Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda akiweka saini kwenye kitabu cha Maombolezo ya Kifo cha Mcheza Filamu Maarufu Nchini,Marehemu Steven Kanumba nyumbani kwake Sinza Vatican,Jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Kanumba amefikwa na Mauti usiku wa kumkia leo nyumbani kwake.
 Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki,Mh. Samuel Sitta akiweka saini kwenye kitabu cha Maombolezo ya Kifo cha Mcheza Filamu Maarufu Nchini,Marehemu Steven Kanumba nyumbani kwake Sinza Vatican,Jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Kanumba amefikwa na Mauti usiku wa kumkia leo nyumbani kwake.
Ridhiwan Kikwete pia akiweka saini kwenye kitabu cha Maombolezo ya Kifo cha Mcheza Filamu Maarufu Nchini,Marehemu Steven Kanumba nyumbani kwake Sinza Vatican,Jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Kanumba amefikwa na Mauti usiku wa kumkia leo nyumbani kwake.
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Mh. Iddi Azzan akiweka saini kwenye kitabu cha Maombolezo ya Kifo cha Mcheza Filamu Maarufu Nchini,Marehemu Steven Kanumba nyumbani kwake Sinza Vatican,Jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Kanumba amefikwa na Mauti usiku wa kumkia leo nyumbani kwake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Tumepokea taaarifa hii ya kifo cha marehem Steven Kanumba (RIP) kwa udhuni kubwa na majonzi,tunatoa pole kwa familia ya marehemu pamoja na jamii yote ya watanzani.
    Tupoe sote,
    Mungu amlaze pema peponi.
    Wadau
    Ngoma Africa band aka FFU
    Ughaibuni,Ujerumani

    ReplyDelete
  2. Ni huzuni na simanzi kubwa sana kuendelela kushuhudia vijana wetu wanatutoka kila leo. Sikufahamiana na Kanumba ila nimekuwa nikiheshimu sana mchango wake katika sanaa na kujifunza kutokana na jitihada zake katika maendeleo.

    Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi Steven! Poleni sana wanafamilia, ndugu, marafiki na wanajamii wote walioguswa na msiba huu.

    ReplyDelete
  3. "INNA LILLAHI" naanza, kwa yake MUNGU hakika, "WAINNA ILAYHI" ongeza, nasi waja kadhalika,
    "RAJIOONA" namaliza, rudi kwake bila shaka,
    Yote kazi ya MWENYEZI, YARABI pema muweka.

    Nimepigwa bumbuwazi, bado tama nimeshika,
    Bubujikwa na machozi, akili mevurugika,
    Kuamini ipo kazi, kama kweli katutoka,
    Yote kazi ya MWENYEZI, YARABI pema muweka.

    YARABI muweke pema, PEPONI kupumzika,
    Nasi sote tuko nyuma, wito wako taitika,
    KANUMBA mlaze pema, 'ghufiri' alopituka,
    Yote kazi ya MWENYEZI, YARABI pema muweka.

    Mwenyeez Mungu mughufirie kwa yote na umlaze pema peponi MAREHEMU: STEVEN KANUMBA - AMEN.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...