Balozi mdogo wa Rwanda nchini Tanzania Mh. Sano Lambert (katikati) akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 18 ya mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994. 

Katika Ujumbe wake ameitaka Jamii ya Wanarwanda na Dunia kwa ujumla kuchukulia tukio hilo kama changamoto ya kudumisha amani na upendo duniani na kutaka Mataifa duniani kote kuishi bila itikadi za Kikabila. Kulia ni Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Stella Vuzo na kushoto ni First Secretary wa Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania Bw. Ernest Bugingo. 

Pia ametumia fursa hiyo kuialika jamii nzima ya Watanzania na wageni waliopo hapa nchini kuhudhuria mkusanyiko utakaofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tarehe 7 mwezi huu wenye lengo la kuzungumzia sababu zilizopelekea kutokea mauaji hayo ya Kimbari, madhara yake, na nini kifanyike ili kuhakikisha matukio kama hayo yahatokei tena si tu Rwanda bali katika Mataifa yote Afrika na Duniani kwa Ujumla. Katika siku hiyo kutakuwa na mashairi, ngonjera, filamu fupi na ushuhuda kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wahanga na walioshuhudia mauaji hayo.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni "Let’s learn from our history to shape a bright future".
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Stella Vuzo akizungumzia maadhimisho hayo yatakayofanyika tarehe 7 mwezi huu ambapo amesema vyombo vya habari ni sekta muhimu ambayo inapaswa kuhudhuria pamoja na jamii nzima kutazama filamu fupi ya dakika 7 inayoonyesha kilichotokea wakati wa mauaji ya kimbari. Kulia ni Afisa kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama na Kushoto ni Balozi Mdogo wa Rwanda, Mh. Sano Lambert.

Amesema katika maadhimisho hayo watakuwepo viongozi wakaoiwakilisha Serikali ya Rwanda na pia kuhudhuriwa na Msemaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbaria ya Rwanda Profesa Chriss Maina ambapo pamoja na mambo mengine pia atazungumzia maendeleo ya Mahakama hiyo ya Kimataifa ya ICTR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wanaadhimisha kufurahia au kusikitishwa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...