Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Watu 30 wakiwemo wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe wakikabiliwa na makosa mbalimbali ikiwemo kuwashambulia Polisi,kuchoma moto matairi ya Magali barabarani na ukorofi.
Mbali na tuhuma hizo,pia wameshtakiwa kwa kufanya maandamano yasiyokuwa na kibali kinyume na sheria pamoja na uzembe na ukorofi wa kuwashambuliya polisi kwa mawe.
Watuhumiwa hao walifikishwa katika mahakama nne tofauti, ikiwemo mahakama ya hakimu Mohammed Ali Mohammed walikofikishwa watuhumiwa wawili, wanne kwa hakimu Janet Nora Sekihola, 11 kwa hakimu Omar Mcha Hamza na 11 waliobakia, wamepandishwa mbele ya hakimu Valentine Andrew Katema.
Kwa nyakati tofauti watuhumiwa hao walishitakiwa kwa makosa ya kufanya mikusanyiko isivyo halali, uzembe na ukorofi pamoja kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani.
Watuhumiwa hao ni Mbarouk Said Khalfani (45), na Mussa Juma Issa (57) wanaodaiwa kuwa ni viongozi wa Jumuiya hiyo, ambapo walifikishwa mbele ya hakimu Mohammed Ali Mohammed, na kusomewa shitaka la kufanya mkusanyiko isivyo halali kinyume na kifungu cha 55 (1) (2) (3) na kifungu cha 56 cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.
Wengine ni Mbwana Hamadi Juma (50), Massoud Hamadi Mohammed (17), Mohammed Juma Salum (35), Abdulrahman Simai Khatib (19), Hashim Juma Issa (54) Matar Fadhil Issa (54).
Watuhumiwa hao kwa upande wao wamefikishwa katika kizimba cha mahakama ya hakimu Mdhamini Janet Nora Sekihola kujibu shitaka uzembe na ukorofi kinyume na kifungu cha 181 (d) cha kanuni ya adhabu sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.
Wengine walifikishwa katika mahakama ya hakimu Omar Mcha Hamza na Valentine Andrew Katema, wakikabiliwa na mashitaka ya kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani.
Wakiwa mahakamani hapo, watuhumiwa hao walishitakiwa chini ya kifungu cha 74 (1) (b) cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.
Mashitaka yote hayo yaliwasilishwa kwa nyakati tofauti na Waendesha Mashitaka, Wanasheria wa serikali Mohammed Kassim Haasan, Suleiman Haji Hassan pamoja na Ramadhan Abdallah, kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).
Katika mahakama ya hakimu Mohammed Ali Mohammed, Mwendesha Mashitaka Mohammed Kassim alidai kuwa watuhumiwa Mbarouk Said na Mussa Juma, bila ya halali walipatikana wakiandamana kupitia katika maeneo mbali mbali ya Manispaa ya mji wa Zanzibar.
Tukio hilo lilidaiwa kutokea Mei 26 mwaka huu majira ya saa 6:30 za mchana huko Lumumba wilaya ya Mjini mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, shitaka ambalo hata hivyo walilikana mahakamani hapo.
Kwa upande wa watuhumiwa sita waliofikishwa katika mahakama ya hakimu Janet Sekihola, Mwendesha Mashitaka Suleiman Haji alidai kuwa watuhumiwa hao walifanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani.
.jpg)
Kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka huyo, kitendo hicho ni cha kuchoma moto mipira ya gari barabarani pamoja na kuwarushia mawe askari Polisi, baada ya kukusanyika isivyo halali katika barabara ya Michenzani wilaya ya Mjini Unguja, majira ya saa 1:00 za usiku wa Mei 26 mwaka huu.
Katika mahakama zote hizo, watuhumiwa hao walisimamiwa na Wakili wa Kujitegemea Abdallah Juma, ambapo aliiomba mahakama hizo kuwapatia wateja wake dhamana, kwa mujibu wa kifungu cha 150 (1) cha sheria za mwenendo wa jinai (CPA) namba 7/2004 sheria za Zanzibar.
Watuhumiwa waliofikishwa mbele ya hakimu Omar Mcha Hamza na Valentine Andrew Katema, Mwendesha Mashitaka Ramadhan Abdallah kwa nyakati tofauti aliwasomea watuhumiwa hao mashitaka ya kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani.
Wote hao kwa pamoja walidaiwa kupanga mawe barabarani, kuchoma moto mipira ya gari barabarani pamoja na kuwarushia mawe askari, kitendo ambacho kingeweza kuleta uvunjifu wa amani.
Matukio hayo yametokea Mei 27 mwaka huu, majira ya saa 7:00 za mchana katika maeneo ya Mfereji wa wima na Amani wilaya ya Mjini Unguja.
Upelelezi wa mashauri yote hao bado haujakamilika kwa mujibu wa Waendesha Mashitaka wa mahakama hizo, na kuomba yaahirishwe ili waweze kukamilisha upelelezi wake.
Mahakama zote hizo zilikubaliana na hoja hizo za upande wa mashitaka, na kuziahirisha kesi hizo hadi Juni 11 mwaka huu kwa kutajwa.
Hadi redio hii inaondoka mahakamani hapo, kulikuwa hakuna hata mmoja aliyetoka kizuizini, licha ya mahakama hizo kuwapatia masharti ya dhamana.
Masharti hayo ni bondi ya shilingi 300,000 na wadhamini watatu waliotakiwa kusaini bondi ya kiwango kama hicho cha fedha kwa kila mdhamini, ambapo mmoja kati yao awe ni mfanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Masharti hayo yametolewa kwa watuhumiwa wawili waliofikishwa mbele ya hakimu Mohammed Ali Mohammed, ambapo sambamba na masharti hayo wadhamini hao pamoja na watuhumiwa wenyewe wametakiwa kuwasilisha kopi ya hati ya kusafiria, barua za Sheha wa Shehia wanazoishi pamoja na kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.
Hakimu Janet Sekihola, Omar Mcha Hamza na Valentine Andrew Katema, kila mmoja aliwataka watuhumiwa hao kujidhamini kwa bondi ya shilingi 500,000 na wadhamini wawili wenye vitambulisho watakao wasilisha kiwango kama hicho cha fedha taslimu, na hakimu Valentine kuongeza kuwa mmoja kati ya wadhamini hao awe ni mfanyakazi wa SMZ.
Mbona kosa la kubomoa kanisa halikutajwa kama moja ya tuhuma? Tuelewe kwamba dola ya zanzibar inabariki kubomolewa kwa makanisa?
ReplyDeleteSafi sana SMZ. next time watafikiria vizuri kabla kuamua kufanya fujo
ReplyDeleteKama hawataki muungano tunawang'ang'ania wa nini? Mbona sioni hata manufaa yake au kuna watu wanamaslahi binafsi?
ReplyDeleteUislam safi sio ukorofi, uvunjaji taratibu, pupa na jazba,
ReplyDeleteJe ninyi UAMSHO
Ni Masheikh zaidi ya Maalim Seif Sharrif Hamad?
Mnajua Uislam zaidi ya Maalim Seif aliyekuwa kwa muda mrefu ktk harakati?
Tunataka 'state of order' yaani mambo kwenda kwa utaratibu.
NI MUHIMU WAKOROFI HAO WASIFUNGIWE KWENYE MAGEREZA YA 'KIKE' ZA ZENJI YA CHUO CHA MAFUNZO ILA WALETWE WAFUNGIWE KTK MAGEREZA YA 'KIUME' YA BARA YA LUPANGO!
Wahalifu hao wa Zenji waletwe kuja kufungiwa kwenye Magereza ya Bara ya kukesha ambayo hakuna kulala.
ReplyDeleteNi vile ukijipindua kulala tu au hata kupitiwa na usingizi au kusinzia ,asalaleee imekula kwako unakuta 'bucha' lako zamani limevunjwa!
kwenye kesi hii naona kama mchezo wa kuigiza tu. unaposema vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani kama vile kupanga mawe barabarani, kuchoma mipira na kuwarushia mawe polisi na ukaacha kusema uchomaji wa kanisa unamaanisha nini??
ReplyDeleteje uchomaji kanisa umehalalishwa na sio kitendo kinachoashiria uvunjifu wa amani??
kama hakuna kanisa lililochomwa, je waandishi mbalimbali waliudanganya umma??
tatizo la zanzibar sio muungano bali ni udini uliokomaa sana, na pia ukosefu wa elimu na akili kwa pamoja so wale wachache wenye upeo na elimu kidogo wanawaburuza wengine wasioweza hata kufikiri.
kama hamtaki muungano au mnakandamizwa kwenye muungano fuateni taratibu za kisheria kutatua matatizo ya muungano hata kuvunja muungano.
Mbona hakuna aliyeshitakiwa kwa kosa la kuchoma makanisa?
ReplyDeleteWazanzibar wako na matatizo Hawa wanataka Rais Kama Yule commando ndio wanatulia.
ReplyDeletesomeni vizuri, for sure mtajua ukweli
ReplyDeleteZANZIBARI:
ReplyDeleteMMESHATUMIA RASILIMALI ZETU NYINGI TU TOKEA MWAKA 1964 HADI SASA.
1.UMEME:
MLIKUWA KWA MUDA MREFU KIFIKIRI KUWA UMEME NI NGUVU ZA ASILI KAMA JUA!!
MFANO UMEME MMEKUWA MKITUMIA BURE MIAKA NENDA MIAKA RUDI HADI MWAKA 2005 NDIO MEIJUA BILI YA UMEME.
2.HUDUMA ZA SERIKALI:
MMESOMA BURE NA KUTUMIA FEDHA ZA SERIKALI YA BARA YENYE MADINI NA MIPANGO KIBAO YA MAPATO MIAKA NENDA MIAKA RUDI.
3.KODI:
MMEHSKWEPA SANA KODI NA KUFANYA MAGENDO KWA MIAKA MINGI TU HADI WENGI MMEKUWA MATAJIRI.
4.ARDHI:
KWENU ARIDHI NI NDOGO SANA NA SERA YENU YA ARIDHI IMEWAPENDELEA NINYI, MMESHIKA MAENEO YETU MENGI BARA NA MMEJENGA.
5.MCHANGANYIKO WA NASABA:
TUMESHAZALIANA SANA WAZANZIBARI WENGI WAMEOA BARA NA WABARA WAMEOA ZANZIBARI HIVYO KUUVUNJA MUUNGANO KUTAWAPA SHIDA KUWA KTK NASABA ZILIZOPO NA MCHANGANYIKO.
6.HARAKATI HARAMU:
HIYO ZANZIBARI (PEMBA+UNGUJA) NI KAMA WILAYA MBILI TU,
WIKI CHACHE NYUMA HUKO MOMBASA KENYA WALIZUKA 'MABWEGE' FULANI(MOMBASA REPUBLICANS COUNCIL-MRC) WAKIDAI MOMBASA IJITENGE KAMA NINYI (UAMSHO) MNAVYOTAKA ZANZIBARI IJITENGE, SASA INA MAANA KILA WILAYA NCHI NZIMA ITATAKA KUTANGAZA IJITENGE!!!,,,
HIVYO MADAI YENU YA KUDAI NCHI NI BATILI,,,ZANZIBARI (Wilaya mbili 2) MNADAI NCHI MNADAI WILAYA?
7.SERIKALI YA MSETO:
KTK MCHAKATO WA MUHIMU NI SERIKALI YA MSETO AMBAYO WAMO SEIF SHARRIF HAMAD MPINGA MUUNGANO NO.1 KULIKO NINYI KUNDI LA UAMSHO, HIVYO MSIWE NA HARAKA SUALA LINATATULIWA NA KUWA HIZO HARAKATI ZENU NI SEHEMU YA UHUNI TU.
ASIYETAKA MUUNGANO APANDE JAHAZI AENDE ARABUNI KWAO KWA BABU ZAKE!
Zaidi ya hapo tutawaweka Gerezani kwa vifungo.
KWA HIVYO KWA SABABU KUBWA NA NYETI HIZO SABA (7) NG'O HATUWEZI KUUVUNJA MUUNGANO!
MUUNGANO HAUVUNJIKI:
ReplyDeleteMwarabu asitumie Tiketi ya Uislamu kupata nchi, Uislamu ni dini yetu Tukufu na tunaipenda saana na wala Mwarabu amsimshirikishe Mwenyezi Mungu na Dini Tukufu ktk kufikia lengo la kujipatia Maslahi ya Kidunia!
Kwa sababu moja (1) kubwa ni kuwa Mwarabu hana nchi ktk Bara la Afrika!
Watanganyika wacheni longolongo mambo ya Zanzibar hayawahusu...wacheni kupoteza muda wenu kwa kufuatilia mambo ya Wazanzibari
ReplyDeleteUAMSHO hamuwezi kuipata nchi kwa staili ya Fisi kuvizia kivuli !
ReplyDeleteMakosa mengine ya kuongezea ktk Mshitaka ni :
ReplyDelete1.KUUHUJUMU UISLAMU NA KUFANYA NI DINI YA WAKOROFI.
2.KUMUHUJUMU MWENYEZI MUNGU KWA KUTUMIA DINI TUKUFU ILI KUFIKIA MALENGO YA KIDUNIA.
3.KUWADHALILISHA WAISLAMU WOTE DUNIANI KWA KUWAFANYA WAONEKANE HAWANA UBINAADAMU NA UTU KWA KUWAFANYIA UBAYA WATU WA DINI NYINGINE.
hao UAMSHO, tatizo sio Muungano, ila tatizo lao ni kwamba hawajui dini, kwa kuwa kamab wangekuwa wanajua dini wasingechoma nyumba za ibada kwa kuwa sio nyumba ya mtu hiyo ni nyumba ya mungu, na uachane nao kabisa kwa kuwa watatupotea muda acha sheria ya kidunia ichukue mkondo wake, na mungu ndie atakaowaamulia, Waislam wema ni wale wanaotangaza kuhusu uislam na sio magovi mafarakano na vita, hao hawajui cha kuzungumza na cha kufanya. hivi kuna mtu aliyewahi kuamua kwamba yeye anatakiwa kuzaliwa katika familia ya kiislam, au ya kikisto? ni mungu ndio aliye amua kama nani aabudu nini, alkini sisi wote tumekuwa watu wakumkosoa mungu kwamba dini yangu ndio nzuri ya kwako mbaya. Mungu ndio aliyetuumba wote hivi tumemaliza kusoma na kuelewa quran? na kuwaelewesha kikazi kinachokuja kuhusu kilichoandikwa kwenye vitabu vya dini? na tumeaachana na mambo ya msingi na kuanza migogoro ambayo hayana msingi?
ReplyDeletehebu tuache hayo, hakuna dini mbaya zote zinatoka kwa mwenyezi mungu, na tuzame katika kutenda yaliyo mema
kama uislam wenyewe ndio huo hata mimi nahamia kwenye ukristo
ReplyDeleteAsiyetaka Muungano aende Omani !
ReplyDeletewewe anonymous uliyesema hao wakifungwa waletwe huku bara nikupongeze kwa point hiyo ninavyojua walivyolegea hao wapemba nafurahia sana,nitahakikisha shea yangu wanakula wao halafu mambo mengine usihoji,nitahakikisha wanapata urojo wa haja,waletwe bara hao
ReplyDeleteUAMSHO:
ReplyDeleteNawaasa mara 10 kama kweli mnafuata Uislam kamili na kumwamini Mwenyezi Mungu mjirekebishe!
Kwa kuwa 'hakuna' ushahidi wowote unaosema kuwa Uislam unaunga mkono 'UHALIFU'
1.MJIREKEBISHE MSIRUDIE TENA:
-MPO NJE YA UISLAM
-MMEUDHALILISHA NA KUUTWEZA UISLAM
-MHUBIRI UISLAM NA SIO MACHAFUKO!
2.MJIREKEBISHE MSIRUDIE TENA:
-MPO NJE YA UISLAM
-MMEUDHALILISHA NA KUUTWEZA UISLAM
-MHUBIRI UISLAM NA SIO MACHAFUKO!
3.MJIREKEBISHE MSIRUDIE TENA:
-MPO NJE YA UISLAM
-MMEUDHALILISHA NA KUUTWEZA UISLAM
-MHUBIRI UISLAM NA SIO MACHAFUKO!
4.MJIREKEBISHE MSIRUDIE TENA:
-MPO NJE YA UISLAM
-MMEUDHALILISHA NA KUUTWEZA UISLAM
-MHUBIRI UISLAM NA SIO MACHAFUKO!
5.MJIREKEBISHE MSIRUDIE TENA:
-MPO NJE YA UISLAM
-MMEUDHALILISHA NA KUUTWEZA UISLAM
-MHUBIRI UISLAM NA SIO MACHAFUKO!
6.MJIREKEBISHE MSIRUDIE TENA:
-MPO NJE YA UISLAM
-MMEUDHALILISHA NA KUUTWEZA UISLAM
-MHUBIRI UISLAM NA SIO MACHAFUKO!
7.MJIREKEBISHE MSIRUDIE TENA:
-MPO NJE YA UISLAM
-MMEUDHALILISHA NA KUUTWEZA UISLAM
-MHUBIRI UISLAM NA SIO MACHAFUKO!
8.MJIREKEBISHE MSIRUDIE TENA:
-MPO NJE YA UISLAM
-MMEUDHALILISHA NA KUUTWEZA UISLAM
-MHUBIRI UISLAM NA SIO MACHAFUKO!
9.MJIREKEBISHE MSIRUDIE TENA:
-MPO NJE YA UISLAM
-MMEUDHALILISHA NA KUUTWEZA UISLAM
-MHUBIRI UISLAM NA SIO MACHAFUKO!
10.MJIREKEBISHE MSIRUDIE TENA:
-MPO NJE YA UISLAM
-MMEUDHALILISHA NA KUUTWEZA UISLAM
-MHUBIRI UISLAM NA SIO MACHAFUKO!
WASSALAM!
WABILLAHI TAWFIQ!
watoa maoni wengi inaonesha ni wa upande wa pili namaanisha Bara,Na wewe ulosema ZNZ wamekosa elimu wewe ndio umekosa akili hasa, kuna matukio mawili tofauti hapo ufahamu,Waliokamatwa wamekamatwa kwenye maandamano sio kwenye kanisa,kanisa lilichomwa usiku walokamatwa ni mchana
ReplyDeletesasa utawahusisha vipi wakati huna ushahidi We ndio kweli huna hata hiyo ya Darasa lenu la saba.
Zanzibar hakuna udini ila nyinyi bara ndio mnauleta nchi ina historia yake zamani na haya mambo yana sababu zake tu ndio inatupelekea huko,Sheria ishafuatwa siku nyingi muungano hatuutaki lakini bado mnang'ang'ania tu sijui una faida gani na hauna faida na nyinyi Mizigo ya nini?
Uamsho wamekanusha na kuhusika na mzanzibari hasapoti kabisa masuala ya kuchomwa hao ni watu binafsi tu wasioelewa dini na mmoja wao anajina hilo hilo la kwenu inaonesha ametumwa ili atupakazie
Hawa jamaa Wahalifu wa Zanzibar wanatakiwa waje wafungiwe Bara sio huko Kisiwani kwenye Vyuo vya Mafunzo wanakolishwa chapati kwa mchuzi wa samaki!
ReplyDeleteWanatakiwa wapandishwe Boti waletwe Bara (Mrima kama wanavyokuita/ TANGANYIKA) ktk Magereza ya Lupango ambako Madishi/ vyakula ni kama vifuatavyo:
PRISON MENU IN TANGANYIKA:
MENU-1
-Ugali wa dona (wenye maturu na vipande vya mabunzi kama ukubwa wa dole gumba)kwa Maharage matatu (3) mchuzi debe !
MENU-2
-Ugali wa dona (wenye maturu na vipande vya mabunzi ukubwa wa dole gumba) kwa dagaa wawili (2) mchuzi ndoo tatu (3)!
MENU-3
-Ugali wa dona (wenye maturu na vipande vya mabunzi saizi ya dole gumba) kwa kabechi iliyokatwa vipande kwa shoka saizi kama viganja vya mikono !
PRISON DAYTIME WORK:
WORK-1
Kuponda kokoto kwa nyundo ya mkono ya kilo 49.5
WORK-2
Kuachana mbao kwenye magogo ya Mvule
BAADA YA KIFUNGO CHA BARA WATAKUWA WAMEKOMA !
jamaa ya zanzibar muungano si lazima hivyo tumieni njia za kistaarabu kuudai hakuna atakaye wang'ang'ania ila mfikiri makini na je kama wapemba wanataka bakia ktk muungano hamuoni kuwa mnawaburuza? hata sie wabara ni kama mbeleko imetoboka sasa mnavyoleta mtikisiko mtadondoka chini na kwetu itakuwa nafuuuuu.mzigo wa kuwabeba pia mzito.ila ni kweli na nyie uhuru ni haki yenu mtakavyo.nendeni tubaki salaaama usalimini.
ReplyDeletecomments nyingi hapa zimejaa u bara hamna lolote.nyinyi wa tanganyika zanzibar inakuhusuni nn?mbn ss hatutaki yenu?mnajuwa kwamba ziliunganishwa nchi 2 kabla ya kuwa tanzania?angalia utanganyika wako kwanza coz huo u tanzania maana yake ni tanganyika na zanzibar,wewe hiyo tanganyika iko wapi katika ramani hii ya dunia?mm najulikana kama nilivyo mwanzo nikiitwa zanzibar hadi leo ni zanzibar wewe je?yako huyaoni unayasema ya mwenzako.au hujui kama tuliungana?na sherehe si ziko hadi leo ikifika tarehe watu wanashereheka muungano?au vp?sasa kasema nani kuna muungano usiovunjika?muungano ni kama ndoa tu anytime mnaa achana sio kama dini yenu ukishaowa au kuolewa hakuna kuachana ,sisi ni waislamu na serikali yetu pia ya kiislamu hadi leo mirathi inarithishwa kiislamu kwenu yapo mambo haya?muungano utavunjika tu,kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho.
ReplyDeleteeti kuna mtu hapa anasema zanzibar ni mzigo ?mwengine anasema zanzibar imetumia rasilimali kibao za tanganyika?kwanza wewe unaesema hivyo una akili timamu?ujuwe ziliunganishwa nchi mbili tanganyika na zanzibar na sio idadi ya watu,na aliemfata mwenziwe kutaka muunganio ni nyerere kaja zanzibar kuleta maombi ya muungano tena ilikuwa miaka 10?sasa ikiwa bado hujazaliwa muulize mzee wako aliekuwepo kabla ya kuunganishwa zanzibar ilikuwa vp na tanganyika ilikuwa vp?usivamie kujibu masuala usiyoyajuwa utachekwa,maana ya muungani ni nn?hata useme hauvunjiki?nakupa mfano hai ujue nyinyi tanganyika mnakula mali za muungano,coz sisi zanzibar tuliungana nae hatumuoni,elewa kulikuwa na TANGANYIKA NA ZANZIBAR.sawa?leo zanzibar ipo au haipo?sasa sisi tunajiuliza huyo tanganyika yuko wapi?tunaambiwa tanzania katika hio tanzania na sisi tumo.mshatuibia sana na sasa tushashtuka kwamba mnatufanyia yalee mambo ya kiini macho ulieungana nae humuoni unaambiwa tanzania.ikitoka msaada flani kutoka nje maana yake nini?tanganyika pasu na zanzibar pasu leo iko wapi?mnaruka eennnh nyinyi mko kidogo?sisi tunailiza udogo au nchi hapa?chambua kwa makini sana ikiwa una akili timamu jiulize tanganyika iko wapi?na asili ya zanzibar ni uislamu kwa asiejuwa ukiristo mnao nyinyi huko.kwa hivyo tunataka maadili ya kiislamu.sera ya nyerere ni kueneza ukafiri zanzibar hakuna jengine.sasa tumeshtuka tunataka nchi yetu,mwengine eti anasema wazanzibar wamejenga huku kwetu wametumia ardhi yetu una akili wewe?wazanzibar wanamiliki ardhi hata marekani na uingereza sio hapo tu.na uvunjike bhana tushachoka.koti likikubana utalivua sisi tumechoka hatutaki na uvunjeni muone jinsi tanganyika itakavyo adhirika.utaanza alifu kwa ujiti sheeeennnz type.
ReplyDeletemwengine kanifurahisha sana ila kasema ukweli eti anasema haoni faida yeyote ya muungano.nakwambiaje faida yake huyo kikwete kwenda nchi za nje kuomba msaada kwa ajili ya tanzania then akanufaisha kwenu hio sio faida?muungano ni nini?wewe nusu na sisi nusu ndio muungano.au jiulize tangu kuzaliwa taifa hili la tanzania nitajie rais mmoja tu aliyetokea kwetu zanzibar nani?usuje kunitajia ali hassan mwinyi huyo wa huko huko kwenu na aulizwe asili yake kazaliwa wapi?je ingelikuwa wewe uko upande huu wa pili wa muungano ungekubali?au ndio mkuki kwa nguruwe tu?
ReplyDelete