KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Nizar Khalfan (pichani kulia) aliyekuwa anacheza soka ya kulipwa Canada, amejiunga rasmi na `Mabingwa Watarajiwa’ wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu, Simba.
Habari za uhakika kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa, usajili wa mchezaji huyo umefanikishwa na mmoja wa wafadhili wa zamani wa klabu hiyo, Azim Dewji.
Dewji mwenyewe alipotafutwa kuzungumzia hilo, alikiri na kusema kuwa, aliombwa na uongozi wa Simba kufanikisha usajili wa mchezaji huyo na kwamba baada ya kufanikiwa, ameshamkabidhi Nizar kwa uongozi wa klabu.
“Kama Mwanasimba, nimetimiza wajibu wangu kama nilivyokuwa nimeombwa na uongozi. Nimeambiwa ataungana na wenzake kuanza mazoezi wakati wowote kuanzia Jumatatu (leo),” alisema na kuongeza kuwa, mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar na Moro United atakuwa na nafasi ya kuanza kuichezea Simba katika michuano ya kimataifa mwaka huu endapo itaingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Baada ya kuzing’oa ya Kiyovu ya Rwanda na Setif ya Algeria, wiki hii Simba itaishukia Al Ahly Shandy ya Sudan na kama ikifanikiwa kuvuka kiunzi hicho, itaingia katika raundi nyingine itakayoamua timu za kucheza Nane Bora Afrika.
Habari zaidi zinasema kuwa, Nizar leo atakabidhiwa rasmi jezi atakayoitumia akiwa Simba. Atakabidhiwa jezi hiyo muda mfupi kabla ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Moro United unaotarajiwa kuanza saa kumi alasiri.
Mmoja wa viongozi wa Simba ambaye hata hivyo hakuwa tayari kutajwa jina akisema si msemaji, alikiri kukamilika kwa taratibu za Nizar kutua Simba huku akiongeza kuwa, ataisaidia klabu hiyo katika michuano ya ligi na ile ya kimataifa kuanzia msimu ujao.
“Ni kweli, timu inazidi kuimarika. Kumpata staa wa kimataifa kama Nizar ni jambo la kujivunia, tunashukuru kwa juhudi zilizofanyika na hatimaye kumpata mchezaji huyu,” alisema.
Nizar ambaye Juni 21 mwaka huu atatimiza umri wa miaka 24, kabla ya kutua Simba aliichezea Philadelphia Union ya Ligi Kuu ya Marekani aliyodumu nayo kwa miezi mitatu tu baada ya kujiunga nayo akitokea Vancouver Whitecaps. Alikuwa Vancouver tangu Agosti 22, mwaka 2009 akitokea Moro United.
Katika soka ya ushindani, nyota huyo aliibukia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys mwaka 2004 na baadaye akajiunga na Mtibwa Sugar kabla ya kutimkia Kuwait kuichezea Al Tadamon ya huko msimu wa 2007-2008. Kutoka Tadamon alikwenda Lebanon na kuichezea Tadamon Sour ya huko na mwaka 2009 aliichezea Moro United.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Wachezaji wa Kibongo kweli sio mchezo,yaani amecheza Canada na Marekani halafu anaruid Bongo kuichezea Simba.Hapo kweli mtu unakuwa umelogwa.Bongo unarudi kufuata nini kucheza mpira,bongo kuna mpira gani wa maana.

    ReplyDelete
  2. wewe mtoto hivi akili inakutosha? wewe unatoka marekani unakuja kucheza bongo kweli WEWE HAMNAZO.

    tafuta trnsfar huko hyuko ukija huku basi tena wewe umekwisha

    ReplyDelete
  3. simba si mchezo bwana, wameweza hata kusajili mchezaji aliyechezea Canada & America!!.......haya jamani, YeboYebo mtatuweza kweli kwa usajili huu?

    ReplyDelete
  4. HAYA NJOO UJIMALIZE SASA KWENYE MPIRA WA RAMLI.YANI UNAKAA NJE UNACHEZA MPIRA UNASHINDWA KUTAFUTA TIMU UKABAKI HUKO UNARUDI UCHEZEE HAWA MACHIZI WA SIMBA NA YANGA?KWELI NYIE MMELOGWA,MKISHAKUMBUKA TU BANGI YA BONGO BASI MNACHANGANYIKIWA.HUKUWA UNAJUA KUWA MKATABA WAKO UNAISHA?ULIKUWA UNACHEZA TU HUJUI KESHO IKOJE?SI HERI UNGETAFUTA HATA TIMU YA DARAJA LA PILI HUKO KULIKO KWENDA KWA-WAUA VIPAJI SIMBA NA YANGA?HATA KAMA UMEKUMBUKA KIJITI CHA ARUSHA,MARA KUMI UNGESEMA UNARUDI UJIUNGE NA AZAM AU MTIBWA KULIKO HUKO UNAKOENDA.HUWA HAMJUI MFANYALO NADHANI ELIMU NDOGO NA PIA HAMNA WASHAURI WAZURI WALIO HURU, HATA KAMA MNAWASHAURI WANAKUWA WASHABIKI WA SIMBA NA YANGA AMBAO HAWAJALI FUTURE YENU.KARIBU BONGO TUHESABU AKIFUNGWA MTIBWA SIE TUKITOA DRAW TUMEPITA.

    ReplyDelete
  5. Nizar hakumalikza mkataba na Vancouver white caps ya Canada, bali walimtema kwenye timu. Baada ya hapo alichukuliwa na Philadelphia Union (ya marekani), ambayo nayo ilimtema kabla msimu wa ligi ya marekani kuanza. Kwa kifupi hakuweza kupata namba kwenye timu zote mbili kutokana na ushindani mkali hususan kwenye mid-field position.

    ReplyDelete
  6. Hayo ni maoni yako...acha mawazo finyu mdau, unadhani utautukuza ukoloni hadi lini! acha mawazo ya kitumwa!!!

    ReplyDelete
  7. Nadhani ni vema kumuomba mwenyewe hasa atueleze kilichomrudisha bongo kuliko kumhukumu bila kujua upande wake hasa nini kilichomtokea! Ila kwa mtazamo wa haraka haraka huenda sio jambo sahihi sana kurudi kwa mtazamo wa kuendeleza kipaji chake cha uchezaji wa mpira wa miguu. Tungependa atueleze zaidi kilichomsibu

    ReplyDelete
  8. i love all the comments,....man! Kalogwa

    ReplyDelete
  9. Pole Star wa Mpira!

    Moja kwa moja hadi Mchangani Bongo kwenye mipira ya Falaki, Makombe ya Maharage na Mbuzi.

    Bora angebaki hata kufua Jezi za Timu au kuwa Msaidizi wa Dakitari wa timu Canada au Marekani kwa majukumu kama kuchua misuli ya Wachezaji majeruhi!.

    ReplyDelete
  10. Wabongo msitie aibu, badala ya kumpa heko kijana ameamua kurudi nyumbani kwa ridhaa yake, mnampiga DONGO la macho, Ouch!!

    ReplyDelete
  11. Hakuna cha ajabu. Olivier Karekezi kacheza Ulaya na akina Henrik Larsson sasa yuko APR. Allan Wanga naye karudi AFC Leopards. Hizo timu mbili zote ni ndogo kuliko Simba. Msishangae pia kusikia mshahara atapewa sawa na ule aliopata Canada!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...