za binadamu. Na hasa Itifaki ya Umoja wa Mataifa ya kuzuia ukandamizaji na unyanyasaji wa wanawake na watoto.


Takwimu zilizotolewa na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na madawa ya kulevya na uhalifu zinaonyesha kwamba. Katika wakati wowote ule watu milioni 2.4 ni waathirika wa biashara ya binadamu. Na kwamba biashara hiyo ni yenye faida kubwa ikiingiza zaidi dola bilioni 32 kwa mwaka na hivyo kuifanya kuwa biashara yenye faida kubwa ikishindana na biashara za madawa ya kulevya na uuzaji haramu wa silaha.


Aidha maelfu ya watu huangukia mikononi mwa walanguzi wa biashara hiyo ndani ya nchi zao na ughaibuni. Huku wanawake wakiwa ni theruthi mbili ya waathirika.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na wanawake wawili Bi Rami Hong na Bi Somely Mam ambao walitoa ushuhuda wa namna walivyopatwa kuuzwa wakiwa watoto wadogo na kufungiwa katika madanguro ya biashara ya ngono kwa zaidi ya miaka kumi hadi pale walitoroka.

Katika ushuhuda wao walioutoa kwa hisia kali na kwa nyakati tofauti wakati wa mkutano huo, wanawake hao wanaeleza kwamba, mtandao wa biashara ya binadamu ni mtandao mpana, wenye nguvu kubwa na unaotumia mbinu za kisasa kukamilisha malengo yao.

“ Hawa watu wamejipanga, wana nguvu sana, mimi nimeyaishi maisha ya utumwa wa ngono hadi pale nilipofanikiwa kutoroka. Kama hamta jipanga vizuri na kuwa na mipango madhubuti inayolingana na ya kwao mtaishia tu kuzungumza, hamtaweza kuivunja” anasema Bi Mam

Aidha wanawake hao wamewaeleza washiriki wa mkutano huo kwamba, ingawa wanaishukuru jumuia ya kimataifa na wanaharakati mbalimbali kwa kuamua kukabiliana vilivvyo na tatizo hilo. Hata hivyo wanasema itakuwa vizuri zaidi kama wao wenyewe waathirika wa biashara ya binadamu wakapewa fursa ya kuzungumzia athari walizopata na hivyo kutoa mapendekezo yanamnga gani wanataka wasaidiwe badala ya watu wengine kuwaamulia.

“Kazi ya kumrejesha muathiria wa biashara hii katika hali yake ya kawadia si kazi ya mwezi mmoja au miwili, ni kazi ya muda mrefu, inahitaji uvumilivu mkubwa na raslimali nyingi, kumtoa tu kule kwenye utumwa na kumpatia chakula au malazi hakutoshi. Sawa utampa ushauri na nasaha na baada ya hapo. Huyu anahitaji kujengewa uwezo, uwezo wa kuja kusimama mwenyewe ” anasisitiza. Bi. Hong

Baadhi ya wachangiaji wa mkutano huo, ikiwamo Tanzania licha ya kuelezea namna serikali zao zinazovyo kabiliana na tatizo hilo. Walikubalia na haja na umuhimu wa kushirikiana na kubwa zaidi ushiriki wa sekta binafsi.

Aidha baadhi ya wazungumzaji walishauri kushughulikiwa kwa tatizo la rushwa lililopo kati ya vyombo vya dola na hususani polisi na wafanyabiashara ya binadamu. Huku wengine wakivitaka vyombo vya habari kutangaza kwa nvugu zote na bila kuchoka pale watuhumiwa wa biashara hiyo wanapofikishwa mbele ya vyombo vya sheria na kuhukumiwa.

Aidha katika mkutano huo, Rais wa Baraza Kuu la 66 la Umoja wa Mataifa, pamoja na kuzungumzia tatizo la biashara ya binadamu. Yeye alitilia mkazo na kutoa wito kwa kila nchi kuchangia katika Mfuko wa Hiari wa kuwasaidia waathirika wa biashara ya utumwa.

Madhumuni ya Mfuko huo, ni kutoa misaada ya hali na mali kwa waathirika na kuazisha miradi ambayo inawajengea uwezo wa kuendesha maisha yao kwa kufanya shughuli za kuwaingizia kipato.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. UN na DUNIA KWA UJUMLA:

    La muhimu ni kurekebisha uchumi wa Dunia ndio vita hii itakwisha hasa kipengele cha 'TOFAUTI YA MAISHA BAINA YA WATU KATIKA JAMII' ****INCOME INEQUALITY IN THE SOCIETY****au KUTA ZA UMASIKINI MIONGONI MWA JAMII ZINAZOWATENGA WATU KWA TOFAUTI YA HALI NA KIPATO.

    Mfano Shirikisho la Ujerumani wakati wa Ukuta Mkuu wa Berlin watu walitengwa ki Siasa Ujerumani Magharibi na Ujerumani Mashariki huku kihali (kiuchumi wakitofautiana kwa mwanya mkubwa) , ili kutatua tatizo hilo waliamua kuuangusha Ukuta wa Berlin Novemba mwaka 1989 sawa ki Siasa walirekebisha lakini kihali bado KUTA ZILIENDELEA MIONGONI MWA JAMII, YAANI WALIOKUWA NAZO NA WASIOKUWA NAZO KTK JAMII AMBAYO SASA NI MOJA TU.

    Sasa baada ya kutatua tatizo la tofauti ya kipato miongoni mwa watu wa jamii Duniani ndio waje kwenye suala la HUMAN TRAFFICKING !

    ReplyDelete
  2. Binaadamu mmoja kumchukulia Binaadam mwenzie kama Biashara ni dalili za kukithiri kwa umasikini.

    MARA NYINGI HATA WANYAMA PORINI WALE WENYE NGUVU AU WAKUBWA WAKISHIKWA NA NJAA HUWACHUKULIA WADOGO KAMA RASILIMALI, Suluhisho la wanyama hawa ni kuhakikishiwa malisho ili waache kutumiana vibaya!

    VIVYO HIVYO KWA SISI BINAADAMU HILO LIPO NDIO KAMA HAPA SASA BIASHARA YA BINAADAMU KUUZANA WENYEWE KWA WENYEWE.

    Utatuzi wa tatizo la Biashara hii ni Umoja wa Mataifa kushughulikia zaidi kuutokomeza Umasikini ili kunusuru tabia hii.

    ReplyDelete
  3. Nikweli kabisa aliyechangia hapo mwanzo, watu wanachakarika walishe watoto na wajiendeleze kimaisha.

    Watu wenyewe kwa hiari yao wanaomba kuwa trafficked.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...