Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia Katibu mkuu kiongozi mstaafu Mzee Timothy Apiyo wakati wa hafla ya sherehe za miaka 48 ya Muungano iliyofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Monsinyori Julian Kangalawe wakati wa halfa ya muungano ikulu jana jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkurugenzi mkuu wa PPF Wiliam Eriyo wakati wa hafla ya sherehe ya miaka 48 ya Muungano iliyofanyika katika viwanja vya ikulu jana usiku
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mmoja wa Wazee waliohudhuria hafla ya sherehe za Muungano iliyofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanasanii kutoka katika Chuo Cha mafunzo ya Polisi, Moshi wakati wa hafla ya sherehe za miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanasanii kutoka katika kikundi cha JKT Oljoro, Arusha wakati wa hafla ya sherehe za miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.Picha na Freddy Maro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. hapo ndio tunaona kwa jinsi gani huu muungano ni wa Tanganyika, nyinyi watanganyika ndio munaosherehekea muungano kwa sababu ndio munaoutaka. sasa tunawambia Wazanzibari muungano hatuutaki na mara hii ama zenu ama zetu

    ReplyDelete
  2. Wewe namba moja nje ya Muungano hakuna cha "sisi Wazanzibari"nje ya muungano mtaparaganyika tu huko.Mifano ipo mingi sina haja ya kuitaja hapa.Samahani kama nitakuwa nimekuongezea hasira..Muungano udumu udumu hadi milele.Nitumie email nikupe sababu zangu za kuupenda Muungano na wewe unipe sababu zako za kuuchukia,humu hapatoshi-fridokazadi@gmail.com

    David V

    ReplyDelete
  3. David V, huyu mshamba anayekataa muungano, mbona hujampa vipande vyake ?? wazanzibari wote tunautaka muungano kasoro yeye tu, sikiliza bwana ,wewe kama kwenu ni Yemen,mbona huondoki ???? nenda kale vumbi huko tuache sisi tuishi, maisha yenyewe ni mafupi kwa hiyo usituchanganye na kutuvuruga,maisha ya kuishi kwenye kambi za wakimbizi-tunayaona kwenye TV tu,kwa hiyo hatutaki tuvurugane kisha tukimbie na kuwa wageni wa UN. wewe nenda kwenu .

    ReplyDelete
  4. mimi nimependa hiyo picha ya kwanza

    ReplyDelete
  5. acha mikwara dogo..sie twautaka sana wazanzibar halisi

    ReplyDelete
  6. VIPANDE VYA MOJA KWA MOJA KWA WAPINGA MUUNGANO:

    *****DIRECT FAX*****

    1-DUNIA INATAFUTA KUUNGANA ILI KUKIDHI MAHITAJI NA KUTATUA MATATIZO KWA PAMOJA, MIFANO YA MASHIRIKISHO, NI UMOJA WAULAYA (EUROPEAN UNION), JUMUIYA YA AFRIKA YA MAGHARIBI (ECOWAS), NA SASA TUNA JUMUIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI IKIWEMO HIYO HIYO UNGUJA NA PEMBA ALIYOPO HUYO MPINGA MUUNGANO WA KWANZA HAPO JUU.


    2-ATASEMA ANAVUNJA MUUNGANO ILI AENDE KWA MWARABU HUKO (YEMENI) AU (OMANI), WAKATI HUKO NDIO HAKUKALIKI KUNA 'ARAB SPRING' MAPINDUZI YAMEWAKA MOTO NI MAANDAMANO KILA KUKIKCHA WANABURUZANA YAO YAMEWASHINDA HIVYO ELEWA HAWANA HAJA YA UNGUJA NA PEMBA!

    SASA HATUJUI HUYO MPINGA MUUNGANO ATAENDESHA VIPI NCHI YAKE AKISHAVUNJA MUUNGANO?

    3-ZANZIBAR NA PEMBA ZINANUFAIKA ZAIDI NA MUUNGANO YEYE KWA VILE NI MVUVI WA SAMAKI HILI HALIJUI , WANAOLIJUA HILI NI VIONGOZI WA JUU PAMOJA NA WAZANZIBARI WAELEWA NA WALIOSOMA.

    4-WENGI WA WAPINGA MUUNGANO NI 'LUPMPEN PROLETARIAT' WATU WASIOSOMA, WALIOJIPOTEZEA MAISHA KWA UJINGA WAO, NA WASIOKUWA WAELEWA KAMA HUYO MJINGA MPINGA MUUNGANO, PANA TOFAUTI KUBWA KATI YA MTU ALIYESOMA NA ASIYE SOMA , ZAIDI YA HAPO PANA TOFAUTI KATI YA MWELEWA (HATA AKIWA HAJASOMA) NA MJINGA !

    5-PANA WAZANZIBARI KADHAA WAELEWA SAANA NA HAWA NDIO WATU MUHIMU SANA AMBAO WATAWEZESHA MAMBO KUWA, LAKINI SIO HUYO MJINGA HAPO MPINGA MUUNGANO.

    6-UJIO WA AFRIKA YA MASHARIKI TULIO NAO SASA NDIO UTAIPATIA ZAIDI ZANZIBARI FAIDA KWA KUWEPO KTK MUUNGANO KULIKO ILIVYOKUWA KABLA NA HIVYO KUVUNJA MUUNGANO NI KUWA ZANZIBARI ITAPOTEZA SANA, *****(((((NDIO MAANA MAALIM SEIF ALIKUWA NI MPINGA MUUNGANO MKUBWA LAKINI KWA KUWA KTK HAO WAZANZIBARI WAELEWA WACHACHE PIA MAALIM SEIF YUPO NA NDIO MAANA HIVI SASA HAONGELEI KUHUSU KUVUNJA MUUNGANO NDIO KWANZA ANATAKA KUDUMISHA UKARIBU NA MSETO WA KISERIKALI ILI KUIPATIA ZANZIBARI FAIDA KWA KUINGIA KATIKA JUMUIA YA AFRIKA YA MASHARIKI IKIWA NI SEHEMU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA)))))*****.

    7-KAMA ZANZIBARI INGEFANIKIWA HAPO NYUMA KUKURUPUKA NA KUUVUNJA MUUNGANO NA HIVI SASA INGEKUWA INAJUTA SAANA KWA KUWA FAIDA YA KISIASA NA KIUCHUMI YA JUMUIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI INGEIKOSA.

    8-FAIDA ZA JUMUIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI,
    (i)Uhamishaji wa Mitaji na kukuza mzunguko wa kiuchumi fedha na biashara, wewe utauza bidha zako ktk nchi 5 (Tanzania, Kenya,Rwanda, Burundi na Uganda)bila vizuizi na Kodi kubwa na vikwazo za vizuizi kama unavyopata kupeleka bisahara au kuleta biashara kutoka huko unakotegema Arabuni.

    (ii)Wewe Mpinga Muungano huna kazi na mtaji huko Zanzibari utaweza kupata kazi na mtaji kwa kwenda nchi zingine za Jumuia (Kenya,Uganda,Burundi na Rwanda)bila vizuizi kama unavyopata ukitaka kwenda Oman na Yemen kwa Waarabu wako hao.

    (iii)Wewe Mpinga Muungano utapata nafasi ya kujifunza Ujuzi kutoka nchi zingine 5 kama inavyoonyesha kuwa akili yako ni finyu kabisa hivyo utanufaika sana.

    Na faida nyingine nyingi tu.

    9-KWA KUWA KTK JUMUIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI UTAJIHAKIKISHIA AMANI ZAIDI KULIKO ILIVYO SASA, KWA KUWA KWA USIMAMIZI MAKINI WA SERIKALI ZA NCHI 5 NA UELEWANO KITU KAMA 'VITA' HUTAKISIKIA TENA MAISHANI.

    10-LENGO LA VIONGOZI WA SERIKALI YA MSETO ZANZIBARI ILIYOUNDWA KWA BUSARA ZA HALI YA JUU KABISA NA C.U.F NA C.C.M NI KUKUHAKIKISHIA WEWE MPINGA MUUNGANO UNAPATIWA MANUFAA ZAIDI NA ZAIDI KAMA UNAVYOOONA KTK JUMUIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI NA PIA IKIWEPO JAMUHURI YA MJUUNGANO WA TANZANIA.

    WOTE WAPINGA MUUNGANO:

    MZINGATIE MAMBO HAYA 10 ILI MPATE UELEWA.

    ReplyDelete
  7. Mdau wa Kwanza Anonymous wa Fri Apr 27, 02:13:00 PM 2012

    ''....Muungano ni kwa faida ya Tanganyika tu''

    Wengi wa Wapinga Muungano ni wenye akili finyu,,,mnaweza kuzaliwa wengi ktk ukoo wenu lakini hamuwezi kuwa wote na akili nzuri au wote mkawa na akili sawa,,,na ndio maana katika Wazanzibari wapo wasio na akili na pia wapo wenye akili.

    Mfano matatizo yako binafsi inaweza kuwa wewe mwenyewe ndio sababu ya hali duni uliyo nayo sasa badala ya kuulalamikia ukoo wako au ndugu wa familia yako.

    WEWE MLALAMIKAJI UPO NJE YA UTAWALA NDIO MAANA HUJUI UZITO NA MAJUKUMU YA UTAWALA.

    KAMA UNGEPEWA WEWE UTAWALE UKAONA MZIGO WA MAJUKUMU NA WEWE PIA USINGEPINGA MUUNGANO.

    KAMA ZANZIBARI INGEJITENGA AU KUVUNJA MUUNGANO MAPEMA, SASA HIVI INGEKUWA INAJUTA KWA SABABU UJIO WA JUMUIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI UTAINUFAISHA ZAIDI ZANZIBARI KULIKO ILIVYOKUWA AWALI.

    NCHI ZA AFRIKA YA MASHARIKI ZIMEBARIKIWA KWA MAJAALIWA NA MALI TOFAUTI TOFAUTI KWA UCHACHE:

    -UGANDA:Wamegundua mafuta (Oil)yanaanza kuchimbwa mwaka 2015

    -TANZANIA:Inayo Uranium,Gas,Metal,Coal,Gold zaidi,Diamonds ,Mafuta yatakuwepo muda si mrefu.

    -KENYA:Ina masoko ya Bidhaa, Viwanda na Huduma za Biashara,

    -BURUNDI:Ina kahawa na masoko ya bidhaa,

    -RWANDA:Ina Bouxite(bati)na Coltan madini ya elektroniki kwa simu na kimputa.

    -SUDANI YA KUSINI:Ina mafuta (Oil)mengi sana ,Kwa sasa ni mwanachama Mwangalizi na muda si mrefu itaingia uanachama kamili.

    HUKU MWARABU MNAYEMTEGEMEA AKIWA ANAHANGAIKA NA MAPINDUZI 'ARAB SPRING' NA MAANDAMANO NA VURUGU KILA KUKICHA HANA MAHITAJI NA UNGUJA NA PEMBA KWA KUWA YA KWAKE YANAMSHINDA YENU ATAYABEBA VIPI?

    KWINGINEKO ULAYA NA MAREKANI WAMESHAFILISIKA KIFEDHA NA KIUCHUMI, KAMA UNAVYOONA WANA MASHARITI YA MISAADA YA AJABU AJABU KWA SASA.

    KWA HIYO:
    VIONGOZI WAKO WENYE AKILI NYINGI, BUSARA SANA NA HEKIMA KAMA MAALIM SEIF WAMEONA NI WAZI KABISA KUWA KATIKA MUUNGANO NI FAIDA ZAIDI KWA KUWA ZANZIBARI ITANUFAIKA ZAIDI NA HIZO RASILIMALI ZA HIZO NCHI ZA AFRIKA YA MASHARIKI NA TANZANIA KULIKO KUTOKA KWA NCHI ZA KIARABU:

    MAALIM SEIF ZAMANI ALIKUWA NI MPINGA MUUNGANO MKUBWA KAMA WEWE LAKINI KWA KUWA YEYE ANA AKILI ZAIDI YAKO UNAONA SASA SIKU HIZI SIO MPINGA MUUNGANO TENA BALI NI MDUMISHA MUUNGANO!

    MAALIM SEIF AKIWA BEGA KWA BEGA NA SERIKALI PAMOJA NA WAZANZIBARI WENGINE SERIKALINI WENYE AKILI NZURI ANATAFUTA NJIA RAHISI YA KUENDESHA SERIKALI NA KUTOA TIJA KWAKO WEWE MLALAMIKAJI HAPA.

    HIVYO KWA TAARIFA YAKO KUTOKANA NA MAELEZO HAYO HAPO JUU NI DHAHIRI KUWA MUUNGANO HAUTAVUNJIKA NG'O UTAKUFA WEWE TU MUUNGANO UTAUACHA KWA FAIDA YA VIZAZI VYENYE AKILI VIJAVYO.

    ReplyDelete
  8. Mdau David V.

    Huyo Mjinga Mpinga Muungano mfuundishe Direct humu kwenye blog kwa yale yete unayoyajua yanaweza kumsaidia yeye na Wajinga wenzake wapinga Muungano.

    Angalia Wazungu wanahangaika kutafuta kuungana kwa Umoja wa Ulaya EU yeye huyu ndugu yetu anawaza Utengano, kweli ana akili?

    Mfano mwingjne wa Muungano ni Hii Afika ya Mashariki inayoelekea kuzipa Serikali wanachama unafuu wa kuyafikia malengo ya kiutawala, kama Zanzibari ingejitenga hapo kabla ingekuwa imepata hasara kubwa saana na ingelazimika kujiunga na Muungano huu mwingine (afrika ya Mashariki) zaidi ya wa awali ambako ingeikuta tena Tanganyika!!!,,,sasa je kuvunja Muungano ni suluhisho au ndio pingamizi kwenu?.

    Na kwa mahitaji makubwa na majukumu ya Kiutawala yanayoongezeka siku hadi siku Zanzibari ingejikuta inauhitaji Muungano zaidi kuliko hapo kabla, angalia mlikuwa mnamtegemea Mwarabu hivi sasa Mwarabu anamatatizo kwake ana mapindizi 'Arab Springs' na amefilisika kwa vile Uchumi wake wa Mafuta unategemea nchi za Magharibi ambazo nazo zina matatizo ya kifedha na Kiuchumi,,,elewa kuwa Matatizo ya Kijamii kama Fedha na Uchumi yana maambukizi kama yalivyo maradhi, nchi unazoshirikiana nazo zikiimarika na wewe unaimarika vivyo hivyo zikiyumba na wewe unayumba.

    Mtikisiko wa Kifedha na Kiuchumi ktk Masoko ya Hisa na Mitaji Nchi za Magharibi inaathiri nchi za Kiarabu ambazo zinauza mafuta na kumiliki hizo hisa ktk Masoko hayo.

    Kulingana na hali halisi ilivyo na mwenendo halisi wa Dunia inavyokwenda...NI DHAHIRI KAMA MNGEKURUPUAKA NA MNGEVUNJA MUUNGANO HAPO KABLA MNGEKWAMA NA MNGEUMBUKA SANA!

    BORA MLIVYO CHELEWA KUUVUNJA MUUNGANO NDIO IMEKUWA SALAMA YENU,,,INGEKULA KWENU,,,!!! NA MAALIM SEIF NA WENZAKE SERIKALINI WAMELIONA HILO.

    MPINGA MUUNGANO ELIMU YAKO NI NDOGO HUWEZI ELEWA TUKIENDA KWA KINA ZAIDI, ELEWA KUWA VIONGOZI WAKO WAPO SAHIHI KUENDELEA KUUNGA MKONO MUUNGANO KWA FAIDA YAKO WEWE.

    ReplyDelete
  9. Anonymous wa Fri Apr 27, 02:13:00 PM 2012

    ''.....hapo ndio tunaona kwa jinsi gani huu muungano ni wa Tanganyika, ......''

    Wewe Mjinga nchi yako unayodai yenyewe masikini inamiliki samaki watatu (3) tena samaki tasa (wasiozaa), na kumiliki gunia moja (1) la karafuu tena iliyokuwa kiwango cha chini ukilinganisha na wazalishaji wengine Duniani kama Sri Lanka,India na Thailand.

    Huku umuliki huo huo wa samaki watatu (3), na gunia moja (1) la karafuu mpate uwezo wa kuendesha Serikali bila msaada wa Kifedha kutoka bara?,,,mtaweza?

    Ninyi Wazanzibari ndio mnaoinyonya Bara kwa kuwa hamna uwezo wa kuimudu kuiendesha Serikali yenu bila nguvu za Bara!

    ReplyDelete
  10. Zanzibari hamsherehekei Muungano kwa vile mnajua ni wazi kuwa mpo tegemezi kwa Bara juu ya Mzigo wa kuiendesha Serikali yenu na mara zote mtu mzima ameumbwa na haya hasa pale anaposaidiwa kupita kiasi!

    ReplyDelete
  11. Hakuna sherehe saana za Muungano kwenu kwa vile mmetahayari kwa kufikiri kuuvunja Muungano ndio ingekuwa suluhisho kumbe mambo ni kuwa mnauhitaji zaidi huo huo Muungano mliokuwa ukiubeza na kuudharau hapo awali!

    Habari hizi na ukweli huu muulizeni Maalim Seif Shariff Hamad yeye alikuwa mpinga Muungano mkubwa na sasa amekuwa ni Muunga mkono Muungano mkubwa baada ya kuona faida zake, yeye atawaelekeza zaidi.

    ReplyDelete
  12. Muungano umetusaidi mambo mengi ila ni watu wachache kwa manufaaa yao haswa watu wenye ubinasi wa madaraka kwa kuona kuwa kukiwa hakuna muungano ni rahisi wao kuwa viongozi wa muda mrefuu, kwa watu wa zanzibar ni wengi wanataka muungano na kama wewe hutaki basi baki zenji usije tanganyika ukaleta chuki yako kama una mawazo ya akili sema hivi muungano hundumu ila kama kuna kasoro kwenye katiba basi tufanyie mabadiliko kwa faida ya yote sio kwa watanganyika au wazanzibar. kila mahali wanataka muungano hata nchini ya uropeani tizama marekani ina state kama 50 na kitu .. kuhusu east africa pia tuna na muungano ila tanzania tuna desturi ya kudhamini mila na desturi zetu kama vianja ni kila kabila wanaaachia vizazi vyao kwa hiyo kuhusu swala ya ardhi kuwa huru kwa east africa wote mie sikupali nao...bye

    ReplyDelete
  13. Mdau Anonymous wa Sat Apr 28, 12:43:00 PM 2012

    Tumeshakubaliana ya kuwa uwepo ktk Jumuia ya Afrika ya Mashariki sio kwamba kila Azimio likija ni kukubali na kulipitisha, HAPANA!:

    Kila nchi mwanachama ina Sera zake ktk mambo mbali mbali na kuwa kila mwanachama ana saini lile analojua halitawagharimu watu wake na ana saini lile analojua litawanufaisha watu wake.

    SERA YA ARDHI:
    Kila nchi mwanachama ana Sera yake ya ardhi kulingana na Katiba yake na halazimishwi au kushinikizwa kutoa ardhi yake.

    TANZANIA: Tulisha kataa na ardhi yetu.

    KENYA: Katiba yao mpya inawamilikisha wa Kenya ardhi yao.

    RWANDA: Wanao mpango wao wa kuitumia ardhi na maelekezo mapya juu ya sera ya ardhi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...