Timu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam,leo imefanikiwa kusonga mbeke kwa hatua nyingine katika masindano ya Kombe la Shirikisho.Timu hiyo ambayo ilikuwa imejitupa dimbani jioni ya leo huko nchini Algeria kucheza na timu ya Es Satif ya nchini humo ambapo matokeo ya mchezo huo (Es Satif 3 - 1 Simba SC) ndio yameipa nafasi ya kusonga mbele timu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam.
Timu Simba imeweza kusonga mbele baada ya kupata bao la ugenini lililotiwa kimiani na Mshambuliaji Machachari wa Simba,Emmanuel Okwi (dk 91) wakati hapo awali Simba iliifunga timu ya Es Satif bao 2 - 0 nnyumbani.
Ankal acha unazi, mpaka useme Simba yasonga kwa mbinde?!!!!!!!!!!!!! toa pongezi tu bwana
ReplyDeletehivi kusonga kwa mbiiindee ndo nini?
ReplyDeleteSafi wana simba.
ReplyDeleteNILIKUTANA NA MCHAWI WA SOKA HUKU ALGERIA AKANIAMBIA IWAPO SIMBA WATAVAA JEZI NYEKUNDU °ROUGE° WATASHINDA ILA SIFIKIRII KAMA WATAIUNGA SETIF KAMA VILE DAR ES SALAAM ILA WATAPITA HII HATUA; DUUU nilisubriii kisha nikta tamaa baada ya kupigwa 3 lakini dk 91 nilishika simu nikamteli kwa kiarabu SAHA ya lkhaj saha yaakhuuya ILS SON GAGNEEEEEEEEE VIVE LE LION.WACHAWI WA SOKA BWANAAAA
ReplyDeleteHongereni simba. lakini nawaombeni next games muwe mnashinda magoli mengi nyumbani ili mkienda ugenini hali isiwe mbaya kiivyo. Hongereni sana cha msingi mmepita. Haijalishi ni kwa staili gani. cha msingi ni kusonga mbele kimahesabu.
ReplyDeleteMichuzi acha kinyongo, kwa mbiindee!!!??? Huo ulikuwa mpango mkakati wa Mnyama, kuwaacha wapate mabao yao matatu ile warelax then tustrike dakika za mwisho kupata bao moja tu, mpango umefanikiwa, Mnyama anatisha!!!! Yanga, dua la kuku halimpati mwewe kamwe.
ReplyDeleteKwanza niwapongeze lunyasi chini ya usimamizi thabiti wa Aden Rage na ujumbe mzito uliotuwakilisha Aljazaair. (hivyo ndivyo waarabu wanavyoiita nchi yao). Pili huyu mdau hapo juu lugha yake imenichefua kidogo. Neno "haijalishi" halimo katika msamiati wetu, mmelitoa wapi? Ingefaa sana kama wale ambao Kiswahili hawakutoka nacho vijijini wakachukua masomo ya muda mfupi ya lugha hii ili kuboresha uwezo wao wa kuiandika na kuizungumza. Na tatizo hili limetelezea hata katika filamu, matangazo ya redio na magazeti. Na matokeo yake badala ya vyombo hivi kusaidia kueneza lugha vinaipotosha. Mdau unaehusika jiunge na darasa la lugha. Ni ushauri tu. Mdau ukerewe
ReplyDeleteSimba bwana!!!!!!!!!!
ReplyDeleteRaha tupu jamani.Wengine mlie tu.