Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na vijana wa Shirikisho la CCM la vijana wa CCM wlioko vyuo vya Elimu ya Juu, walipofika leo kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, kumfikishia ujumbe wao kuhusu mawaziri na watumishi wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na upotefu wa fedha za umma.
Nape akisoma ujumbe uliloonyesha kumvutia zaidi kwenye moja ya mabango ya wanavyuo hao.
Vijana hao wakionyesha bango lenye ujumbe mahsusi kuhusu maana ya Mapinduzi.
Vijana wakionyesha bango la kuwataka 'magamba' waendelee kujitoa CCM.
Nape akisoma ujumbe kwenye moja ya mabango waliyofika nayo wanafuvyo hao.
Wanavyuo wakionyesha bango la kuwataka wasaidizi wa Rais kuwajibika inapobidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Sawa kabisa maana mafisadi ni wengi sana na wameiba pesa za wananchi kwa ubinafsi wao,wananchi wenye elimu kuweni ngangari na sisi tupo nyumma yenu tunawasapoti!

    ReplyDelete
  2. Nilidhani wasomi hawa watakuwa na ujumbe wa kuwawajibisha wanaokula pesa za wanyonge ila mnawashauri wahame tu na kujiuzulu then? msikurupuke na mabango tu bila kuonyesha ni jinsi gani hao mafisadi wenu wamefikisha nchi hapa ilipo. Mnapowashauri wahame aliyewalea hadi wakafika hapo kwanini asitafutwe na kuwajibishwa?

    ReplyDelete
  3. Nothing will happen, we have seen it before. They will lose their ministerial posts but not the money they have accumulated. For example how on earth can they do that - $1m in a foreigh account is vijisenti, how did he get that vijisenti. Kuleni nchi, eventually there will be nothing to steal.

    ReplyDelete
  4. Hawa mawaziri was JK wanatakiwa wote washitakiwe kwa wizi was mali ya umma. TUKURU haifanyi kazi, nchi inamtegemea Zitto tu, bila yeye hakuna hatua yeyot. Tuone serikali ikiwavua uwaziri wot follows? Yale yale na watabaki kuwa wabunge. Angalia Shirika la Reli lisivyofanya kazi kumbe linahujumiwa na mawaziri ili magari yao yafanye kazi. Nchi imeoza kabisa!!!!

    ReplyDelete
  5. These all just ccm, past or now they are all just savages, do not fit at all, to relieve the problem nikuvunja all ccm and not allowed to join any party in the country
    all ministers expelled from the CCM from the top until the bottom ... is this country will continue ..

    ReplyDelete
  6. If I was JK, I would make Nape a MInister or PM, tuone atakavyosafisha mawizara mbalimbali, anaonekana kama ni mtu ambaye anajali watanzania wenzake. Jinsi tu watu wanavyohonga na kupata ubunge inasikitisha sana. Ubunge ni stepping stone ya kuingia kwenye mapilau etc etc. Nchi gani iliyojaa ma Drs and maprofesa kwenye bunge - lazima kuna kitu hiko. Watanzania lazima tuamke in 2015, tuchague vijana watakaoendeleza nchi.

    ReplyDelete
  7. Yaani nimecheka hadi basi

    David V

    ReplyDelete
  8. Kama kawa, kumpigia mbuzi gitaa!!

    Kumuambia fisadi ajiuzulu ama ahame ni sawa na kupanda mahindi sakafuni, kamwe hautavuna!!

    Wahusika wote kama imedhihirika wamekula jasho la umma, sharti na wao wawajibike kwa kufilisiwa. Vijisenti walivyojipendelea ni haki ya raia, hawatakiwi kubaki hata na senti moja!!

    Kunahitajika mfano uliokomaa kuwawajibisha ili watakaoingia madarakani na waliobaki madarakani wasipate hata chembe ya mawazo ya kurudia kosa lao hiyo mifisadi.

    ReplyDelete
  9. wasomi hata kuandika kiswahili fasaha wanashindwa ????,kaaaaaaaaaaazi kweli kweli
    sad ,ndio tulipofikia sasa!

    ReplyDelete
  10. Upuuzi mtupu. Watanzania tutaendelea kudanganyika mpaka mwIsho wa dahari.

    ReplyDelete
  11. Are this young guys really serious?

    how on earth can you waste your time moving all the way to lumumba expecting one political giant even to feel your there!

    Wanataka kuibadilisha CCM kweeeli?

    Deep down their heart i can see they have something very different from what they are displaying in those posters.

    Ni wanafiki tu hao.

    ReplyDelete
  12. Well doctored. Ze Komedi at work.

    ReplyDelete
  13. David wewe unacheka tu,nchi inaliwa mpaka mfupa wa mwisho ,wewe bado uko kichekoni, join the force please, Taifa imeamuka sasa, mafisadi ole wenu. mnapita vijijini wananchi hata kisima cha maji ya kuchimbiwa hakuna, tannesco wanafanya wanavyotaka ukipeleka madai ya kulalamika kwamba umeletewa bili isiyo halali ,husikilizwi.una acha shughuli zako siku nzima kwenda tannesco kulia shida lakini unaonekana wewe fara tu.kumbe wengine wanacheka tu eti ni kawaida.enough is enough,they must cough the money they took.

    ReplyDelete
  14. Hakika vijana wamefanya vyema na dhamira ilio ndan ya mioyo yao ni njema sio kama wanavofikiria wengne,vijana ni jesh kubwa pamoja tunaweza pamoja sana...

    ReplyDelete
  15. TAKUKURU nao wanatakiwa waachie ofisi, waulizwe haya mambo wao hawayaoni na wao ni wasafi kiasi gani? au ndio ile ya nani wa kumfunga mwenzie kengere?

    ReplyDelete
  16. MUDA WA KUUBEBA UFISADI UMEKOMA:

    Sasa basi imetosha,

    Ni wakati wa kuchagua mawili:

    1.Kuendelea kusaidiana ktk chama tawala C.C.M badala ya kuwajibishana kwa ufisadi na uzembe.

    AU

    2.Kuichezea Shilingi Chooni kwa kuipa CHADEMA nafasi ya kukubalika.

    TUAMUE MOJA KATI YA HAYO MAWILI:

    ReplyDelete
  17. kufukuza uwaziri haitoshi, kama Nape na hawa wanaojiita wasomi wanania nzuri na CCM yao basi wawavue uanachama, ama niseme wawavue gamba.
    itakuwa vizuri na labda tutapata matumaini kidogo na hii sirikali ya dk kikwete.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...