Wanafunzi hawa wakiwa wamepozi kwa raha zao katika moja ya mabango yanayotangaza vivutio mbalimbali vya utalii.
Kaimu Balozi wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Dr. Justin Seruhere Ph.D akitoa darasa kwa sehemu ya wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Westfield cha nchini Marekani. Wanafunzi hao wameichagua Tanzania kama nchi wanayotaka kuiwakilisha katika Mkutano huo wa UN- MODEL . wanafunzi hao walipata fursa ya kujielimisha zaidi kuhusu historia ya Tanzania, watu wake, mila na tamaduni, maendeleo ya kiuchumi na kijamii, sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania, misimamo ya Tanzania katika Umoja wa Mataifa katika maeneo kama vile , biashara haramu ya usafirishaji binadamu, biashara haramu ya silaha, uhuru wa kupata habari, silaha za maangamizi, mkataba wa biashara ya silaha, ushiriki wa Tanzania katika masuala ya ulinzi wa amani, usalama wa chakula, tatizo la njaa nchini Somalia , mafaniko na changamoto mbalimbali zinazoikabili Tanzania.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Westfield wakiwa katika picha ya pamoja kutoka kushoto ni Bw. Modest Mero ambaye ni Afisa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akisimamia pia Kamati ya Pili ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kamati hiyo hushughulikia masuala yote yanayohusiana na maendeleo ya kiuchumi. Anayefuatia ni Prof. Brian Steinber,Ph.D mkuu wa msafara wa wanafunzi hao na Kaimu Balozi, Dr. Justin Seruhere,Ph.D ambaye pia husimamia Kamati ya kwanza ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Kamati inayohusika na masuala yote ya upokonyaji wa silaha
Kila mwaka katika mwezi huu wa April wanafunzi zaidi ya 5,000 kutoka mataifa mbalimbali duniani, hukusanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Jijini New York. Mkusanyiko huo ambao hujulikana kama UN- MODEL wanafunzi hao huigiza katika uhalisia namna ambavyo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanavyo jadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu masuala muhimu na changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia.
Ili kufanikisha mkutano huo, wanafunzi hao hujipanga kwa misingi ya nchi wanachama. kila Chuo huchagua nchi wanayotaka kuiwakilisha katika mkutano huo. Na ili waweze kuiwakilisha vema nchi wanayoichagua hulazimika au wanawajibika kujifunza na kujielimisha kuhusu nchi ile.
mtume, kumbe Ph.D nayo ni sehemu ya utambulisho? au ndio tunatofautisha dr na '
ReplyDeletedr'?