TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH: KUWATANGAZIA WADAU KUHUSU “PUBLIC HEARING” JUMATATU TAREHE 02 APRILI, 2012

Ofisi ya Bunge kupitia Kamati yake ya Viwanda na Biashara inaendelea kutekeleza majukumu yake katika kipindi hiki cha Mikutano ya Kamati za Bunge inayoendelea katika Ofisi ndogo za Bunge, Dar es Salaam. Hii ni kwa mujibu wa Kanunui za Kudumu za Bunge, Nyongeza ya Nane (9) (1) Toleo la 2007.

Mojawapo ya shughuli zinazofanyika wakati wa Vikao hivi na kamati hii ni kujadili Muswada wa Marekebisho ya Sheria za Biashara (The Business Laws (Miscellaneous Amendments) ACT, 2011 unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni katika Mkutano ujao. Ili kukidhi masharti ya Kanuni ya 84(2), ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Mwaka 2007, Kamati imepanga kusikiliza na kupokea Maoni ya Wadau katika Muswada huu (Public Hearing) tarehe 02/04/2012 kuanzia saa 3 Asubuhi, katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam. 

Wadau wote wanakaribishwa kuja kushiriki kutoa maoni yao kwa lengo la kuboresha Muswada huu kabla ya kupita katika hatua zake zote na kuwa sheria kamili baada ya kupitishwa na Bunge.

Wadau wote watakao sikia mwaliko huu kupitia vyombo vya Habari, wawaarifu na wengine kwa lengo la kuja kutoa maoni yao ili kuboresha Muswada huu wa Marekebisho ya Sheria za Biashara (The Business Laws (Miscellaneous Amendments) ACT, 2011.

Imetolewa na
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
Ofisi za Bunge
Dar es Salaam
31 Machi, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ankal si ungeuweka huo mswada hapa ili watu waupitie kwanza na wapate kuandaa mawazo yao kwa ajili ya kuchangia katika mjadala huo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...