Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. RIP Mwalimu, kwa kweli we miss you loads, busara zako ni za nguvu.

    ReplyDelete
  2. Baba wa taifa i wish ungekuwa hai..maana your last statement ya kiongozi bora hawezi kutoka nje ya CCM ungeibadilisha, rushwa,ufisadi na mambo yote uliyoyasema CCM hawana tena

    ReplyDelete
  3. Msukuma wa BagamoyoApril 06, 2012

    HII SPEACH ANKAL MURUA KABISA JAPOKUWA WEWE NI CCM UMEIWEKA KWENYE MUDA MUAFAKA KABISA. MABADILIKO TUSIPOYAPAT CCM TUTAKWENDA KUITAFUTA NJE YA CCM. TOMECHOKA NA RUSHWA,UMASIKINI, UDINI NA MUUNGANO.

    LAKINI SASA KUNA JIPYA LA KOO, HATUNA UONGOZI WA KIFALME SISI. HAIWEZEKANI BABA ANAMRISISHA MTOTO. JAMANI TUWE MAKINI HAPA.

    THIS GENTLEMAN WAS AN IDOLOGIST, HONEST,HARDWORKING AND A BELIEVER.

    RIP

    ReplyDelete
  4. Kaka michuzi hii hotuba utafikiri imetoka leo kweli Mwenyezi Mungu amrehemu Mwalimu. Yaani aliyosema ni ukweli mtupu ila kwenye swala la kiongozi safi bado CCM kuna tatizo tena ni tatizo kubwa sana, sijaona kiongozi anayepinga rushwa sijaona kiongozi mwenye jitihada za kuwakwamua wananchi kwenye kilimo zaidi naona tu wanajilimbikizia ardhi kuubwa pia sijaona kiongozi mwenye nia ya DHATI kutaka kuondoka tatiozo la ajira kwa watu wa aina zote kuanzia mkata nyasi mpaka mkurugenzi,sijaona kiongozi anayekemea UDINI kwa mfano kuna watu wanaoendesha mihadhara ya kukashifu DINI za wengine mfano MAZINGE na wengine wengi tu na wala hawachukuliwi hatua yeyote.Kwenye ukabila sina hakika mimi baona wote ni watanzania tu ila naamini hayo mambo ya ukabila yapo. WAISLAM NA WASABATO CHONDECHONDE JAMANI.

    ReplyDelete
  5. Kaka michuzi hii hotuba utafikiri imetoka leo kweli Mwenyezi Mungu amrehemu Mwalimu. Yaani aliyosema ni ukweli mtupu ila kwenye swala la kiongozi safi bado CCM kuna tatizo tena ni tatizo kubwa sana, sijaona kiongozi anayepinga rushwa sijaona kiongozi mwenye jitihada za kuwakwamua wananchi kwenye kilimo zaidi naona tu wanajilimbikizia ardhi kuubwa pia sijaona kiongozi mwenye nia ya DHATI kutaka kuondoka tatiozo la ajira kwa watu wa aina zote kuanzia mkata nyasi mpaka mkurugenzi,sijaona kiongozi anayekemea UDINI kwa mfano kuna watu wanaoendesha mihadhara ya kukashifu DINI za wengine mfano MAZINGE na wengine wengi tu na wala hawachukuliwi hatua yeyote.Kwenye ukabila sina hakika mimi baona wote ni watanzania tu ila naamini hayo mambo ya ukabila yapo. WAISLAM NA WASABATO CHONDECHONDE JAMANI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwanini useme waislam na wasabato? na sio waislam na wakristo!!! wewe ndio mdini sasa unabagua hata wakristo wenzio...lol hii hatari

      Delete
  6. Mwl. Mungu akurehemu huko uliko. Uliowategemea kutuongoza wameshatuuza, tunataabika kama kondoo wasio na mchungazi!

    ReplyDelete
  7. Bwana michuzi nashukuru sana kwa video ya mzee wa Africa The greatest African man born in African a man with vision im from you uganda but Mwalimu is the greatest African man who had a vision asante sane i wish i could get the dvd of this speech,asante bwana michuzi we miss you mzee,you made me cry today because today in Africa we dont have leaders we have crooks and politician who love to lie,
    asante wamala

    ReplyDelete
  8. What a great man. We will always miss your wisdom and intellect. RIP Mwalimu.

    ReplyDelete
  9. Nadhani Baba wa Taifa alikosea aliposema hakuna kiongozi mzuri kutoka vyama vya upinzani. Viongozi wazuri wapo na siku moja watapatikana na Tanzania itakuwa nzuri kushinda hata wakati wa utawala wa CCM.

    Baba wa Taifa, tunamheshimu kwa busara zake, lakini hata yeye ni mwanadamu na ana mapungufu yake kama binadamu wengine. Si kweli kwamba kiongozi mzuri lazima atoke CCM.

    ReplyDelete
  10. R.I.P JKN.

    ReplyDelete
  11. Mwl. Nyerere alikuwa Mwanafalsafa mzuri kwa vile mara nyingi mtoa Falsafa hutoa kwa kinyume nyume na ndio ilikuwa makusudio yake, endapo Wanafunzi wake wasipokuwa wanafuata maadili.

    Itabidi iwe kinyume chake kutokana na Ufisadi, Ubinafsi, Ukiukaji na Ukandamizaji na sasa Kiongozi Mzuri atatoka NJE YA C.C.M !

    ReplyDelete
  12. Mdau unaedai kina Mazinge wanakashifu dini za wengine una hakika na hilo? Au unaimba wimbo mradi tu unaimbwa na wengi? Kwa miaka mingi nimefatilia hii mihadhara, pale jamaa wanapodai kukashifiwa ukichambua utakuta si kashfa ni maandiko. Sababu ya kukosa kuelewa, wengine hudhani ni kashfa. Huwezi kudai kuna kashfa usipoweza kuiainisha. Jamaa hawa mara zote wameelezea kuwa HUWEZI KUWA MUUMINI WA KWELI WA UISLAMU KAMA HUMHESHIMU NA KUMWAMINI YESU (NABII ISA-Amani ya Mwenyezi Mungu imfikie). Na kwa maana hiyo wahubiri hawa humpamba na kumuenzi Nabii Yesu, na kwa mujibu wa maandiko, hasa Biblia, huthibitisha kuwa dini na ujumbe wa kweli wa Nabii huyu mteule ulitiwa mikono ukapotoshwa. Na hilo ni kwa mujibu wa Injili na Qurani pia. Tafadhali mdau tumia muda wa kutosha kuchambua wanachosema wahubiri hawa then naamini utawaelewa na hatimae kubadili fikra na uelewo wako. I'm not writing from a jazba point of view. Mihadhara aina hii inafanyika kwingi duniani na hakuna madai ya kashfa. Si Afrika tu, hata Amerika na Ulaya, that can prove to u kwamba zingekuwa kashfa mihadhara isingeruhusiwa. Ila kama "baba wa Taifa" alivyojenga mentality kuwa upinzani hauzai kiongozi bora, dhana isiyothibitika kisayansi, ndio hivo hivo imejengwwwa dhana kuwa mihadhara inakashifu. Mdau ukerewe

    ReplyDelete
  13. Mwalimu was the best ever in Africa politics,wapi nitapata zile nyimbo za kuomboleza kifo cha mwalimu zilizoimbwa na John comba?

    ReplyDelete
  14. Rushwa, udini na wizi wa mali ya umma ndio vimezidi kuongezeka. CCM imeshindwa kuzuia hivi, kwa hiyo mabadiliko lazima yatoke nje ya CCM. Tuache ushabiki wa vyama na ubinafsi, bali tutangulize maslahi ya taifa kwanza kwa faida ya watoto wetu na vizazi vijavyo. Kukumbatia ufisadi jinsi ilivyo sasa ni kujihujumu wenyewe. Itakula kwetu!

    ReplyDelete
  15. Mwalimu na watanzania tulipigwa vumbi la macho na viongozi waliofuata kuanzia 1985 hadi leo.
    "watanzania wasipopata mabadiliko na matumaini CCM watayatafuta kwingine"! Mzee alijaliwa maono ya hatari! RIP Kambarage! Tunahitaji Kambarage mwingine!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...