Basi la abiria la Kampuni ya Muro Investment, lenye nambari za usajiri
Mmoja wa wahusika wa basi hilo alidai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya umeme iliyotokea katika gari hilo. Inadaiwa kuwa gari hilo lilipata hitilafu katika taa na walipofika mjini Morogoro walifanyia marekebisho na kuendelea na safari na walipofika maeneo hayo ya Maseyu likashika moto.
Magari yakipita pembeni ya basi hilo lililokuwa likiteketea kwa moto na hapakuwa na askari wala magari ya zima moto yaliyoweza kuwahi kufika na kuzima moto huo ulioliteketeza basi hilo kabisa.
Wakazi wa Maseyu na wasafiri wakiangalia basi hilo likiteketea kwa moto.
Hili basi lilikuwa na matatizo tangu ijumaa ya tarehe 4..Mi nilikuwa msafir na basi la Lucky Star kutoka Mwanza Ticket No 3181(ni kampuni moja na Princess Muro)na lenyewe likutokea Mwz..kufika Misungwi boc anapiga simu "Tufaulishwe'from lucky star to princess muro kisa tilikuwa wachache ilhal tumelipa elf 45..(princess Muro nauli ni 35,000)..Tukakataa.so wakaenda na basi lao likiwa na matatizo ,kioo kina crack,nk..na mashahidi ni madereva wa Lucky star ambao walikuwa wanaongea live kwamba hilo basi lina matatizo..Ushauri wangu wa bure kwa wamiliki wa mabasi,kama hamuwezi kuyafanyia service magar yenu ni bora muache biashara kuliko kuweka roho zetu rehani kwa maslah yenu na ubahili wenu.
ReplyDeleteMdau wa kwanza hata mimi nilikuwa najiuliza hivi haya mabasi huwa yanafanyiwa service au kuchekiwa kisawasawa?
ReplyDeleteJamani musihatarishe maisha yetu kwa sababu ya faida za muda mfupi. Kila kazi ina ethics zake na wamiliki munatakiwa kufuata hayo.
Jamani sio Hilo tu sisi tumesafiri na basi la sumry tarehe 9/5/2012 kwa ticket namba 31941kutokea mwanza kwenda dar kwa kweli tulifika kwa neema ya MUngu Kwani tokea tunaondoka nyegezi lilikuwa limechomoka propela huko chini tumeharibikiwa mara mbili misigiri na manyoni na kutufanya tulale kwenye basi na kufika kesho yake. Hivi kweli tunapishana na mtu aliyetoka Kampala? Wamiliki wa vyombo vya usafiri kuweni makini mnahatarisha maisha ya watanzania kwa tamaa zeni. Mimi sipandi tena mabasi haya ya sumry kuelekea kanda ya ziwa
ReplyDeleteEeeh Mungu tunakuomba umsaidie mmiliki wa mabasi ya Scandinavi arudi uwanjani na kutupatia huduma saaaafi ya usafiri. Mara nyingi najiuliza huyu mmiliki lipi lilimfika hakuna basi linaweza fikia huduma zake. Mwaka jana nilibahatika kufika uingereza nikagundua huyo mmiliki wa scandinavia alishapita mitaa hii akaona style ya kuendesha mabasi, huduma za makonda nk. Jamani makonda wa scand walikuwa wasafi na wana lugha nzuri sana lakini hawa wengine hata waige vp hawawezi makonda wanatukana ovyo hawana ustaarabu ni wachafu nk. Nakumbuka scand tuliwahi fika mahali dereva akaona jiwe kubwa barabarani ambalo labda lingeweza kuleta ajali kwa hao wengine wasiojali njiani alisimama akamwambia konda akalitoe so sweet. EWE MMILIKI WA SCAND POPOTE ULIPO UJUE TUNAMISS SANA HUDUMA YAKO HATA UKISEMA NAULI NI KUBWA TUTAJITAHIDI TUPANDE TUKIJUA TUTAFIKA SALAMA KULIKO KUPANDA VYA BEI NAFUU HALAFU ROHO MKONONI
ReplyDelete