Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Ltd, Henry Machoke (wa pili kulia), akikabidhi mifuko 100 ya saruji kwa Kaimu Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dar es Salaam (Serikali za Mitaa), Method Mkoba ikiwa ni msaada uliotolewa na shirika hilo kupitia kitengo cha huduma kwa jamii kwa ajili ya wahanga wa mafuriko wanaoishi katika kambi ya Mabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kutoka (kushoto) ni Mwenyekiti wa Wahanga hao, Khalid Msuya, Meneja Masoko wa NIC, Adelaida Muganyizi na (Kulia) ni Ofisa Masoko Mwandamizi wa NIC, Elisante Maleko.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Ltd, Henry Machoke (wa pili kulia), akifafanua jambo baada ya kukabidhi mifuko 100 ya saruji kwa Kaimu Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dar es Salaam (Serikali za Mitaa), Method Mkoba (wa tatu kushoto), ikiwa ni msaada uliotolewa na shirika hilo kupitia kitengo cha huduma kwa jamii kwa ajili ya wahanga wa mafuriko wanaoishi katika kambi ya Mabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kutoka (kushoto) ni Mwenyekiti wa Wahanga hao, Khalid Msuya, Meneja Masoko wa NIC, Adelaida Muganyizi na (Kulia) ni Ofisa Masoko Mwandamizi wa NIC, Elisante Maleko.
Kumbe NIC bado ipo, ni moja kati ya mashirika machache yaliyobaki aliyoanzisha baba wa taifa.
ReplyDeletebaba deborah fatukobonye upo......
ReplyDeleteNIC HONGERENI, KUMBE BADO MNA UKWASI MZURI KUFIKIA KUTOA MISAADA, MBONA BASI HAMTULIPI BIMA ZETU ZILIZOIVA (MATURE) MUDA MREFU. BIMA TUMEANZA KULIPIA KTK MIAKA YA 1980s ZIMEIVA 2005 HADI LEO HATUJALIPWA, MPAKA SASA PESA YENYEWE HAINA THAMANI KULINGANISHA NA HIYO MIAKA. JITAHIDINI KULIPA KILA BIMA ILIYOIVA. AHSANTENI.
ReplyDelete