Mwanamuziki Rebbeca Malope akiwa na baadhi ya wanamuziki wenzake wa nyimbo za injili waliowasili jioni ya leo sambamba na wenyeji wao,Bw.Alex Msama akiwa na Mkewe (wa tatu kulia).WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ndiye atakuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Kiingilio katika tamasha la mwaka huu kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh. 2,000 kwa watoto, sh. 5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh. 10,000.
Pichani kati ni Mwanamuziki wa nyimbo za Injili kutoka nchini Afrika Kusini,Rebbeca Malope akizungumza na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere,mara baada ya kuwasili jioni ya leo,jijini Dar,kulia ni Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex Msama ambaye ndiye muandaaji wa tamasha la pasaka linalotarajiwa kufanyika Uwanja wa Taifa hapo siku ya Jumapili jijini Dar.


Mbali na Dar es Salaam, tamasha la Pasaka pia litafanyika mjini Dodoma Aprili 9 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri ambayo ni Jumatatu ya Pasaka.Habari zaidi Bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ndugu msama,vp mtoto mdogo huyo unamuweka mbele ya kamera kama hivyo..au hujui kama flash za kamera zina madhara?

    ReplyDelete
  2. KARIBU TANZANIA REBECCA MALOPE, QUEEN OF GOSPEL MUSIC.
    Wasanii wa Gospel jifunzeni kutoka kwa huyu sister mtafanikiwa sana.
    Huyu dada yuko simple na sirious katika kazi yake, na hujichanganya na watu wote bila kujali dini, rangi nk.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...