Wadau wapendwa,
Hivi tunavyoongea kuna watu wana kamchezo ka kutafuta password za email za watu na kutaka kufanya ndivyo sivyo. Wamejaribu kulamba password ya ankal bila mafanikio na sasa wanatumia email ya uwongo kujaribu kuwasiliana na wadau wangu, kama inavyoonesha juu.
Jihadhari na ujumbe wa aina hii katika TWITTER kwani ukiwajibu tu ama ukifungua link waliyokupa, na kompyuta yako haina kinga, ujue umekwisha. Msisitizo hapa ni kwamba ukipata ujumbe wa TWITTER aina hii achana nao na badili password yako haraka sana. Hakikisha umeweka japo tarakimu moja ama mbili katika hiyo password yako. Inasaidia
- Michuzi
ankal jana nimepata DM ya twitter kwa user name yako halafu ilikua usiku wa manane..imagine nilistukaje!
ReplyDeleteMZEE JANA USIKU NILIPOKEA MSG YAKO, NIKAHISI KUNA KITU....!! it happens hawkers pole Br Ankal - na pole pia na Bwawa letu la Maini ngoja tuone jioni hii kama tutalipiza....!! mchana mwema.
ReplyDeleteMUSWAADA WA KATIBA MPYA:
ReplyDeleteInabidi tuwe na Katiba inayokwenda na wakati pia iliyo kuwa sambamba na kasi ya maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.
Ili tuwe na nafuu na mustakabali mzuri masuala ya namna hii yapatiwe mwelekeo ktk katiba mpya na kuingizwa kama sehemu yake.
Kama anavyoripoti Ankali juu ya Udukuzi wa hatari aliofanyiwa!