Tanzania imeshinda katika michuano ya kila mwaka ya soka ya The Football4Hope-United Cup 2012 iliyodhaminiwa na SABMiller katika uwanja wa Thayagaraj Sports Complex jijini New Delhi, India. Jumla ya timu 14 zilishiriki mwaka huu, wakiwemo mabingwa wa mwaka jana, UN Organisations. Timu zingine zilikuwa Team India, Hope Team, Balozi za Denmark, China, Spain, Misri, Saudi Arabia, Indonesia, Uholanzi, Israel, Botswana na Tanzania.
Katika fainali Tanzania waliibwaga Botswana kwa bao 2-1.
Mechi za awali na matokeo za Tanzania ni kama ifuatavyo:
Denmark 0-11 Tanzania
France 0-4 Tanzania
India 0-2 Tanzania
Israel 1-7 Tanzania
Hope1-5 Tanzania
--------------------------------
Spain 0-2 Tanzania
China 1-6 Tanzania
India 0-1 Tanzania
--------------------------------
Botswana 1-2 Tanzania
Vijana wa Kitanzania wakifurahia ushindi wao kwa staili tofauti
Hapo ni Full kizazi kipya cha taifa stars
ReplyDeleteikiwa taifa stars itakuwa inasaka wachezaji wenye vipaji vya ukweli kutoka sehemu mbalimbali mikoani na vijijini
lakini kama taifa stars itaendelea kuangalia wachezaji kutoka simba yanga na azam basi tutabaki kuwa mkia duniani.
Hongera sana vijana wetu tunajivunia kuona mnatangaza nchi yenu kwa mapenzi makubwa dunia nzima.
Hongereni kwa kupeperusha vyema bendera ya Nchin yetu..
ReplyDelete