Watazamaji 41,733 walikata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga iliyochezwa jana (Mei 6 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 VIP C, sh. 30,000 VIP B na sh. 40,000 VIP A. Watazamaji 36,980 walinunua tiketi za sh. 5,000 wakati 203 walikata za sh. 40,000.
 
Mechi hiyo ambayo ni moja kati ya saba zilizochezwa siku hiyo kufunga msimu wa 2011/2012 iliingiza sh. 260,910,000. Kila klabu ilipata sh. 62,646,395.85. Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 39,799,830.51 wakati Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilipata sh. 19,908,361.95.
 
Gharama za mechi kabla ya mgawo ni nauli ya ndani ya waamuzi na kamishna sh. 20,000, posho ya kujikimu kwa kamishna sh. 40,000, mwamuzi wa akiba sh. 30,000, gharama za tiketi sh. 8,539,950, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, ulinzi na usafi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.
 
Mgawo wa uwanja ni sh. 19,908,361.95, gharama za mechi sh. 19,908,361.95, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 9,954,180.97, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 1,990,836.19 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 10,467,324.78.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 07, 2012

    I see huo mgao umekuwa mkubwa mno.
    hadi BMT nao wanachukua mgao alafu wanacho kifanya hakuna kitu
    Mdau Fidel

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 07, 2012

    mimi nazani kukuza mpira wetu hayo mapato na waamusi wa mpira wagapate kipande kinuno nao, si issue kabisa kiwango wanachopata

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 07, 2012

    TFF-Mil.260.9 zimewachanganya hadi mkasahau kuwashukuru Mashabiki/watazamaji waliojitokeza kuangalia mechi,hao ndiyo wadau wakuu.

    Na mimi naomba mgawo(nasema tu)

    David V

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 07, 2012

    Makato ni mengi mno, gharama wanazoingia viongozi wa timu ni nyingi sana inabidi ipatikane njia ya kubakiza fedha zaidi ktk timu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2012

    Hayo malipo ya waamuzi na kamishna mbona kiduchu sana jamani?
    Kwa hali hii mtu akihongwa atakataa kweli?
    TFF angalieni viwango hivi ni vidogo sana hasa ukizingatia hali halisi ya upandaji wa gharama ya maisha na risk wanayokutana nayo waamuzi hawa.
    Hivi marefa hawana chama cha kulisemea hili?Inashangaza kama hawasemi lolote katika hali kama hii.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 07, 2012

    Naomba kueleimishwa hayo malipo yanayoenda kwa wachina ni kwa ajili ya nini? Wao kazi yao si kujenga uwanja ambayo tayari kuna fungu wanapata huko?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 07, 2012

    Kwa kweli hawa marefarii wanaonewa sana. Yaani mtu anayepewa jukumu zito la kuchezesha mechi kama ya Simba na Yanga anapata posho ya 20,000? mmmh jamani tuwe serious kidogo. sasa huyu akipewa milioni moja hataua upande wa pili?

    Mdau HK.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 07, 2012

    Mgao bado unazidhoofisha club husika.Wao ndo wenye huduma kubwa kwa mambo mengi.

    Vilabu vinajukumu lakuwalipawachezaji,kumlipa kocha,gharama za kambi,usafiri kwa wachezaji naviongozi.

    Serikali ilisema inajenga uwanja kumbe wachina wanalipwa na mechi!!!!

    Club jengeni viwanja vyenu mupunguze gharama zisizo za msingi.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 07, 2012

    kwa mtu mwenye biashara inayomfanya achapishe maelfu ya tiketi kila wiki Sh200/- kwa kila tiketi ni bei mbaya sana. Huwezi ukachapisha tiketi 40,000 ukapewa bei hio, si bora mnunue mashine zenu wenyewe?

    Che

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...