Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwapongeza wajumbe wa Tume hiyo baada ya kuapishwa rasmi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam leo.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, na Makamu wake wawili, Maalim Seif na Balozi Seif Idd, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na Viongozi wateule na wajumbe wa Tume hiyo baada ya kuapishwa rasmi. Tume hiyo inatarajia kuanza kazi rasmi Mei 01, mwaka huu. 
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Jaji Joseph Sinde Warioba, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya mchakato wa kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Mwantum Malale,  kuwa Mjumbe wa Tume ya mchakato wa kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Picha zaidi Bofya Hapa.Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Priiiiiiiii!!! haya kipenga hicho, wananchi tuchangamkie na tuache ushabiki utakuja tucost

    ReplyDelete
  2. KIPELE KIMEPATA WAKUNAJI KAZI KWAO

    ReplyDelete
  3. Pongezi Mheshimiwa Raisi kwa kazi nzuri uliyofanya. Kutokana na maoni ya wengi, hii kamati uliyo chagua ni team nzuri. Ina maana wananchi wana imani nayo. Kama hali ndio hii basi ni zawadi kubwa kwa taifa letu. Tuna imani hii kamati itakuwa makini na kufanya kazi yake wakiwa huru na kwa lengo la kuandaa katiba nzuri yenye manuafaa kwa taifa letu na watu wake na vizazi vijazo. Ubinafsi uwekwe pembeni na hii timu ifanye kazi kwa ushirikiano mkubwa na kwa moyo mmoja kwa manufaa ya taifa letu, amina.

    ReplyDelete
  4. hayawihayawi sasa yamekuwa, well done my dear leader JK i salute you SIR.

    ReplyDelete
  5. Watanzania wasiwe wepesi sana wa kukurupuka na kuanza kumwaga sifa.Tusubiri tuone nini Tume hii itafanya ndipo tuanze kutoa tafsiri na maono yetu kuhusu ubora wa Tume hii ya Katiba.Same faces time and again si jambo zuri sana,lakini mazoea ndivyo yalivyo.Mimi siwezi kutoa comments zangu kwa sasa mpaka nitakapo ona utendaji halisi wa tume katika kuitafuta Katiba Mpya,narudia Katiba Mpya,na siyo Marekebisho ya Katiba iliyopo sasa.Katiba iliyopo sasa itumike kama "Malighafi tu"katika kuipata Katiba Mpya.Na Katiba iliyopo sasa bado itaendelea kuwepo hadi pale hiyo Mpya itakapo patikana.Isipopatikana kwa ridhaa ya watanzania walio wengi,basi ile iliyopo sasa itaendelea kutumika mpaka hapo mpya itakap patikana.Tusikimbilie kuisifu Tume kwa kuangalia sura za watu au majina tu ya wajumbe.Its the Contents that matters,not the packaging! Mambo critical katika kuitafuta Katiba Mpya ni matatu:kwanza kabisa,suala la kuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi yenye muundo ulio wazi na itakayo kuwa na watumishi wake wenyewe nchi nzima katika kila wilaya ambao watafanya kazi bila kuogopa shinikizo za viongozi wa serikali katika maeneo yao ya kazi;pili,suala la kupunguza Madaraka ya Rais wa nchi,ikiwa ni pamoja na kutafuta mfumo bora zaidi wa kumpata Kiongozi wa Serikali(Head of Government)ambaye ndiye atakayepigiwa kura na wananchi katika kila uchaguzi mkuu,na jinsi ya kumpata Kiongozi wa Nchi (Head of State) na mustakabali wa mfumo mzima wa utawala nchini;tatu,mipaka ya madaraka ya Mihimili Mikuu Mitatu ya Dola,Bunge,Mahakama,na Serikali au Utawala,pamoja na nafasi ya Vyombo Huru vya Habari kama jicho la wananchi katika kufuatilia kwa karibu na kuratibu wa utendaji wa mihimili yote hiyo mitatu katika kutoa na kutenda haki kwa raia wake wote bila ya ubaguzi wowote.Hayo yakifanyika kwa umakini mkubwa,mengine yote kuhusu Haki za Raia (bill of rights)na jinsi wapiga kura watakavyo kuwa na uwezo wa kuiadabisha na kuidhibiti serikali walioiweka madarakani kwa ridhaa yao,yatafanyika bila ya kikwazo chochote.Huu sio wakati wa kuelimisha watu kuhusu Katiba iliyopo sasa.Ni wakati wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu aina ya Katiba watakayoitaka sasa kulingana na mazingira ya kisiasa na kiuchumi yaliyopo sasa.Wakati hilo likifanyika,elimu kuhusu Katiba iliyopo sasa itakwenda sambamba na hilo.God Bless!If this noble opportunity is allowed to go waste and rot,those in power now will live to regret!Tusifanye mzaha na fursa hii muhimu iliyojitokeza kwa ustawi wa mustakabali wa nchi na Taifa letu!

    ReplyDelete
  6. Jambo jingine kwa maoni yangu binafsi ni kwamba,Tume hii ya Katiba iliyo teuliwa ina Makundi Makubwa Matatu ya Kimtazamo na Msimamo (three schools of thought),nazo ni,kuna kundi la "Wahafidhina/Conservatives)ambalo halitopenda kuona mabadiliko makubwa sana katiba Katiba iliyopo sasa yanafanyika au yanatokea.Hili ni kundi ambalo lilinufaika sana na kuwepo kwa Katiba ilyopo sasa na zilizokuwepo huko nyuma.Kama ni Maboresho,basi ni yale tu ambayo hayata hatarisha "Status Quo" ulaji wa wale walio otesha mizizi katika utawala wa nchi yetu;kundi la pili,ni lile la "Wapenda Mageuzi/Mabadiliko (Reformists)katika Katiba iliyopo sasa na wangependa iundwe Katiba Mpya kabisa ambayo itazingatia yote mazuri na muhimu yaliyomo katika Katiba iliyopo sasa,na kuachana na vipengele vyote kandamizi vilivyopo katika Katiba ya sasa,Katiba itakayo kidhi kiu ya mahitaji ya mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa;kundi la tatu,ni lile la "Wenye Msimamo kuhusu Maslahi ya Zanzibar (Zanzibar school of thought)ambalo lingependa Zanzibar ipewe uhuru zaidi wa kujiamulia mambo yake yenyewe bila ya kubanwa na mahusiano baina yake na Bara,nk nk.Kwa muhtasari sana hiyo ndiyo Mitazamo Mitatu (three schools of thought)iliyopo miongoni mwa wajumbe wa Tume ya Katiba iliyoteuliwa hivi karibuni.Maoni ya wananchi yatakusanywa nchi nzima,lakini utakuwepo "Mvutano Mkali"baina ya mitazamo hiyo mitatu miongoni mwa wajumbe wa Tume,na kazi kubwa itakuwa kujaribu kutafuta uwiano (Balanced Perception)wa maono miongoni mwa wajumbe wa Tume.Kwa hiyo,watanzania wasije wakalala usingizi wakitarajia kwamba tume hiyo itawatayarishia KATIBA WALIO IKUSUDIA bila ya ushiriki wao.Lazima wafuatilie kila hatua itakayo fikiwa katika kukusanya mawazo na kutoa tahadhari pale ikapo bidi.Siyo Tume ya "Malaika",waliomo ni binadamu kama sisi wengine wote.Kila Mtanzania awajibike kikamilifu katika kuhakikisha kwamba zoezi hili la kutayarisha Katiba Mpya "halitekwi Nyara"na wajanja wachache kwa maslahi yao binafsi.Katiba Mbovu haitakubalika kabisa na mtanzania yoyote,hilo lazima lieleweke mapema.Lets not waste Time and Resources.Katiba nzuri na makini isipopatikana sasa,upo wakati lazima itakuja patikana,na sio lazima iwe leo au kesho.Lets all be serious about this.Tuache ile tabia ya "Uswahili"kugeuza wengine "hawajui kinacho endelea".Tukiweka pembeni Ubinafsi na kutanguliza mbele Uzalendo na Utaifa,kila mtu akawa mkweli akaacha Unafiki, kila kitu kitakwenda sawia na Katiba nzuri itapatikana katika wakati ulikusudiwa.Tumtangulize Mungu katika kila hatua ya zoezi hili gumu lakini rahisi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...