Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR) Dkt. Julius Massaga(kulia) akitoa ufafanuzi leo jijini Dar es salaam kuhusu chanjo ya satarani ya shingo ya kizazi kwa wanawake wakati wa semina na waandishi wa habari.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR) tawi la Mwanza Dkt. John Changalucha(kulia)akiongelea leo jijini Dar es salaam na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya utafiti wa mapokeo ya wananchi kuhusu chanjo ya saratani ya njia ya kizazi kwa wanawake . Kushoto ni Mtafiti Mkuu wa Utafiti wa Chanjo ya kuzuia saratani ya njia ya kizazi  wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR) tawi la Mwanza Dkt.Deborah Waston Jones. 
Mtafiti Mkuu wa Utafiti wa Chanjo ya kuzuia saratani ya njia ya kizazi  wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR) tawi la Mwanza Dkt.Deborah Waston Jones(kushoto) akiongelea leo jijini Dar es salaam na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya utafiti wa mapokeo ya wananchi kuhusu chanjo ya saratani ya njia ya kizazi kwa wanawake . Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR) tawi la Mwanza Dkt. John Changalucha(kulia).  Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es salam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. hongera watafiti wetu kwa kudeal na matatizo yanayowagusa wananchi

    ReplyDelete
  2. Hii ni habari njema.
    Naomba pia muangalie uwezekano wa kufanya research ya kungundua chanjo ya kansa ya kibofu cha mkojo maana inasumbua na kusababisha vifo vya akina baba wengi.

    ReplyDelete
  3. Hebu tupeni taarifa kuhusu hiyo chanjo:

    1. Jee inapatikana katika hospitali zote kuu (Regency, Mikocheni....)

    2. Jee mwanamke ye yote anaweza kupata hiyo chanjo?

    Tunaomba ufafanuzi kuhusu hilo tafadhali.

    ReplyDelete
  4. sio Deborah Waston Jones ni Deborah Watson Jones

    ReplyDelete
  5. Mdau hapo juu kansa ya kibofu cha mkojo ni tatizo sugu. Jamani tuache kuruka ukuta. Hii ni tatizo sasa, kizazi kitateketea.

    ReplyDelete
  6. Ok,kansa ya kibofu cha mkojo ni tatizo sugu,below are the contributing factors to the urinary bladder cancer,some of them are modifiable factors, watafiti wakiwa kazini, wanachi wajaribu ku modify some lifestyle issues.
    UROTHELIAL CANCER IS COMMON.
    -No single factor is identifiable in the majority of cases, but in others, there may be an association with.
    1,Cigarette smoking- increases risk 2fold!
    2,Occupational exposure to carcinogens widely used in rubber, cable, textile and printing industries.
    3,Some drugs like Aspirin and Cyclophosphamide.
    4,Endogenous carcinogens(keep fit and eat well to reduce this risk).
    5, Schistosomiasis (KICHOCHO).aka Bilharziasis.
    6,Urinary bladder stones.
    Wengi wanafikiri uvutaji sigara waleta kansa ya mapafu tu,think twice buddy, tena kwa bongo yetu kama huna uwezo wa kifedha, ukipata kansa ya kibofu(au yeyote ile), kwa kweli gharama za matibabu ni kubwa mno.
    Mungu ibariki Tanzania- Amen/Inshallah.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...