Waziri wa Nishati na Madini,Mhe.William Ngeleja akichangia mada katika Mkutano unaojulikana kama European Union Sustainable Energy for ALL (SE4ALL) ulioanza tarehe 16/4/2012 mjini Brussels Ubelgiji. .
Waziri Nishati na Madini Mhe.William Ngeleja akisikiliza moja ya mada zilizokuwa zikijadiliwa kwenye mkutano huo.
Wadau wakimsikiliaza mmoja wa wachangiaji katika mkutano huo.

Waziri wa Nishati na Madini Mhe.William Ngeleja amehudhuria Mkutano unaojulikana kama European Union Sustainable Energy for ALL (SE4ALL) ulioanza tarehe 16/4/2012 mjini Brussels Ubelgiji.

Mkutano huo uliofunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon unajadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya nishati ikiwamo mpango mpya wa Umoja wa Ulaya kutoa huduma endelevu ya nishati kwa watu wapatao milioni 500 katika nchi zinazoendelea ifikapo mwaka 2030.

Waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Mawaziri kutoka nchi zinazoendelea zikiwemo za Afrika, Asia na nchi za Ulaya, Taasisi mbali mbali kama vile Umoja wa Mataifa, Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika, Kampuni zinazowekeza kwenye nishati na vyombo vya habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...