Waziri wa Uchukuzi,Mh. Omari Nundu (aliesimama) akifungua Mkutano wa kwanza wa Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) jijini Tanga leo, wenye wajumbe 70. Katika hotuba yake Waziri amesema kwa kutumua umuhimu wa mfanyakazi katika kuongeza tija na Ufanisi wa Mamlaka,wizara inampango endelevu wa mafunzo wenye lengo la kukuza Ustadi na Uwezo wa Wafanyakazi katika kumudu mazingira yake ya kikazi, Ili kufikia lengo hili Mamlaka yake hutenga fungu la fedha za mafunzo, zisizopanua asilimia tano ya Bajeti yake ya kawaida ya kila mwaka, hivyo katika mwaka 2012/13 Mamlaka inategemea kutumia sh.1.5 bilioni.
Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu (kushoto) akiongea na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Usafiri kutoka Wizara ya Uchukuzi Saad Fungafunga (mwenye Kaunda) wakati wa kufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Baraza la wafanyakazi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga jijini Tanga leo.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga ambao unafanyika jijini Tanga leo na umefunguliwa na Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu (hayupo pichani) wajumbe 70 wanahudhuria, (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Hizo billioni moja zitumike kuziba mashimo na kutoa matope uwanja wa ndege wa Kigoma!!
ReplyDeletebillioni moja zipi?
ReplyDelete