Waheshimiwa Wabunge na Watanzania
Ni kwa unyenyekevu mkubwa na ninajiwakilisha mwenyewe kama mgombea kwa ajili ya uwakilishi wa bunge la Afrika Mashariki. Ni kwa ajili ya upendo kwa nchi yetu, nikaamua kuchukua hatua ya kutafuta huu uwakilishi muhimu. Hatarini tuliyonayo ndugu zangu watanzania ni masuala ambayo kwa sasa yanamadhara kwetu, itaathiri watoto wetu na watoto au wajukuu zetu kwa kiasi kikubwa siku za mbeleni. 

Hivyo Waheshimiwa wabunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania na watanzania, ni lazima kuwa makini katika itifaki hii ya uwakilishi. Miaka yangu katika fani ya elimu, utafiti, kushauri serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na sekta ya umma, umenitayarisha vya kutosha kuweza kuliwakilisha taifa letu katika bunge letu la Afrika Mashariki.

Tanzania ni moja ya mataifa tajiri duniani. Tuna hazina ambayo kamwe haiwezekani kupatikana mahali pengine popote duniani.  Tumebarikiwa na ardhi yenye hazina kubwa na watu wa kipekee. Tuna amani na utulivu japo matatizo madogo ya hapa na pale hayakosekani katika jamii hai, na juu ya yote, tunajivunia  fahari ya utamaduni wetu wa upendo. Leo hii watanzania wenzangu, hakuna Mtanzania ambaye anatambulika kutokana na itikadi yake ya kisiasa au udini wake. Hakuna mtanzania ambaye ukabila wake umeandikwa katika paji la uso wake. Tutambue kuwa hali hii ni tofauti kwa wenzetu, majirani zetu hawezi kuonana jicho kwa jicho, linapokuja maswala ya kikabila na udini. Sisi watanzania tumeshikamana  na tupo chini ya umoja wa kitaifa. Umoja wetu na uzalendo wetu unatokana na misingi iliyojengwa chini ya bendera yetu na lugha yetu tunayojivunia.

Ndugu zangu watanzania, muda umefika kutambua kwamba badala ya kuzungumza mafanikio yetu makubwa ya kibinafsi, familia tunazotoka, inatupasa kuzingatia na kutafakari zaidi utaifa na zaidi ni kwa jinsi gani tunaweza kueneza ushawishi wetu, uzalendo, umoja wetu na mbegu ya amani na utulivu kwa majirani zetu. Nikiwa kama mbunge muwakilishi, sitakubali kuwakilisha maslahi binafsi au yale ya kundi Fulani, bali nita nitapigania na kutetea maslahi ya Watanzania milioni 45. Nitapigania maslahi ya taifa langu
Nitasimama kulinda nchi yetu na rasilimali zake. Nitasimama kulinda utamaduni wetu, urithi, na mipaka yake na bendera yetu. Nitasimama kulinda maslahi ya wakulima wetu na wajasiriamali ambao wanakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa washindani wa nje ya mipaka  yetu. 

Nitasimama kupigana kwa ajili ya manufaa ya watu wetu
Katika Bunge la Afrika Mashariki, naenda kupigana kwa ajili ya maslahi ya wahitimu kutoka vyuo vyetu vikuu wasijione kama raia wa daraja la pili katika nchi yao wenyewe. Kama ilivyo katika nchi nyingine, lazima nikapiganie kipaumbele cha kuwapa nafasi ya kwanza vijana wetu nafasi ya kwanza katika soko la ajira na kuwawekea mazingira ya kuwafanya waweze kumudu changamoto za ushindani. Ni muda muhafaka kusema  INATOSHA . Ni lazima kutafuta ushirikiano mzuri zaidi katika ushirikiano wetu wa kikanda. Ninaenda kuwaelewesha wenzangu katika bunge la Afrika Mashariki "KWAMBA ARDHI YA TANZANIA" ni ya Watanzania.

Waheshimiwa wabunge na Watanzania kwa ujumla, naamini kuwa pamoja na kuwepo ushindani mkubwa ninaokabiliana nao, ndani yangu, kuna kiu ya kuipigania na kuiwakilisha vyema nchi yangu.  Ninawaahidi kuiparejeshea serikali na taifa letu heshima inayostahili. Ni lazima kuilinda hiba ya  hayati  Mwalimu Nyerere. Katika sehemu yake ya mapumziko ya milele inatakiwa ajisikie kuwa nchi aliyoiacha nyuma imekuwa nuru na dira kwa mataifa mengine kiuchumi, na pia kuwa nguzo ya amani kutokana na rasilimali watu na uongozi bora. Watanzania wenzangu, mimi nawekeza kwenu, kwa kuniwezesha kupata nafasi hii kwa sababu naenda kupambana kwa ajili ya utukufu na maslahi ya Tanzania; na kuipa nchi yetu sifa iliyokuwa nayo siku zote kama mwanga na taifa lenye nguvu katika ukanda wetu  badala ya kuwa mshabiki na mfuasi.
Tanzania inapaswa kuchukua nafasi ya uongozi. Hatupaswi kuwa wasindikizaji, vinginevyo historia ituhukumu kama wasaliti. Itakuwa vyema zaidi iwapo historia ituhukumu kama watu ambao tulisimama na kupigania maslahi na haki za watanzania. Ndugu zangu, nawaombeni ridhaa yenu ili niwe mwakilishi wa taifa letu katika Bunge letu la Afrika Mashariki

“John F. Kennedy Quotes. “My fellow Americans, ask not what your country can do
for you, ask what you can do for your country”
Mungu Ibariki Tanzania
Hildebrand Shayo, PhD
Mgombea Ubunge: Bunge la Afrika Mashariki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Jamani wa-tz ule ujinga wetu wa nyumbani Tz wa uchanguzi wa wabunge tusiupeleka kwenye bunge la East Africa, maana huko wabunge wenzetu wa Kenya & Uganda, Rwanda hawachaguliwi kwa njaa za kutafuta ulaji (ajira), kuuza sura, umaarufu, au ujamaa, Wanachaguliwa kwa sifa za uongozi, credentials haswa, na proven capability haswa kutetea maslahi ya nchi/wananchi wao, ujuzi ktk nyanja za uchumi, uongozi na jamii. Pia utagundua kuwa wao ni wajuzi wa biashara/uchumi haswa. Kwenye bunge la EA sio sehemu ya ubishi wetu wa damu eti mimi napinga/sikubali bwanaaa bila hoja msingi, na hakuna mambo ya ujamaa huko. Sasa wa-tz tukiwachagua wabunge wetu wa EA kwa vigezo vilevile vya wabunge wa kizota tumeumia. Kumbukeni kuwa Tz tuna kura 1 tu kati ya 5 ili kupitisha mswada bungeni la EA, sasa tuchague wabunge wenye sifa za kukabiliana na hao wenzetu 4 kwa hoja zenye mantiki (intellectual & social-economic sense) la sivyo tutapigwa mabao kibao ikiwemo bao la Ardhi na tutajilaumu wenyewe. Namuunga mkono Dr Shayo. alex bura, dar

    ReplyDelete
  2. Umepotea njia mchaga,siasa haikufai endelea kujuza wanafunzi.Halafu jifunze Kiswahili Tofauti ya nji na nchi

    ReplyDelete
  3. HUYU SASA NAYE ANAOMBA KWA NGUVU SIE KENNEDY ANATUHUSU NINI? WAKATI KAUMIZA WATU WEUSI SANA MAREKANI, LETE SOKOINE KASEMA NINI AU ABDUL SYKES AU BIBI TITI, ZAIDI YA HAPO NAKUOMBEA MUNGU UPATE HIKO KITI NA UTIMIZE AHADI. A

    ReplyDelete
  4. Mtanzania mzalendo wa kweli hawezi kutoka ndani ya CCM. Upo kutafuta ulaji as simple as that!

    Sikutegemea kwa upeo ulionao na umri wako ujitumbukize ndani ya CCM. Pole sana, Ph.D isikupe jeuri. Wapo wasomi wengi Afrika wanazo digrii hata za HAVARD lakini ni hopeless.

    ReplyDelete
  5. Ndugu yangu Shayo usitumie nguvu kubwa kiasi hiki kwa ajili ya siasa ni bora uendelee na ualimu wako ambao ni fani yako na unaumudu vilivyo!

    Inaweza kukubomoa zaidi kuliko kukujenga na ukajutia nafsi yako hasa kipindi hiki ambacho mwenendo wa CCM ni mbaya mno mno na ukaonekana ni wale wale huko mbeleni.

    ReplyDelete
  6. We anoni unayesema kuwa "mzalendo hawezi kutoka CCM" - atatoka wapi?? Acha umamluki wewe. Kama ulaji wewe hutaki kula? Sifa zako finyu bro..kubali yaishe!

    ReplyDelete
  7. Mangi..una matatizo gani? Wewe ndiyo unatumia nguvu kubwa kumkatisha tamaa Dr. Shayo. Tunahitaji vijana wenye nguvu, wenye upeo, kisomo kinachohitajika, ari na nguvu. Dr. usimsikilize huyu Mangi...

    ReplyDelete
  8. Dr mimi na kukubali kwani nakujua tangu uliponifundisha vision college kwa Mch Irungu london,ni moja ya vichwa naviamini,usikatishwe tamaa timiza ndoto zako tupo pamoja sana.

    ReplyDelete
  9. Upuuzi mtupu..hadithi zile zile tuache uongo huu...kuijenga tanzania si lazima uwe mbunge...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...