Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumpokea katika uwanja wa karume Pemba alipowasili kisiwani humo kwa ziara maalum kuangalia maendeleo katika sekta mbali mbali za kijamii.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mtoto Suleiman Shaaban Juma,pamoja na wanachama wa Kampuni ya Mkipi Miliki Tungamaa,kuzindua Mradi wa uzalishaji wa sabuni kwa kutumia mashine maalum ya Mkipi Miliki,leo akiwa katika ziara kisiwani Pemba,kuangalia maendeleo ya jamii.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu George M.Buchwafwe, wakati alipoangalia Sabuni iliyotengenezwa katika kampuni ya Mkipi Miliki Tungamaa,ambayo inayozalisha sabuni kwa kutumia mashine maalum,alipokuwa katika ziara ya kutembelea maendeleo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi wa Mkipi Miliki Tungamaa, baada ya kuzindua rasmi uzalishaji wa sabuni kwa kutumia mashine maalum ya kampuni ya Mkipi Miliki,alipokuwa katika ziara ya kutembelea maendeleo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Baadhi ya watendaji wa Ofisi mbali mbali za Taasisi za serikali za Mkoa wa Kaskazini Pemba,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na watendaji hao,wakati alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo katika sekta mbali mbali za Mkoa wa kaskazini Pemba,katika ukumbi wa Jamhuri Hall Wete Pemba.Picha na Ramadhan Othman,Pemba.
Kaka braza Ras Makunja namuona kwa mbali!
ReplyDelete