Mkuu wa Wilaya ya Bunda,Mh. Francis Mtinga ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati ufunguzi wa kongamano la siku ya wadau wa NHF kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mara .
Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa NHIF,Bw.Gratian Mukoba akiwaasa wadau wa Mkoa wa Mara kutimiza wajibu wao katika kuwahudumia wanachama wa NHIF na CHF ili dhima ya huduma bora za afya vijijini iweze kufanikiwa,alisema hayo wakati wa mkutano wa siku ya wadau uliofanyika Mkoani mara kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.
Washiriki wakimsikiliza mgeni rasmi ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Bunda bwn. Francis Mtani hayupo pichani.
Mama Leticia Nyaboke akiwa amemlaza na kumfunika mtoto Neema kwenye hospitali ya mkoa wa mara ambapo NHIF ilitoa msaada wa mashuka 400 kwa hospital hiyo,ikiwa ni maadhimisho ya miaka 10 ya mfuko iliyoambatana na siku ya wadau wa mkoa huo.
madereva wa pikipiki wa Mkoa wa Mara,wakiwa na vihakisi mwanga kwa ajili ya usalama barabrani (reflector) vilivyotolewa na NHIF/CHF.Hawa si boda boda kama ilivyozoeleka kwa wengi wenyewe wanajiita madereva wa pikipiki.

NA.Paul Marenga-Mara

Watendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mifuko ya Afya ya Jamii wametakiwa kuhamasisha wananchi kujiunga na mifuko hiyo kwani uelewa mdogo wa utendaji wa Mifuko hii kwenye mkoa Mara ndiyo chanzo cha kuwa na Idadi ndogo ya wanachama wachangiaji,kwani hadi disemba mwaka jana ni kati ya kaya 237,071 zilizopo ni kaya 1,460 tu zilizojiunga na CHF sawa na 0.6 %asilimia.

Akizungumza Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda bwn. Francis Mtinga alisema ‘Pamoja na agizo na maombi ya bodi ya wakurugenzi wa NHIF, nawataka muandae utaratibu na kuwa na program maalum za kuwashirikisha watendaji kuanzia ngazi ya kata,kutoa elimu stahiki kuhusu utendaji wa mifuko hii,sanjari na maboresho ya huduma za afya hapa mkoani kwetu kwani wananchi wana uwezo wa kuchangia kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato walivyo navyo lakini elimu ndiyo kikwazo.

Pia amewaomba wananchi kuwa walinzi wa huduma za matibabu hususani wanapokutana na dawa zinazotolewa na serikali zinauzwa katika maduka ya watu binafsi,toeni taarifa kwa wahusika ili hatua stahili zichukuliwe,.bwn Francis Mtinga alisema.

Naye mjumbe wa bodi ya wakurugenzi NHIF ambaye pia ni Rais wa CWT bwn. Gratian Mukoba amewataka wakuu wa wilaya,waheshimiwa wabunge, makatibu tawala na watendaji kuanzia ngazi ya kata na Halmashauri, kuunganisha nguvu ya pamoja katika kusimamia fedha za NHIF/CHF ,sambamba na uhamasishaji wa wananchi kuchangia Mifuko ya Afya ya Jamii,Mikopo ya Vifaa Tiba na Ukarabati wa Majengo.

Bodi imeidhinisha mikopo hii zaidi ya miaka mitatu (3) lakini watoa huduma wengi hawajachangamkia fursa hii,hivyo nitumie nafasi hii kuwahamasisha ili kuboresha huduma za matibabu kwa wanachama na wananchi kwa ujumla kwenye hospitali,zahanati na vituo vya afya vilivyopo mkoani kwenu.

Wakichangia katika kongamano hilo bwn Alfonce Mwita mtoa huduma wa kata ya kyabakari kutoka Tarime alisema watoa huduma wachache wasio na maadili wamekuwa wakidhoofisha,nia njema ya serikali kupitia mifuko hii ya NHIF/CHF katika kuboresha huduma za matibabu nchini.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeendelea kuwa na makongamano ya siku za wadau kwenye mikoa yote nchini sanjari na maadhimisho ya miaka 10, kama ambavyo umefanyika Mkoani Mara ,lengo likiwa ni kufanya mrejesho na kukusanya maoni na ushauri kwa wadau wake,ili kuboresha utendaji wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...